Samahani sana August kwa kutumia neno damn!,nimegundua halikuwa zuri pale..sorry ila bado siamini kuwa kuna usafi wowote CCM. August tuwaze kuiondoa CCM, hakuna cha uafadhali humo wala justification yeyote.
Kwa kifupi, katika zama hizi za vyama vingi , kiongozi yeyote wa CCM anayejiona msafi ni mnafiki na mwongo.Kubaki CCM ni kutaka kula, marupurupu na vijisenti fulani.Hamna mwenye uchungu wa taifa, ndio maana hatujawa na akina Morgan Tsavangirai bado.
Kubaki ndani ya system ya CCM , huku ukisema wewe ni msafi , hali ukijua huwezi kufanya lolote lile, ama sivyo watakukolimba , chifupa n.k....Nape naye yumo humo humo.
Sina maana wahame chama!!! wakijitokeza wawili watatu, waseme tunajivua uanachama wa CCM kwa ni hatujaridhika na jinsi inavyopafom, nchi itataharuki, wananchi wataamka!, nchi itatikisika, lakini watakuwa mashujaa, HAWAPO HAO!!!! tunalala tunaamka tunapiga kelele -UVCCM!!!!!
Hivyo basi usalama pekee ni kuwa mbali na CCM na kurusha makombora ya mbali.Wengi wana CCM, tumewaona wanapiga kelele, na jamii inawatambua , sasa wako kimya, kesho tena wataamka na kupiga kelele.jamii itawaona mashujaa, miaka inaenda , nothing has been done 3 years now, tunaimba CCM na JK, hao mashujaa wako humohumo!!!!
August ni lini unafikiri utatuaminisha kuwa hao waliochaguliwa wanaweza kuleta mabadiliko , kuliko aliyotegemewa kufanya Kikwete aliyechaguliwa kwa 80%????
Kwa nini tusikae chini na kuona kuwa Rais ndiye tatizo?? hivi unapoua nyoka unaangalia mkia??
Kichwa ndio tatizo, kichwa kikielekea kulia mwili wote unafuata hata kama kuna kiungo kilema, kitavutwa tu
Mtu anakaa chini na kuona mabadiliko ya UVCCM ,na kuwa katibu makamba akiondoka basi ndio nchi imeendelea!!!-Kwa namna hii kwa nini magazeti ya udaku yasiwatajirishe akina Shigongo?
Ukishaona jamii inafurahia habari fulani, ambayo imetengenezwa na watawala, ujue jamii hii imechoka, imeonewa imenyanyaswa au imekata tamaa ya kuwa ni jinsi gani watakavyowaondoa watawala, au imekosa mbinu sahihi ya kuwaondoa watawala.Hivyo basi taarifa, habari yeyote ile inayohusu mabadiliko kutoka kwa watawala inawafurahisha, kwani wameshindwa kufanya makubwa.
Sina lengo la kukosoa taarifa wala dataz kama hizi, ila tunapopata dataz hizi, zisitulemaze na kupumzika au kuhema kwa mapumzika, la tujue kuwa kazi iliyopo ni kumuondoa rais, kwa gharama yeyote hata ikilazimu kizazi hiki kuangamia.
let our motto be 'Leave state house JK', akilala, akiamka, akute wimbo huu, akijifanya kufanya anayoyafanya sasa, akute wimbo ni huu huu, kuwa ondoka Kikwete. Akiona tunakuwa excited na matendo yake butu anafurahi na kesho analeta lingine, 2010 hiyi mnampeleka ikulu kama kawa.
Mungu iokoe Tanzania
waberoya