CCM yafanya maamuzi mazito Kamati Kuu?

CCM yafanya maamuzi mazito Kamati Kuu?

Waberoya
Acha ukali mkuu,,,, haya maneno huku kwetu siyo! Tumia lugha laini kidogo,,, hata kama ni haki yako USIMAKE hivyo

Hili ndio tatizo la kusoma post moja moja na siyo thread nzima,
mbona posy yangu iliyopita nimegundua hilo na nimeomba msamaha kwa muhusika?

By the way is this your only comments in this thread?

we need to hear from you! your comments in this matter is highly needed

waberoya
 
Kinana anayepigiwa chepuo ni yupi?.Kinana ninayemfahamu ni fisadi kama mafisadi wengine.Huyu Kinana alidivert msaada wa mashine za kufulia nguo za wagonjwa Mt Meru Hospital akazipeleka kwenye kampuni yake Falcon drycleaner.Miradi yote ya Kinana kaajiri wasomali wenzake wasiojua hata kiswahili.
Kinana anajulikana kwa kufanikisha deal la Loliondo,alilidhalisha jeshi letu wakati huo akiwa waziri wa ulinzi kutumia magari kusafirisha wanyama kwa faida yake binafsi.
Kinana anahusika kwa kiasi kikubwa kuwapatia uraia wakimbizi wa kisomali walioko katika kijiji cha Chogo Handeni.


Mkuu anataka kuweka Ex-soldier mwenzake mhhhh wanajeshi wazamani wamepata sana nafasi za juu tokea muungwana ameingia madarakani labda anataka kutawala kijeshi kuanzia chamani hadi serikalini..

Ushi
 
pixel_white.gif


5.jpg


10.jpg



Operations
Tanzania
tanzania.gif


Mainland Area:945,087 Square Miles Population:Approximately 37 million Government😀emocratically elected republic Untapped Potential
Tanzania has been intermittently explored over the last 50 years with most multinational petroleum companies being present, at one time or another. So far only 35 exploration and development wells have been drilled in 280,000 square kilometres of hydrocarbon potential sedimentary basins.

Doing Business in Tanzania
The Government of Tanzania is encouraging the oil & gas upstream sector to produce local resources to reduce Tanzania’s reliance on imported petroleum products. Artumas management has established strong relationships with the highest level government officials in East Africa through the Company’s continuing commitment to its gas-to-electricity business plan. These relationships, combined with the Company’s knowledge of the region and its ability to address some of the energy challenges there, allow Artumas to operate successfully in the area.

Investment Climate - Tanzania offers:
  • Competitive Investment Climate
  • Large Potential Market
  • Abundant Natural Resources
  • Infrastructure Facilities
  • Peace and Stability
  • Fiscal Governance
  • Investment Guarantees
  • Transparent Investment Laws
  • Investment Incentives
OverviewMnazi Bay Concession Mtwara Energy Project Off-Take Gas Markets

tanzania.gif


Hapo juu ni kuhusu Artumas...Naona Mrope na Kinana hawamo humo tena...Inaelekea waliufuatilia ule mjadala..Lakini bado tunaweza kuona kama miradi hiyo inawanufaisha wananchi ama la.

NB:Kama kuna wenye data za mikataba hiyo waweke hapa.
 
Tatizo langu ni kuwa yote haya yanafanyika kwa lengo moja tu ambalo ndio limekuwa lengo kuu la kisiasa la CCM yaani kulinda nafasi yake kiutawala na sio kujenga chama ambacho kutawaendeleza watanzania kisiasa, kijamii na kiuchumi....

Hata hivyo kitendo cha kuwapa Wazanzibari UENEYEKITI wa UVCCM (meaning CCM future) ni muhimu sana kwa sasa kwa mustakabali wa kujenga kuaminiana kati yetu lakini pia ni muhimu kwa kuhakikisha MAFISADI hawatumii kura za Zanzibar kumuondoa 2010

Suala la kuwa MAFISADI wameshindwa kwa kuwaondoa hao tunaodhani kuwa ni wagombea wao yaani Beno Malisa kama Kubenea na FMES wanavyoamini na Hussein Bashe ambaye ndiye haswa mgombea wa FISADI Rostam Aziz (sina uhakika na mkono wa LOWASSA hapa), sidhani kama ni kweli wao MAFISADI ndio walioshindwa. Actually kwa ninavyojua ugombea wa BENO MALISA ulivyo na mahusiano yake na MAFISADI tangia alipokataa ufadhili wao wakati wa kugombea NEC hivi karibuni ni wazi MAFISADI ndio walioshinda.....

Chondechonde JK asijipige bao lingine kwa kumchagua POLITICAL MERCENARY Mwakyembe kama katibu mkuu kwani hapo atakuwa ndio amehakikisha ushindi wa MAFISADI dhidi yake. Ukweli ni kuwa wapo tayari kwenda na MWAKYEMBE kumtumia mwaka 2010 ili kumuondoa JK ambaye wanamuona ni mtu asiyeaminika na aliyeonyesha kutotabirika to their cause (suppresing opposition and internal party dessenting voices na pia kulinda maslahi yao kiuchumi).....Chonde JK asijivike kitanzi cha Mwakyembe ama yeyote wa aina yake.....

Idumu Tanzania yetu....

Tanzanianjema
 
Samahani sana August kwa kutumia neno damn!,nimegundua halikuwa zuri pale..sorry ila bado siamini kuwa kuna usafi wowote CCM. August tuwaze kuiondoa CCM, hakuna cha uafadhali humo wala justification yeyote.

Kwa kifupi, katika zama hizi za vyama vingi , kiongozi yeyote wa CCM anayejiona msafi ni mnafiki na mwongo.Kubaki CCM ni kutaka kula, marupurupu na vijisenti fulani.Hamna mwenye uchungu wa taifa, ndio maana hatujawa na akina Morgan Tsavangirai bado.

Kubaki ndani ya system ya CCM , huku ukisema wewe ni msafi , hali ukijua huwezi kufanya lolote lile, ama sivyo watakukolimba , chifupa n.k....Nape naye yumo humo humo.

Sina maana wahame chama!!! wakijitokeza wawili watatu, waseme tunajivua uanachama wa CCM kwa ni hatujaridhika na jinsi inavyopafom, nchi itataharuki, wananchi wataamka!, nchi itatikisika, lakini watakuwa mashujaa, HAWAPO HAO!!!! tunalala tunaamka tunapiga kelele -UVCCM!!!!!

Hivyo basi usalama pekee ni kuwa mbali na CCM na kurusha makombora ya mbali.Wengi wana CCM, tumewaona wanapiga kelele, na jamii inawatambua , sasa wako kimya, kesho tena wataamka na kupiga kelele.jamii itawaona mashujaa, miaka inaenda , nothing has been done 3 years now, tunaimba CCM na JK, hao mashujaa wako humohumo!!!!

August ni lini unafikiri utatuaminisha kuwa hao waliochaguliwa wanaweza kuleta mabadiliko , kuliko aliyotegemewa kufanya Kikwete aliyechaguliwa kwa 80%????

Kwa nini tusikae chini na kuona kuwa Rais ndiye tatizo?? hivi unapoua nyoka unaangalia mkia??
Kichwa ndio tatizo, kichwa kikielekea kulia mwili wote unafuata hata kama kuna kiungo kilema, kitavutwa tu


Mtu anakaa chini na kuona mabadiliko ya UVCCM ,na kuwa katibu makamba akiondoka basi ndio nchi imeendelea!!!-Kwa namna hii kwa nini magazeti ya udaku yasiwatajirishe akina Shigongo?

Ukishaona jamii inafurahia habari fulani, ambayo imetengenezwa na watawala, ujue jamii hii imechoka, imeonewa imenyanyaswa au imekata tamaa ya kuwa ni jinsi gani watakavyowaondoa watawala, au imekosa mbinu sahihi ya kuwaondoa watawala.Hivyo basi taarifa, habari yeyote ile inayohusu mabadiliko kutoka kwa watawala inawafurahisha, kwani wameshindwa kufanya makubwa.

Sina lengo la kukosoa taarifa wala dataz kama hizi, ila tunapopata dataz hizi, zisitulemaze na kupumzika au kuhema kwa mapumzika, la tujue kuwa kazi iliyopo ni kumuondoa rais, kwa gharama yeyote hata ikilazimu kizazi hiki kuangamia.

let our motto be 'Leave state house JK', akilala, akiamka, akute wimbo huu, akijifanya kufanya anayoyafanya sasa, akute wimbo ni huu huu, kuwa ondoka Kikwete. Akiona tunakuwa excited na matendo yake butu anafurahi na kesho analeta lingine, 2010 hiyi mnampeleka ikulu kama kawa.

Mungu iokoe Tanzania

waberoya

Nashukuru for your appology, basi sisi wote ni ndugu moja na tanzania ni nchi yetu, ukiwa ccm au nje ya ccm etc, lengo ni moja kujenga nchi.
asante kwa wote wanaochangia hii mada na nyingine.
 
Mwezi machi mwaka huu katika pita pita yangu humu ndani JF nilikumbana na maneno yafuatayo yaliyoandikwa na Kitila Mkumbo akimjibu Mwanakijiji, nanukuu.

"Ni vizuri sana kufikiri kwamba CCM itaanguka kutoka ndani na itaangushwa na wana ndani wenyewe. This is a belief (I hope it is not a misconception or a myth) like any other belief kama zile za kwangu, and it is fine to think so. Tatizo langu hapa ni impact ya imani hizi katika struggles ambazo tumeamua kwenda nazo. Mtu akisoma hii post yako ya sasa anaweza kupata picha kwamba mimi (na wengine bila shaka) na wewe tuna lengo moja lakini tunatofautiana kimkakati. Lakini hii ni kama mtu atakwenda deep na sio asome maandishi yako from its face value,which is the case with the majority of our readers. Sasa maanake ni kwamba imani yako haiwi tu imani bali pia misconception ambaye inawachanganya wananchi ambao wameanza kushika kasi ya kuondokana na umateka wa CCM. Maandishi yako yanatoa picha kwamba CCM bado ndicho chama kinachostahili kuongoza madamu kitaamua kubadilika.

Rejea makala yako ya jana kwenye Tanzania Daima. Umekariri maandishi ya Mwl Nyerere pale aliposema kwamba bila CCM madhubuti nchi itayumba na umeondoka nayo as if this is absolute truth bila kuyaweka maandishi haya in context. Lakini sote tunajua kwamba katika mfumo wa vyama vingi chama kinachotawala kikiyumba haina maana kwamba nchi inayumba. Kinachofanyika hapa ni kwamba kikiyumba wananchi wataachana nacho na uchaguzi ukija watakichagua chama kingine lakini nchi inaendelea kusonga mbele.Huu ndio ukweli duniani kote. Hakuna nchi iliyowahi kuyumba eti kwa sababu chama tawala kiliyumba; vyama tawala huwa vikishindwa kutawala huwa vinafukuzwa madarakani kwa njia ya kura.

In contrast, maandishi yako yanatoa picha kwamba Tanzania haiwezi kusimama bila CCM, which, I believe, is 200% wrong. Huu ndio ambao mimi naita ni umateka wa CCM. Ni kama vile mlevi wa pombe au madawa ya kulevya anayeamini hawezi kuishi bila hayo madawa. Lakini CCM sio dini yetu wala madawa yetu ya kulevya, kama wanayumba na wameshindwa kutawala, wajibu wetu ni kuwaambia wananchi ukweli huo ili watumie ufahamu wao kuchagua chama kingine na wala sio kuwachanganya kwa kuwaambia kwamba bila CCM imara nchi itayumba. Na wala sisi tunaotaka mabadiliko hatupaswi kuwa kama mafisi kwa kuwavizia CCM waangushe mkono kwa baadhi yao kukitema chama chao ndipo tupate mwanga wa mabadiliko. Tumesubiri wadondeshe hiyo mikono for the past 15 years na hatujaona ikidondoka lakini hatuwezi kusubiri CCM wagawanyike ndipo nchi yetu ipate uponyaji. Ndio maana nasema kama kweli tunataka mabadiliko there is very little room for a short cut; we must be prepared for the difficult struggle as other nations have done, and we have to tell our people as such badala ya kuwapa false impression.

Hii ya kuuma na kupuliza haitufikishi popote wala hatutaweza tule kakeki ketu halafu tuwe nako wakati huohuo, hii hapana, haiji kabisa".
Mwisho wa kunukuu.


Nachukua fursa hii kumpongeza Ndugu Kitila kwa ujumbe huu mzito alioutoa baada ya kikao cha CCM Butiama, Mkoani Mara. Miezi miwili baadaye nilijiunga na JF na huu ujumbe wa Kitila ulichangia sana uamuzi wangu huo.

Ningependa kuongezea kuwa wengi humu ndani tunao uchungu wa kweli na taifa letu tunalolipenda, Tanzania. Pia ukitoa tofauti zetu za kiitikadi inawezakana tunakubaliana kwa mengi tu kuhusu hatma ya nchi na namna ya kujinasua kutoka mikononi mwa wakoloni weusi ambao ni ndugu zetu na marafiki zetu. Ujasiri wa kutetea unachokiamini huonekana hasa pale unapokuta kuwa wabaya wako ni hao hao unaoishi nao, unakula nao, unalala nao n.k. - yaani kikulacho kimo nguoni mwako. Tofauti kubwa ni namna ya kupambana na watu kama hao ambao wengine ni kaka zetu, dada zetu, baba na hata mama zetu.

CCM kwa upande wake imejenga na kujizatiti kwenye falsafa ya kulindana na kwa msingi huo ama wewe ni moja wao au haupo nao. Baada ya miaka mingi hii tabia imekua na kukomaa kiasi cha kufunga milango yote ya kujirekebisha ndani yake. Inawezekana kuna kadirisha kadogo bado kako wazi kanakoingiza hewa safi humo na njia ya kujikwamua ni kujipenyeza kwa kutumia hako kadirisha sasa kabla hujaelemewa zaidi. Yeyote yule anayeota ataweza kuisafisha hii hewa akiwa humo ndani anajidanganya - hii hewa haisafishiki tena. Utajaribu kupiga kelele kwa muda lakini mwishowe hiyo sumu itakumaliza nguvu.

Kuna waliopanga foleni wakimeza mate waweze kufunguliwa milango wajitome humo ndani lakini ukweli ni kuwa tamaa zao ndizo zinawasukuma. Mkuu Kitila aliyaona hayo mapema na bila shaka anatambua huu mchezo wanaoucheza CCM kutusahaulisha machungu ya maisha yanayotukabili. Nasema na nitarudia bila kuomba msamaha wowote, kuna wanaotumiwa bila kujua na si kwa utashi wao kutuaminisha kuwa wana nia thabiti ya kujirekebisha, la hasha. Wachache tunaokataa hizi mbinu zao chafu tukae tukijua hivi vita si lelemama na kila aina ya silaha itatumiwa. Fisadi hana ndugu wala rafiki ulaji wake unapokuwa hatarini.
 
Kwa wapiganaji,

Sisi tunaopigana hatuangalii nyuma na hatuangalii sana walioshindwa kwa sababu ya unafiki au ufisadi ule ule tunaoukataa kutoka viongozi wetu wa sasa, ambao familia zao ziliwahi kuhusika nao, hasa kule Kiwira.

Sisi tutaendelea kupigana tukitumia akili na busara, knowing kwamba tuko kwenye nchi ambayo rais ni kama mfalme, knowing ni taifa lililojaa wanafiki wenye sura mbili, knowing kwamba ni taifa la wananchi wasiokuwa na msimamo, knowing ni taifa lislokuwa na sheria, na knowing kwamba tunapopigana tunapigania taifa na tutalipwa na Mungu, lakini sio wananchi,

maana pamoja na juhudi zake zote za kutaka kuwaokoa, wananchi walimkataa Mrema, pamoja na juhudi zake zote za kutuamsha na mafisadi tumejionea Dr. Slaa akitukanwa humu kama mjinga, pamoja na juhudi zake zote za kutaka kutuamsha wananchi tumeona Zitto akitukanwa na kurushiwa maneno ya chooni humu kama vile ni fisadi, na wale wale ambao wamebadili rangi tu na sasa wanajaribu kuwaambia wananchi hapa kwamba wana uchungu sana na taifa letu kuliko sisi wengine,

Kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake, binadam hatukuzaliwa sawa, hatukuumbwa sawa, kama tatizo ni kuingia kuna watu hapa wangeshaingia zamani sana, maana kama wewe huoni ndani haina maana kila mwananchi haoni ndani, we are what we are hakuna anything cha kubadilisha kwa maneno ya kulazimishana hapa JF, tumekua huru sasa 45 years na kuna wanaokaribia kupumzika sasa you wonder walikua wapi siku zote hizi?

Naona the game inazidi kunoga sasa anatafutwa Kitila maana so far ana-miss katika the new bandwagon, humu ndani tuna ma-genius wanaoweza kufikiria tu na kujua nani ni fisadi na nani sio, what a geniusess, you wonder kwa nini hawako Tukukuru, au our anti-corruption squad kwa nini hawako huko ili wapeleke huu u-genius wao? Maana humu JF ambapo hatujuani wao wana akili ya kuweza kujua kwa kusoma maandishi tu ya wananchi wengine wasiokubaliana na mawazo yao kwamba wanapenda ufisadi,

Wote humu ndani ni lazima tukubali mawazo yao, otherwise tukipingana nao tunakua mafisadi na wao ndio mashujaaa wa kulikomboa taifa hili, you wonder nia na madhumuni yao ni nini? Sasa imekua Kitila, the only thing they know ni divide and rule, na siku zote ni lazima wa-dominate kila mtu by any means necessary, ni lazima tukubali tu mawazo yao, ni lazima wote tuchukue amri zao, wao ndio waamue kama tuna akili za taifa letu au hatuna, ni lazima wao ndio waamue,

ninaomba kuwakumbusha kwamba taifa letu hatuwezi kufundishwa na wengine namna ya kulipigania, kwamba nafasi zipo siku zote za kuingia kwa kila mwananchi hakuna anayekatazwa, vidole ingawa ni vya mkono wa binadam lakini kuna virefu na vifupi, so is maisha ya mwanadam, hatukumbwa sawa, urefu wa kamba yangu hauwezi kuwa sawa na wa kamba yako, tusisingizie wananchi wengine maneno ambayo hatuwezi kuya-prove mbele ya jamii, au bila ushaidi,

Tunashukuru Mungu kwamba, wapiganaji tuko wengi, tena kutoka walks za kila aina, na wote tunajuana na kuaminiana na we work together as a team, tumekwua pamoja sasa for at least three years, na tunazidi kushikamana na kusimama imara kwa pamoja, tukilisimamia taifa letu, hatuogopi anybody, hatutishiki na maneno hewa! Tunaelewa mazingara tuliyomo, na tunaelewa wananchi tunaowapigania na tutasimama imara mpaka mwisho bila kuogopa maneno wala vitisho.

Mungu Ibariki Tanzania, na heshima zangu za juu hapa zimuendee Shujaaa Saeed Kubenea, maana ndiye mshindi wa kweli na matokeo ya kikao hiki cha kamati kuu majuzi na jana.


Es! Wazee wa sauti ya umeme, kutoka radio station ya FMES. Mpaka Kieleweke, hakimbii mtu! Wala hakimbiwi mtu!
 
Field Marshall,
Kwa hali ilivyo katika nyakati zetu hizi,hali ya uelewa wa umma,hali ya kuishi katika mfumo wa Chama kimoja kwa miaka 30,hali ya kuwa na katiba isiyokidhi maslahi ya taifa kwa enzi hizi na umaskini uliokithiri mimi naungana na wewe kuwa tuanpiga kelele tu.dalili za hawa watawala kuchaguliwa tena kwa kishindo zipo hiyo 2010 na zitaendelea kuwepo kwa karne hii yote.Madhara ya Nyerere ni makubwa kuliko yote ni kututawala kwa fimbo ya Ujamaa,kuhodhi fikra ma kuwafanya watu wengine wakiishi bila kujitambua,na umma ukabaki na fikra zilizodumaa.

Bila kuondoa huu ugonjwa wa fikra zilizodumazwa kwa kubadili mfumo mzima wa utawala ,kuunda katiba mpya na kuzindua akili za umma zilizolala na kudumaa tutakuwa na CCM hadi mwisho wa karne ya 21,na siyo hivi karibuni.Wengine tutakuwa tumeshakufa na Mungu pekee ndiye anayejua huko mbele watabadika lini hawa Watanzania wa leo.Tuendelee kupiga kelele humu nadani ya forum sisi wenyewe,huko nje mmmmhh kazi ni kubwa!


Mkuu Al-danaby,

Heshima yako mkuu, naomba kukwambia kwamba uko right kwa 100%, na tupo ukurasa mmoja.

Wengine wote ndugu zangu naomba ku-retreat mapka kesho, the last three days zilikuwa ngumu sana na vita ya mafisadi, lakini I promise kesho asubuhi tutahabarishana wote huko kwenye e-mail, nyeti ambazo ni za moto bado kuziweka hapa, kama nilivyoahidi! Wote ninao ujumbe wenu, everything is under control!

Ahsante wakuu Wote!
 
.Madhara ya Nyerere ni makubwa kuliko yote ni kututawala kwa fimbo ya Ujamaa,kuhodhi fikra ma kuwafanya watu wengine wakiishi bila kujitambua,na umma ukabaki na fikra zilizodumaa.



This is hard saying Alnadaby, ''madhara ya Nyerere'' ! well ni kweli.

Ninachoweza kumtetea Nyerere ni kuwa alifikiri watu wote wako kama yeye! alijua ametengeneza watu wenye tabia na mawazo kama yeye '' kuwaza taifa lao'' hili ndilo kosa kubwa sana, na imepelekea hayo unayoyasema, madhara yake ni makubwa kuliko maelezo. Hakujua na ninaamini akifufuka leo na kuona hali halisi , atakufa tena kwa presha, jakamoyo, uchungu, potelea mbali hata kujiua! ila naamini mawazo yake yanaishi

Nasema kama wasomi waliotukuka walimshangilia Kikwete mwaka 2005!bila sababu, vipi kuhusu babu yangu aliyeko tukuyu Mbeya, ambaye anaamini kuwa CCM tu ndio wanaotakiwa waongoze??

Kazi ipo, tunayo kubwa sana kuliko maelezo, tufanye nini? na nani afanye? tusipojibu haya maswali CCM watakuwa madarakani miaka mingi sana kama Msekwa alivyowahi kusema!

Mungu tusaidie

waberoya
 
Suala la kuwa MAFISADI wameshindwa kwa kuwaondoa hao tunaodhani kuwa ni wagombea wao yaani Beno Malisa kama Kubenea na FMES wanavyoamini na Hussein Bashe ambaye ndiye haswa mgombea wa FISADI Rostam Aziz (sina uhakika na mkono wa LOWASSA hapa), sidhani kama ni kweli wao MAFISADI ndio walioshindwa. Actually kwa ninavyojua ugombea wa BENO MALISA ulivyo na mahusiano yake na MAFISADI tangia alipokataa ufadhili wao wakati wa kugombea NEC hivi karibuni ni wazi MAFISADI ndio walioshinda.....

Ahsante sana mkuu TZnjema, strong analysis.

Mkulu Halisi,

Cheki PM, fungua bomba inakuja.....!
 
Ahsante sana mkuu TZnjema, strong analysis.

Mkulu Halisi,

Cheki PM, fungua bomba inakuja.....!

Mkuu FMES usinsahau na mimi majita wa watu wa wanakijiji wangu kuni-PM kama kuna habari ya moto mkuu manake madataz yako huwa ya moto kwelikweli.
 
Mkuu FM ES na Wakuu wengine Heshima,
tunasubiri kwa hamu kupata yoyote yatakayojiri ndani ya NEC-CCM.
 
Mkuu wa medani leo ni kikao kile cha nec, tupatie latest mtumishi wa umma.

Masatu, cc huripoti maamuzi yake kwa nec na siyo public, nec yenyewe inaweza kutangaza maamuzi yake na siyo cc.

Hiyo ndiyo ccm yetu, hatutegi bali tunatenda.

Ukubwa ni jaa muungwana.

Mkuu wa medani twende kazi kaka, tupatie yanayojiri sisi tunaohitaji taarifa hizo ili tuhamasike .

2010 tutapambana na aziz abood kama atathubutu kuuvuka ule mto, lakini bado tunahitaji maarifa ya medani toka kwa watu wa kariba yako ili tuijenge nchi.
 
Wakuu heshima mbele sana, ila samahani sana kwa udhuru maana leo nimealikwa kwenye sherehe nzito sana ya ushindi wa Obama inayofanywa na Balozi wa Kenya, ambako ninatakiwa kusoma ka-paper kadogo,

Na baada ya hiyo shughuli ninaelekea kwenye kuselebuka Live na Wenge Musica BCBG (Bece Bejhee), I mean nataka kwenda kuwacheki wakulu kina Jibe Mpiana, Kibense Profeseee, Seke Minyo, Clintooon, na Filipo, ingawa mkulu Afande ametoka, lakini Suvereee jibe Mpiana bado wamo sana,

Kwa hiyo wakuu mijadala iliyo na wema, labda kesho jioni tutakuwa hapa hapa uwanja wa damu Giladi, na ni matumaini yangu kwua kuna watakaoleta dataz za huko ndani, lakini nitajitahidi popote nilipo kujaribu ku-access as soon nikiwa nazo, otherwise kesho jioni nitakua nazo zote in full.

Shukrani Wakuu, Later!
 
Wakuu heshima mbele sana, ila samahani sana kwa udhuru maana leo nimealikwa kwenye sherehe nzito sana ya ushindi wa Obama inayofanywa na Balozi wa Kenya, ambako ninatakiwa kusoma ka-paper kadogo,

Na baada ya hiyo shughuli ninaelekea kwenye kuselebuka Live na Wenge Musica BCBG (Bece Bejhee), I mean nataka kwenda kuwacheki wakulu kina Jibe Mpiana, Kibense Profeseee, Seke Minyo, Clintooon, na Filipo, ingawa mkulu Afande ametoka, lakini Suvereee jibe Mpiana bado wamo sana,

Kwa hiyo wakuu mijadala iliyo na wema, labda kesho jioni tutakuwa hapa hapa uwanja wa damu Giladi, na ni matumaini yangu kwua kuna watakaoleta dataz za huko ndani, lakini nitajitahidi popote nilipo kujaribu ku-access as soon nikiwa nazo, otherwise kesho jioni nitakua nazo zote in full.

Shukrani Wakuu, Later!

Nakuaminia kaka, kila la kheri na sherehe hizoooo
 
...kaka fmes..tunangojea details kaka ..hasa baada ya wajumbe wa halmashauri kuu kumkatalia kikwete live ....kumuengua nimrod mkono..wakimtajia hadi jina la kukata ili mkono abaki[ambalo ni jina la mgombea anayesadikika kumtaka awe chairman wazazi]..thats a face snab to jk..tunategemea kwa mara ya kwanza kusikia veto ya mwenyekiti..leo ..ili kuwanusuru wagombea wake na kumbwaga mkono.......au anaweza kumita mkono na kumuomba awatulize section kubwa ya wajumbe wanaokataa jina lake kuenguliwa[inaaminika mkono si mtu wa mtandawo].....

Uchaguzi huu jk anakuwa makini kuhakikisha watu ambao ana mashaka na uaminifu wao kwake hawapiti na kuingia kamati kuu..ili wasije mbele ya safari wakaleta kanza ya kuzaa mbeki mwingine....

Tunakusubiri mukulu!!!
 
...kaka fmes..tunangojea details kaka ..hasa baada ya wajumbe wa halmashauri kuu kumkatalia kikwete live ....kumuengua nimrod mkono..wakimtajia hadi jina la kukata ili mkono abaki[ambalo ni jina la mgombea anayesadikika kumtaka awe chairman wazazi]..thats a face snab to jk..tunategemea kwa mara ya kwanza kusikia veto ya mwenyekiti..leo ..ili kuwanusuru wagombea wake na kumbwaga mkono.......au anaweza kumita mkono na kumuomba awatulize section kubwa ya wajumbe wanaokataa jina lake kuenguliwa[inaaminika mkono si mtu wa mtandawo].....

Uchaguzi huu jk anakuwa makini kuhakikisha watu ambao ana mashaka na uaminifu wao kwake hawapiti na kuingia kamati kuu..ili wasije mbele ya safari wakaleta kanza ya kuzaa mbeki mwingine....

Tunakusubiri mukulu!!!

magazeti ya leo yameandika vitu vya ajabu ajabu ila ninahisi wanategemea sana jf i break news kama pm unavyododosa.

Mkuu wa medani umetuacha solemba!!!
 
...kaka fmes..tunangojea details kaka ..hasa baada ya wajumbe wa halmashauri kuu kumkatalia kikwete live ....kumuengua nimrod mkono..wakimtajia hadi jina la kukata ili mkono abaki[ambalo ni jina la mgombea anayesadikika kumtaka awe chairman wazazi]..thats a face snab to jk..tunategemea kwa mara ya kwanza kusikia veto ya mwenyekiti..leo ..ili kuwanusuru wagombea wake na kumbwaga mkono.......au anaweza kumita mkono na kumuomba awatulize section kubwa ya wajumbe wanaokataa jina lake kuenguliwa[inaaminika mkono si mtu wa mtandawo].....

Uchaguzi huu jk anakuwa makini kuhakikisha watu ambao ana mashaka na uaminifu wao kwake hawapiti na kuingia kamati kuu..ili wasije mbele ya safari wakaleta kanza ya kuzaa mbeki mwingine....

Tunakusubiri mukulu!!!

Hili linashangaza sana. Mimi nilifikiri baada ya kushinda uchaguzi na hasa ukizingatia sasa hivi ana matatizo makubwa ya kisiasa, JK angekuwa concilliatiry na kuwa-take on board watu serious kama akina Mkono. Kumbe bado anaendeleza yaleyale ya umtandao? Hivi hajui kwamba umaarufu wake hata katika chama chake umeshuka sana? He must be having a very mediocre team of advicers!
 
Hili linashangaza sana. Mimi nilifikiri baada ya kushinda uchaguzi na hasa ukizingatia sasa hivi ana matatizo makubwa ya kisiasa, JK angekuwa concilliatiry na kuwa-take on board watu serious kama akina Mkono. Kumbe bado anaendeleza yaleyale ya umtandao? Hivi hajui kwamba umaarufu wake hata katika chama chake umeshuka sana? He must be having a very mediocre team of advicers!

thanks for your comment, na ni na support unacho sema au kwa kuliona hilo, ila wengine tukiandika hivi, wengine sijui ndio wenye chama au wanajiona kama nchi ni yao au wao wanauchungu saana na nchi kuliko wengine au ndio huluka ya mwanadamu basi wanadai unajifanya genius na blah blah zingine zisizo na maana. Keep it up Bro
 
Back
Top Bottom