CCM yaitisha Kikao Kizito Maalumu cha kamati Kuu

CCM yaitisha Kikao Kizito Maalumu cha kamati Kuu

Ndugu zangu Watanzania ,

Chama cha Mapinduzi chini ya uwenyekiti wa Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Samia Suluhu Hasssan kitakuwa na kikao maalumu na kizito sana cha Kamati kuu.

Ikumbukwe ya kuwa hiki ni kikao cha juu kabisa na chenye kutoa mstakabali wa Masuala mbalimbali ya chama na Taifa kwa ujumla wake.ni kikao ambacho maamuzi yake hutoa Dira na muelekeo wa mambo mbalimbali.

Ndio sababu vikao vya namna hiyo hufautiliwa sana na vyombo mbalimbali vikubwa vya kitaifa na kimataifa.ni vikao ambavyo hata vyama vya upinzani husimamisha shughuli zake zote kwa ajili ya kutenga muda wa kutosha kufuatilia vikao hivi na maamuzi na maazimio yake.

Ni vikao ambavyo huteka anga la siasa za Tanzania pamoja na kuitetemesha nchi,ni vikao ambavyo huteka mijadala yote ya siasa za nchi hii. Ni vikao ambavyo husubiriwa Na watanzania wote. Tukae kwa utulivu tusubiri nini kitajili kutoka huko. Tulizeni mioyo na wala msiwe na presha.View attachment 3083087

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Lucas Mwashambwa katika Moja na mbili, haya utuletee mrejesho yakiwemo maazimio
 
Masauni mda wake unahesabika.
Msiye mpenda anaweza teuliwa ubunge viti maalum na akashika wadhifa wake
 
Duh...!, niliwahi kusisitiza humu kuwa mtu kuwa kichaa sio lazima aokote makopo!, kiukweli kabisa tuna vichaa wengi humu kuliko tunavyojidhania!. I doubt hata kama umewahi kuisoma katiba ya CCM!. Tusilete ushabiki maandazi humu, kikao cha juu kabisa cha CCM ni mkutano mkuu!, nakusubiria kwa hamu ulete huo ushahidi na ukiukosa, nathibitisha humu kuwa wewe ni miongoni mwa waliomo kwenye kundi hili Kuwa kichaa sio mpaka kuokota makopo! Je, Tanzania tuna vichaa wengi kuliko tunavyojidhania!. Mtu unaweza kuwa unajibishana na mtu humu ukijua ni timamu kumbe...
Nakusubiria!.
P
Bora umemtia msumari wa moto, huyo jamaa kiukweli hajitambui
 
baada ya kukamilika kwa ikulu ya chamwino na sgr kufika dodoma tulitegemea vikao vingi vyabrais vingefanyika Dodoma, hivi rais anavyotangatanga simnamchosha au mnababaisha asi concentrate na majukumu na sijui kama akisafiri anabeba na mafaili,
 
Kikao cha majizi ya rasilimali, watekaji na wauaji wa wananchi wasio na hatia, kikao cha waiba kura maarufu wa nchi tena wanajinasibu kuwa na bao lao la mkono, kikao cha mediocre leaders
 
Kikao cha majizi ya rasilimali, watekaji na wauaji wa wananchi wasio na hatia, kikao cha waiba kura maarufu wa nchi tena wanajinasibu kuwa na bao lao la mkono, kikao cha mediocre leaders
Endelea kuweweseka wakati CCM ikiendelea kujenga imani kwa watanzania na kuaminiwa mioyoni mwao mamilioni ya watanzania
 
Back
Top Bottom