CCM yalaani mauaji ya mjumbe wa CHADEMA Ali Mohamed Kibao

Mnawapa pole CHADEMA kwa unafiki mkubwa.

CCM ina mkono wake kwenye haya mauaji yanayoshamiri
 
Ndiyo wahusika
 
Namwona tu anavyojaribu kujiweka mbele. Yeye na Nchimbi suala la kukamatwa kwa akina Mbowe na Lissu. Waliingilia kati mpaka hawa jamaa kuachiliwa. Naona anajisahau. Haoni Mwenyekiti amenyamaza? Au anadhani yeye Makalla ni mkubwa kuliko Mwenyekiti?

Suala la kuuawa Kibao Makalla analaani? Analaani yeye kama nani? Na anasema suala la sijui utu , ubinadamu. Hizi habari aachane nazo. Mtu au binadamu ni mwanaCCM tu hawa wengine ni Fisi tu wanakuwa wameingia zizini. Shurti waondoshwe.

Sijui kama atadumu maana naona anaanza naye kuota mapembe , anaanza kuona naye anaweza zungumza wakati Mwenyekiti yupo ana onesha mapishi mbalimbali.

Inawezekana hawa watu hawashirikishwi haya mambo. Atulie.

Soma Pia: CCM yalaani mauaji ya mjumbe wa CHADEMA Ali Mohamed Kibao
 
Ipo siku tu Mungu atayajibu haya. Fisiem asahv wanahisi hii inchi ni mali yao sasa na wanaamua nan wa kuishi na nan wakufa.
 
Mwenyekiti yuko bize kuonesha mapishi haafu Makalla anajitanguliza mbele mbele
 
Mungu ndiye anayejua ingawa sisi sote kwake tutarejea
 
Siku zote mhalifu Huwa wa kwanza kukikemea kile kitendo kiovu alichokifanya ili aonekane kwenye umma kama ni mtu mwema
 
Wanazuga.
Siyo tu kuzuga ila kejeli mbaya sana. Ni kama ile ya Sativa kupewa fedha wakati walitaka kumuua bado wapo na wanaendelea kuua. Au wanataka kutuambia kuwa Samia hana control na nchi tena? Kuwa kuna kundi la wauaji linaongoza Tanzania na yeye ''ameshikwa mateka'' na kuambiwa asifanye chochote? Siyo ajabu huyu aliyeuawa Samia akatoa rambirambi pia.
 
Haya ndio madhara ya wananchi kutumia muda mwingi kushabikia ujinga badala ya kujadili mambo muhimu ya kitaifa.

Watu wanashabikia mpira siku nzima unategemea nini toka kwao??

Anyways.

Yanga Bingwa tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…