The Khoisan
JF-Expert Member
- Jun 5, 2007
- 16,434
- 14,547
===
CCM YASIKITISHWA KIFO CHA MJUMBE WA SEKRETARIETI YA CHADEMA YATOA POLE.
"Nimeona kwenye Vyombo vya Habari kuanzia asubuhi mpaka sasa nitoe pole kwa Chama cha Chadema kwa kumpoteza mmoja wa Wajumbe wa Sektarieti bwana Ali Kibao nimekuwa nikifuatilia sisi ni vyama vya siasa linapokuja suala la ubinadamu Chama unaweka pembeni, nawapa pole kwa msiba"
"Mimi niombe Jeshi la Polisi likatimize wajibu la kuendelea na uchunguzi wa jambo huo , na katika hili sisi ni binadamu ,utu na ndio mana nimesimama hapa kutoa pole kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi"
Katibu wa NEC-Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa Ndugu Amos Makalla amesema hayo akizungumza na Wananchi wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara .
Soma Pia:
- Ally Mohamed Kibao auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana
- CHADEMA: Mzee Ally Kibao ametekwa na Vyombo vya Ulinzi na Usalama akiwa kwenye basi. Usalama wa Taifa waeleze alipo
- Polisi: Tunachunguza kubaini chanzo na watu waliohusika kumchukua Ally Kibao
- Majibu ya Postmoterm yaonyesha kwamba Mzee Kibao alipigwa sana na kumwagiwa Tindikali
===
Wahuni tu hawa MaCCM. Wao ndiyo wako nyuma ya haya yanayoendelea.