Namwona tu anavyojaribu kujiweka mbele. Yeye na Nchimbi suala la kukamatwa kwa akina Mbowe na Lissu. Waliingilia kati mpaka hawa jamaa kuachiliwa. Naona anajisahau. Haoni Mwenyekiti amenyamaza? Au anadhani yeye Makalla ni mkubwa kuliko Mwenyekiti?
Suala la kuuawa Kibao Makalla analaani? Analaani yeye kama nani? Na anasema suala la sijui utu , ubinadamu. Hizi habari aachane nazo. Mtu au binadamu ni mwanaCCM tu hawa wengine ni Fisi tu wanakuwa wameingia zizini. Shurti waondoshwe.
Sijui kama atadumu maana naona anaanza naye kuota mapembe , anaanza kuona naye anaweza zungumza wakati Mwenyekiti yupo ana onesha mapishi mbalimbali.
Inawezekana hawa watu hawashirikishwi haya mambo. Yeye Amos anadhani polisi wanaamua tu kufanya wanayofanya bila mwongozo? Atulie. Mama anaiponya Nchi. Hii nchi iliharibika sana. Mnaomkwamisha mama mtakiona.
Soma Pia: CCM yalaani mauaji ya mjumbe wa CHADEMA Ali Mohamed Kibao