CM 1774858
JF-Expert Member
- May 29, 2021
- 5,621
- 5,029
Wana jamii forum hii ndio habari kuu mpya toka mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa kuwa Mhe Dkt Emmanuel Nchimbi ndio Mgombea mwezi wa CCM katika Uchaguzi Mkuu Ujao Oct 2025.
Uteuzi na mabadiliko haya yataanza rasmi baada ya mwezi July Bunge litakapovunjwa hivyo Dkt Philip Esdori Mpango na Dkt Emmanuel Nchimbi wataendelea kuwa katika nafasi zao mpaka wakati wa Uchaguzi Mkuu huku Dkt Philip Esdori Mpango yeye atasalia mpaka siku ya kuapishwa kwa Rais na Makamu wa Rais.
===
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameridhia kwa kauli moja kumpitisha Katibu Mkuu wa CCM Taifa Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwa Mgombea mwenza (Makamu wa Rais) kwa Mgombea Urais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu wa 2025.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni mgombea urais, Samia Suluhu Hassan alimpendekeza Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba 2025 baada ya Makamu Wa Rais, Dkt. Philip Mpango kuomba kupumzika.
Soma:
- Breaking News: - Uchaguzi 2025 - Dr. Mpango aomba apumzike kuwa Makamu wa Rais, Rais Samia aridhia ombi hilo
- Wajumbe Mkutano Mkuu CCM wapitisha Rais Samia, Dkt. Mwinyi kugombea Urais 2025
Dkt. Nchimbi alichukua nafasi iliyoachwa wazi na Daniel Chongolo aliyejiuzulu Novemba 29, 2023.
Rais Samia amempendekeza Dk Nchimbi leo Jumapili, Januari 19, 2025 katika mkutano mkuu maalumu jijini Dodoma.