Pre GE2025 CCM yamchagua Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza katika Uchaguzi wa Oktoba 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mtabiri tambi tambi anasema milio itaanza mwishon mwa mwez huu na mwanzon mwa mwez Feb..
Mamaee january
 
Watu watofautishe Dr Nchimbi na Dr Nchemba Jamanii. Leo Songea huko ni kugalauka mpaka pakuche.

**Jokate Mwegelo ajipange
 
Naam, Nchimbi ni mwanasiasa kwelikweli. Ni mtulivu sana, anaijua nchi yetu na matamanio ya watanzania
 
Sjui nataka kusema Nini ila ya jiwe maybe yakajirudia one term prez ?

Anyway wazee wa mikakati wanamuingiza kingi mbaya sana

M.A.P IN ADVANCE

Mbichi Alianza ongelewa Toka yupo Kwa kina VINNI
 
Hakika hili ni jembe haswa! Wapinzani kazi wanayo huku Rais Samia huku Dk Nchimbi
 
Mambo yanakwenda kwa kasi ndani ya chama dola kongwe CCM kuelekea 2025
 
Bado sijaelewa kwanini imekua mapema sana. Au makundi yalishaanza chinichini wameamua wayawahi?
Kuna chenga ya mwili watu wamepigwa Dodoma jana hawaamini likichotokea. Samia hatari sana🀣🀣🀣
 
πŒπŠπ”π“π€ππŽ πŒπŠπ”π” πŒπ€π€π‹π”πŒ 𝐖𝐀 π‚π‚πŒ π“π€πˆπ…π€ π–π€π‘πˆπƒπ‡πˆπ€ πƒπŠπ“. ππ‚π‡πˆπŒππˆ πŠπ”π–π€ πŒπ†πŽπŒππ„π€ πŒπ–π„ππ™π€ 𝐖𝐀 π‘π€πˆπ’ πƒπŠπ“. π’π€πŒπˆπ€

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameridhia kwa kauli moja kumpitisha Katibu Mkuu wa CCM Taifa Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwa Mgombea mwenza (Makamu wa Rais) kwa Mgombea Urais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu wa 2025.
 

Attachments

  • VID-20250120-WA0014.mp4
    22.5 MB
Nyerere, Mkapa, Magufuli, Mpango na Nchimbi ni baadhi yao.

Julius Nyerere, rais wa kwanza wa Tanzania, ambaye alipenda kuwa padre, alisoma katika Shule ya White Fathers Missionary school huko Musoma na baadaye kufundisha St. Mary High School. Wakati akisoma, alijihusisha sana na Kanisa na baadaye aliziandika Injili zote 4 kwa mfumo wa mashairi.

Benjamini Mkapa rais wa tatu wa Tanzania, alisoma katika Seminari ya Kigonsera, Ndanda akipenda kuwa padre, lakini aliona aende kwenye masomo mengine ya mambo ya kidunia.

John Magufuli rais wa tano wa Tanzania, alisoma katika Seminari ya Katoke, Biharamulo Kagera, lakini aliondoka kabla ya kumaliza kutokana na changamoto mbalimbali zilizomkumba akiwa shuleni.

Philip Mpango, makamu wa rais wa JMT, naye alikuwa akisoma katika Seminari ya Ujiji na Itaga, Tabora na pia alifikia uamuzi wa kutoendelea na masomo ya upadre.

Na sasa, mgombea mwenza wa CCM Emmanuel Nchimbi ni ex-seminarian katika Seminari Ndogo ya Mitume wa Yesu, Uru mkoani Kilimanjaro.

Wapo viongozi wengi sana nchini waliosoma seminari za Kanisa Katoliki na wametoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya nchi. Hongera kwa Kanisa Katoliki na mtandao wa shule za seminari kwa kuwa viwanda vya kuzalisha viongozi wakubwa katika Taifa letu.
 
Sikua nafahamu hili, So Nchimbi ni mpango maalumu wa Kanisa Katoliki au Ni Coincidence????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…