Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwani U-waziri Mkuu unapatikanajeUtakuwa ni ufalla wa hali ya juu utoke Uwaziri mkuu urudie ubunge...ujinga mtupu
Alimalizia term yake pekeeMbona lowassa aliendelea kua mbunge wa monduli mpaka 2015
Tanzu ni nn?A
Act ni chama Tanzu cha ccm
Nchimbi atatimiza unabiiKwahiyo likitokea la kutokea huyo Nchimbi ndiyo anakuwa Raisi wa Tanzania
Hakika hili ni jembe haswa! Wapinzani kazi wanayo huku Rais Samia huku Dk Nchimbi===
Wana jamii forum hii ndio habari kuu mpya toka mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa kuwa Mhe Dkt Emmanuel Nchimbi ndio Mgombea mwezi wa CCM katika Uchaguzi Mkuu Ujao Oct 2025.
Uteuzi na mabadiliko haya yataanza rasmi baada ya mwezi July Bunge litakapovunjwa hivyo Dkt Philip Esdori Mpango na Dkt Emmanuel Nchimbi wataendelea kuwa katika nafasi zao mpaka wakati wa Uchaguzi Mkuu huku Dkt Philip Esdori Mpango yeye atasalia mpaka siku ya kuapishwa kwa Rais na Makamu wa Rais.
===
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameridhia kwa kauli moja kumpitisha Katibu Mkuu wa CCM Taifa Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwa Mgombea mwenza (Makamu wa Rais) kwa Mgombea Urais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu wa 2025.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni mgombea urais, Samia Suluhu Hassan alimpendekeza Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba 2025 baada ya Makamu Wa Rais, Dkt. Philip Mpango kuomba kupumzika.
Soma: Breaking News: - Uchaguzi 2025 - Dr. Mpango aomba apumzike kuwa Makamu wa Rais, Rais Samia aridhia ombi hilo
Dkt. Nchimbi aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM Januari 15, 2024 katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho kilichofanyikia Unguja, visiwani Zanzibar.
Dkt. Nchimbi alichukua nafasi iliyoachwa wazi na Daniel Chongolo aliyejiuzulu Novemba 29, 2023.
Rais Samia amempendekeza Dk Nchimbi leo Jumapili, Januari 19, 2025 katika mkutano mkuu maalumu jijini Dodoma.
Wanachochea moto CHADEMA ili kufunika moto ulioko kwao.Bado sijaelewa kwanini imekua mapema sana. Au makundi yalishaanza chinichini wameamua wayawahi?
Hata Kinana alijiuzulu… Utaratibu wa Kuomba kupumzika ni mzuri kuliko wa kusubiri kuondolewahaha hata J.Ndugai akiomba kujizulu pia …
Ameomba kupumzikaMpango imekuaje tena?
Kuna chenga ya mwili watu wamepigwa Dodoma jana hawaamini likichotokea. Samia hatari sana🤣🤣🤣Bado sijaelewa kwanini imekua mapema sana. Au makundi yalishaanza chinichini wameamua wayawahi?
Kwani nani anatisha?Anahofia uhai wake.
Ma CCM haishindwi kuua kwa ajili ya madaraka.
Pambana na mambo ya CHADEMA KwanzaCCM haina viongozi kwa sasa.
Halafu huu ndio utaratibu?
HIiyo heading haika sawa.
Sikua nafahamu hili, So Nchimbi ni mpango maalumu wa Kanisa Katoliki au Ni Coincidence????Julius Nyerere, rais wa kwanza wa Tanzania, ambaye alipenda kuwa padre, alisoma katika Shule ya White Fathers Missionary school huko Musoma na baadaye kufundisha St. Mary High School. Wakati akisoma, alijihusisha sana na Kanisa na baadaye aliziandika Injili zote 4 kwa mfumo wa mashairi.
Benjamini Mkapa rais wa tatu wa Tanzania, alisoma katika Seminari ya Kigonsera akipenda kuwa padre, lakini aliona aende kwenye masomo mengine ya mambo ya kidunia.
John Magufuli rais wa tano wa Tanzania, alisoma katika Seminari ya Katoke, Biharamulo Kagera, lakini aliondoka kabla ya kumaliza kutokana na changamoto mbalimbali zilizomkumba akiwa shuleni.
Philip Mpango, makamu wa rais wa JMT, naye alikuwa akisoma katika Seminari ya Ujiji na Itaga, Tabora na pia alifikia uamuzi wa kutoendelea na masomo ya upadre.
Na sasa, mgombea mwenza wa CCM Emmanuel Nchimbi ni ex-seminarian katika Seminari Ndogo ya Mitume wa Yesu, Uru mkoani Kilimanjaro.
Wapo viongozi wengi sana nchini waliosoma seminari za Kanisa Katoliki na wametoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya nchi. Hongera kwa Kanisa Katoliki na mtandao wa shule za seminari kwa kuwa viwanda vya kuzalisha viongozi wakubwa katika Taifa letu.