CCM yamfukuza uanachama Bernard Membe, Kinana apewa karipio kali huku Makamba akitoka salama

Tunasema Siku zote, hivi vyama Ni Mali ya watu badala ya taasisi, membe kafukuzwa uwanachama kwa sababu ya kutaka kumpinga jpm ndani ya ccm kugombea urais sio kingine.
 
Kwa sasa CCM inaabudu MTU, tena jpm..huo ndo ukweli.
 
Hapo CCM wamekosea kweli, hao watu walitakiwa wawekwe ndani (mahabusu) kwa kipindi kisichojulikana mpaka hapo rais atakapoapishwa, haiwezekani watu wanatukana mkuu wa nchi eti adhabu ni kuwafukuza chama.😎 😎 😎 😎
 
Kufuatia kwa kufukuzwa chamani Bernard Membe kwa makosa mbali mbali ya kanuni ya chama kama ilivoyoelezwa na msemaji wa chama ndugu Hamfrey polepole,hivi kwa mfano hapo mbeleni tena kama miezi kadhaa akaomba kujiunga tena na chama hicho hicho kama mwanachama mpya aombe kuwa kajirekebisha ,hivi sheria/ kanuni ya chama inasemaje ,je?atakubaliwa kwa masharti au huwa inakuwaje ufafanuzi tafadhali.
 
Upo sahihi na mtaji wa chama cha siasa ni watu
Mbona mashinji katoka Chadema kahamia CCM kwahiyo huo nao tuite mtego ? Na wengine wengi mpaka vyeo mmewapa kwenye siasa kawaida sana hiyo. Kama akitaka kuhamia upinzani wala sioni tatizo wamkubalie tuu.

In God we Trust
 
Ni mchezo kama game zingine tu na huu wa safari ni rahis kabisa.
 
Walichokifanya Ni divide and rule,Membe katimuliwa,Kinana karipio na Makamba kusamehewa.
Ili hata Kama walikuwa na mipango yao ivurugike.

Hapo itakuwa ngumu kuungana tena japo binafsi Makamba nilikuwa najua aweza kuomba msamaha.

Wanaamini Membe hatakuwa na nguvu tena hata wakimuondoa,ila wamepata hofu kubwa juu ya makatibu wasitaafu
 
Bahati mbaya sana CCM ya Magufuli hakuna mtu mwenye umaarufu; wote wanategema umaarufu wa Chama. Anayeondoka ataondoka yeye na familia yake na pengine hata familia yake wanaweza wamkatalie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…