CCM yamfukuza uanachama Bernard Membe, Kinana apewa karipio kali huku Makamba akitoka salama

CCM yamfukuza uanachama Bernard Membe, Kinana apewa karipio kali huku Makamba akitoka salama

Wameshaanza michezo yao usishangae membe akahamia chama pinzani Act wazalendo au Chadema..... Yakaja kutokea kama yake ya lowasa ccm inambinu kali sana inapofikia kipindi cha uchaguzi mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
June 8, 2015
Lindi, Tanzania

Membe : Ikulu Hainunuliki
Mwezi Juni mwaka 2015 cherekochero na Kusini 'kuchele' Katika viwanja vya CCM mjini Lindi kusini mwa Tanzania, waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Ndg. Bernard Membe akitangaza nia ya kugombea Urais kwa tiketi ya CCM mbele ya mamia ya wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara waliofika kumsikiliza. Agenda yake akifanikiwa kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Afya, viwanda vinavyotegemea mazao ya kilimo na nishati ya gesi kwa watanzania wote


Source: MCL Digital
 
Kaandika hivi kupitia twitter:

Watanzania wenzangu nimepata habari ya kufukuzwa kwangu kutoka kwenye Chama changu cha CCM. Simu zinamiminika hadi nashindwa kuzijibu. Tulieni! Nitapata muda wa kuongea na wote muda si mrefu!
Aongee tu nasi, tushachoka kumsubiri.
 
Hadi sasa haijaeleweka bayana mgombea urais wa Chadema mwezi October atakuwa nani japo Tundu Lissu na Nyalandu wamekuwa wakitajwatajwa na wanachama wachache wa kusini mwa Dodoma.

Awali ilisemekana kuwa Chadema watamuunga mkoni Maalim Seif kama atagambea urais wa Tanzania na Mbowe atakuwa mgombea mwenza lakini baada ya uchaguzi mkuu wa Chadema mambo yalibadilika.

Je Chadema itasimamisha mgombea mhamiaji?

Niishie hapo

Maendeleio hayana vyama!
 
Back
Top Bottom