CCM yamfukuza uanachama Bernard Membe, Kinana apewa karipio kali huku Makamba akitoka salama

CCM yamfukuza uanachama Bernard Membe, Kinana apewa karipio kali huku Makamba akitoka salama

Halafu utasikia makada wanasema CHADEMA/ ACT hakuna Demokrasia, Leo hii Membe mnamfukuza uanachama huku hamuwaambii wanachama wenu makosa ya Membe A-Z zaidi ya kusema general eti kukosa maadili.

CCM waambieni wanachama wenu makosa ya mbobezi Membe A-Z na sio kufanya mambo gizani.
 
Wangeanzisha kampuni sio vyama
Vipo vyama vinamilikiwa na watu Ila sio CCM
CCM Wamiliki wake wanabadilika kila wakati

Sent using Jamii Forums mobile app

Mmiliki wa CCM ni dola. Ndio maana unaona ikijisifia kutawala milele kwani wanajua dola itachezea uchaguzi. Namna pekee ya CCM kusambaratika ni kutokea machafuko ili tujipange upya.
 
Naonya CCM wasifanye Maamuzi ya Hasira na Kukomoa dhidi ya hawa Makada Waandamizi kwani wanaweza wakaja Kujuta kama si Kujutia hapo baadae. Nimeonya hivi hasa baada ya kupata za chini chini kuwa Maamuzi yatakayotolewa dhidi yao yatakuwa ni ya Kuwakomoa zaidi badala ya kuwa ya Kibusara kwa Afya na Ustawi wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM )
Umeandika kwa hisia ya mlango usio sahihi. CCM ingevurugika 2015 pale ilipoondokewa na viongozi wenye nguvu kIsiasa na chama kilikuwa taabani. Kwa sasa chama kina nguvu sana kisiasa.

Isitoshe mwanasiasa anapata nguvu ya kisiasa akiwa ndani na siyo nje ya CCM.
 
Ni kweli hana mvuto kwa wananchi ila nafikiri ametumia nafasi yake kama Waziri mambo ya nje kusabotage nchi yetu, kwa kifupi ni vurugu tu lkn hana uwezo wowote wa kushinda Uraisi TZ kwanza hata 1/3 ya kura alizopata Lowasa hawezi kufikisha.
Yeah kwahilo sawa,maana ana exposure kubwa nje ya Tz kuliko hata Rais......
 
Back
Top Bottom