mbenge
JF-Expert Member
- May 15, 2019
- 4,864
- 10,483
Chama kikongwe kama CCM kinapaswa kusimama ktk misingi yake ya awali, ile ambayo waasisi wake walienenda kupitia kwayo. CCM ambayo ilikuwa ni vikao vya chama vyenye vyenye maamuzi ya uhakika, na pia ni sehemu muhimu sana ktk kuambiana ukweli, kuonyana, kurekebishana na hata kuwekana sawa pale endapo kulionekana kuwa na dalili hasi za mgawanyiko miongoni mwa makada wenye nguvu kiasi cha kutishia kukigawa chama.
Sasa tunaiona siasa mpya ambayo inaendeshwa na hisia za Mwenyekiti Taifa. Endapo kada akakosa kibali mbele ya macho yake, pasipo kujali mchango wake ndani historia ya chama, atadukuliwa mazungumzo yake ya faragha, afuatiliwa kwa ukaribu nyendo na maongezi yake. Yote yatafanyika ili kuhalalisha kukosa kwake utiifu kwa chama.
Mh. Membe tambua ya kuwa wewe bado ni mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa sana nchi na pia mwenye kuiheshimika, na umeishi maisha ya kisiasa kwa muda mrefu. Sasa umeingia ktk ukurasa mpya wa maisha haya. Bado una uwezo, ama kufanya uamuzi wa kustaafu siasa za kiushindani ili kukwepa adha, maudhi na maisha mengine ya mahangaiko ambayo mahasimu wako ni lazima watakuwa wamejiandaa kukupitisha ktk tanuru la moto, ili kuzidi kukitia madoa ya fedheha mbele ya jamii.
La kama si hivyo, bado una uwezo wa kuendelea na mapambano ya kisiasa, ili kufungua ukurasa mpya wa siasa ndani ya nchi yetu, ndani ya CCM hata nje yake pia ktk vyama vya upinzani. Unao uwezo mkubwa wa kuwa kiunganishi cha wapenda mabadiliko ya kweli ktk siasa za nchi yetu. Unao uwezo wa kukabiliana na siasa chafu na michezo dhalimu na ya dhuluma ktk kupindisha maamuzi ya kweli ya umma kupitia upigaji wa kura ktk chaguzi mbalimbali zifanyikazo hapa nchini, kama huu tunaoutegemea mwaka huu wa 2020.
Jipe, muda wa kutosha na tena kwa kushauriana na watu makini, kabla ya kutoa msimamo wako mpya. Nakutakia kila la heri.
Naamini, watu wengi bado wapo nyuma yako, na pia wanakuunga mkono. Umevuliwa uanachama si kwa sababu ya kukosa utiifu kwa chama chako, ambacho umekitumikia kwa uaminifu, umakini na uweledi mkubwa, isipokuwa kwa vikao vya uamuzi kuweza kukidhi hisia za Mwenyekiti Taifa dhidi yako.
Sent using Jamii Forums mobile app