CCM yamfukuza uanachama Bernard Membe, Kinana apewa karipio kali huku Makamba akitoka salama

CCM yamfukuza uanachama Bernard Membe, Kinana apewa karipio kali huku Makamba akitoka salama

Msamaha wa Makamba ni kwa vile mwanae aliomba msamaha.. Inajulikana wazi msamaha ule ulichagizwa kwa sehemu kubwa na ushawishi wa baba

Karipio kali la Komredi Kinana nibkujihusisha na majungu na masimango lakini hajaonesha nia ya kutaka nafasi yoyote.. Vile vile karipio kali linaambatana na maneno MZEE KAA KIMYA TUNAKUFAHAMU

Kufukuzwa kwa Membe ni sababu ya kuonesha nia ya kugombea nafasi kubwa kwenye uchaguzi wa mwaka huu...

Kwa sasa vumbi halijatulia... Likishatulia kuna mengi yatokanayo yatajitokeza... Hulka ya binadamu wengi ni kukosa koromeo.. Kuna ambao wataropoka kama walivyokwisha anza tayari... Lakini pia mpaka kufikia hatua ya kumfukuza Membe walishapima nguvu yake na kuona ni mwepesi... Japo kuna kitu kingine kikubwa sana nyuma yake.... Kumfukuza MEMBE uanachama ni sawa na kumpika kofi la kelebu JK... Je ataweza kuvumilia haya maumivu?
Muda utasema!

Jr[emoji769]
 
Hivi ni kosa kuchukua fomu ya uraisi? Hicho chama chenu mnakiendeshaje? Mwambieni mwenyekiti asiogope upinzani ndani ya chama.yeye anadhani kila mtu anamkubali na ubabe wake?
Membe alikosea sana.
 
Demokrasia ni kitu gani??? Unajua maana ya demokrasia au maana ya kuminyaa demokrasia?? There is no absolute democracy anywhere in this world...
Ikija survey mpya, IQ ya watanzania itakuwa ya chini kabisa duniani. Tuna kila sababu ya kuwa hivi tulivyo hata Mungu atuongeze rasilimali mara bilioni moja ni kazi bure tu.

Afadhali awaongezee hata samaki baharini ambao hata wakishindwa kuzitumia ni haki yao.
 
Pale CCM sasa hivi wote mikia iko matakoni Mwenyekiti kishaamua.
 
Hivi ni kosa kuchukua fomu ya uraisi? Hicho chama chenu mnakiendeshaje? Mwambieni mwenyekiti asiogope upinzani ndani ya chama.yeye anadhani kila mtu anamkubali na ubabe wake?
Membe aliongoza kikundi kupinga wale waliokuwa wakitaka kushindana na kikwete, ila yeye anafanya kile ambaho alikuwa akikipinga hapo awali. kwanini abadilike haraka namna hiyo?? Anapenda madaraka. Ila Jamaa hana mvuto wa kisiasa kabisa.
 
TUWE TUNAAMBIWA UKWELI, AKINA NAPE WALIENDA KUMWOMBA RADHI MZEE JIWE. HIVYO TUAMBIWE JE, HAWA WATU WANAKIKOSEA CHAMA AU WANAMKOSEA JIWE? KAMA WANAKIKOSEA CHAMA INAKUWAJE WAKAMWOMBE RADHI MTU MMOJA NDANI YA CHAMA?

MIMI NAFIKIRI TUAMBIWE TU UKWELI KWAMBA HAWA NDUGU ZETU AKINA MEMBE WAMEHITILAFIANA NA JIWE. MSITUINGIZE SISI WANACHAMA WOTE WA CHAMA CHETU BALI NONGWA NI JIWE!!!
 
umeandika vzr the first points, ila umekuja kuharibu kuwa kinana ana nguvu huku nje, u cnt be serious, au ulimanisha Membe? na hata huyo Membe nguvu kwishine, make huko Mtwara wote wameamua kuunga juhudi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mwenye kumbukumbu ajuze kuhusu wanachama wengine waliowahi kufukuzwa uanachama wa CCM
 
Kwa maneno yake Zitto waliopo katika kikao hiki wote walikuwa "Kanya Boya". Walikuwa wasinziaji tu maamuzi ni ya mtu mmoja😀😀.

Na anataka tumuamini maamuzi yatolewayo na vyama vya siasa Tanzania hata huko ACT, juu ya nani awe mwanachama au awe kiongozi, huwa si ya kuzingatia vikao bali maamuzi ya mtu mmoja kiongozi wa juu wa chama.

CCM inawashauri wazuri sana, kumzuia Magufuli asiseme neno baada ya kukashifiwa bali aziachie Machinery za chama zifanye kazi yake.
 
Wewe unaijua Demokrasia?!

Mkuu TFF imeamua nini kwa Morrison wa Yanga kudandiadandia mpira bila sababu ya msingi, naona juzi alianza tena kubinua binua inyaa yake kama vile anataka kudandia mpira au naye ni Democrasia yake inamruhusu?
 
Hii ni wazi kabisa Magufuli aliona Membe ndio mpizani mkubwa kwake, ilikua inatafutwa sababu tu.
Mtukufu Rais akae akijua ana miaka mitano mingine na yeye yatakuja kumkuta tu.
Hivi akitoka bila kumuweka kibaraka wake ataishi wapi maskini maana hata pa kuficha ule mkichwa wake hajapaandaa kabisa
 
Kuonesha nia ya kugombea uongozi ndio kuvuruga chama? Mwalimu Nyerere alikuwa muumini wa demokrasia na haki ya kila mwanachama kuwania uongozi.leo CCM imeshikwa na intarahamwe poleni sana
Hii ndio CCM aliyoiacha Baba wa Taifa Mwalimu J.K Nyerere. Chama hiki ni lazima kiheshimike, asitokee mtu mmoja mpuuzi anayejaribu kuvuruga Chama. Pongezi kwa Kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi kwa maamuzi hayo.
 
Back
Top Bottom