CCM yamfukuza uanachama Bernard Membe, Kinana apewa karipio kali huku Makamba akitoka salama

CCM yamfukuza uanachama Bernard Membe, Kinana apewa karipio kali huku Makamba akitoka salama

Sema magufuli Kwanza wewe ndio ccm ifuate.
CCM chama imara sana aisee. Hakiyumbishwi na mtu hata mmoja, CCM kwanza, vingine ndio vitafuata, ukitaka kuiyumbisha CCM utapotea katika siasa za Tanzania.
 
Yudatade Edesi Shayo,
Lengo ni ACT Wazalendo Arawa!... Wembe ule ule uliowanyoa CHADEMA ndio huo huo unatayarishwa kupunguza nywele ndefu za chama cha Ayatollah, CHADEMA kazi yake imeishakamilika.
 
Lowasa na Sumaye wametosha kutupatia aibu kubwa
Naona Mkuu awamu hii tumeamua tufungue mioyo ili tuseme yaliyo ndani ya mioyo yetu.

Ni ukweli usiopingika, Lowassa alikuja kumaliza nguvu ya upinzani, na mimi ninaona kabisa ulikuwa ni mpango wa CCM.

Leo hii pia wamemtoa Membe, nadhani shida yao ni jamaa kwenda ACT ili ACT kiwe chama rasmi cha Upinzani.

Mbowe asipoamka hiki chama tunakizika, karata ya mbowe ilikuwa ni ya hovyo 2015.

Nakumbuka kuna wadau tulichangia ktk uzi flani kuwa hatufurahishwi na CDM kumpokea Lowassa maana ni kubomoa msingi wetu.

Leo hii wote twajionea, japo tuliitwa mamluki, tukafananishwa na Dr Slaa.

CDM isipokuwa makini mwaka huu ktk uchaguzi itaanguka kwa kishindo kizito kuliko hata 2015.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona mashinji katoka Chadema kahamia CCM kwahiyo huo nao tuite mtego ? Na wengine wengi mpaka vyeo mmewapa kwenye siasa kawaida sana hiyo. Kama akitaka kuhamia upinzani wala sioni tatizo wamkubalie tuu.
Tena agombee urais ili amtoe Jiwe maana huyu kachero mzoefu hagusiki kabisa.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
....two options.
1.wanazuiwa kufanya siasa for sometime -mpaka uchaguzi upite
2.watasema tumewasamehe lakn mmeonywa

.....hawana uwezo wa kuwafanya nje ya hayo mawili coz wanajua nguvu ya Kinana si ya kitoto

Sent using Jamii Forums mobile app
MAAMUZI YA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM, hayakulenga uwanachama wa mtu bali yalilenga mwenendo na tabia ya mwanachama. Yalilenga mapungu ya mwnachama. Chama kina kanuni katika misingi yake na mwanachama hatakiwi kuzivuja. Ukivunja tu, unasukumwa nje bila kujali hata kama ulishiriki kutunga hizo kanuni.

Ndani ya chama hakuna mwenye chama bali yupo mwanachama. Hao uliowataja, sio wenye chama, ila ni wanachama. Wanachama ni wengi, na hakuna wenye chama. Kama kungekuwa na mwenye chama, basi kingekuwa cha Mwl. J.K Nyerere na baada ya kifo chake, basi chama kingelisambarika.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani si nilisikia sheria mpya ya vyama vya siasa ni kuwa kama haujafikisha mwaka mmoja kwenye chama cha siasa hauna nguvu ya kugombea au ilikuwa sio ivyo tena

Sent using komputa mpakato

Vyama vya upinzani ni muhimu kutambua kuwa kinachohitajika sasa kuliko wakati wowote ni namba, namba ya wanachama na hivyo namba ya wapiga kura.

Ni muhimu sasa, wale jamaa zetu wa TSIS ambao wameyatelekeza maslahi ya nchi na kujiuliza kwenye maslahi ya watawala watambue kuwa hatudanganyiki.

Be it - Membe, Mashinji, Sumaye, Lowassa, wale wanaotoka kuondoka au wanaotaka kurudi upinzani nk nk - enyi TSIS mjue wanakaribishwa na wala hatuna pressure nao.

Waambieni wanaowatuma wazi wazi kuwa wale jamaa hawadanganyiki tena kwani 'watanzania wa leo siyo wale wa jana'.

2020 twende na membe itakuwa tamu kuliko maelezo.
 
Eti mhaya fake bashiru anamfukuza membe uanachama ccm. Tamaa mbaya, ccm ni chama ya mtu mmoja. Maamuzi anatoa yeye kisha wanafunikafunika eti kuoji ili ionekane kama vile haki inatendeka. Jamaa anaogopa ushindani balaa.

Kaanza na wapinzani kawazima na kuwatisha sasa ameamia ndani familia yake ya ccm. Kwa siasa za ccm zilivyo uenda hata hao akina makamba na kinana walitumwa kumtega membe ili afukuzwe, na yote yaliyokuwa yanaendelea ni mission waliokuwa wanaijua.
 
Mbona mashinji katoka Chadema kahamia CCM kwahiyo huo nao tuite mtego ? Na wengine wengi mpaka vyeo mmewapa kwenye siasa kawaida sana hiyo. Kama akitaka kuhamia upinzani wala sioni tatizo wamkubalie tuu.
Sio Mashinji pekee, bali pia aliyekuwa mgombea urais wao na kupata asilimia nyingi kahamia CCM
 
Back
Top Bottom