CCM yaridhia Katiba Mpya, kwamba ni takwa la Wananchi, je itaafikiwa na Wananchi?

CCM yaridhia Katiba Mpya, kwamba ni takwa la Wananchi, je itaafikiwa na Wananchi?

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,132
Reaction score
64,416
Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimekubaliana na umuhimu wa kupatikana katiba mpya kwa kuzingatia mazingira ya sasa hivyo kimeishauri Serikali kuona namna bora ya kufufua, kukwamua na kukamilisha mchakato wake kwa maslahi mapana ya Taifa na Watanzania wote.

====

1. Maridhiano ya kifaifa.
2. Kufufuliwa kwa mchakato wa Katiba kwa kuzingatia mazingira ya bora ya sasa.
"Chama cha Mapinduzi tunasisitiza umuhimu wa uwepo wa Katiba mpya kwa kuzingatia mazingira ya sasa na kuona namna bora ya kufufua, kukwamua na kukamilisha mchakato wa katiba mpya kwa masilahi mapana ya taifa na maendeleo kwa ujumla." ameeleza Ndg. Shaka Hamdu Shaka, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi ya Taifa - Itikadi na Uenezi wakati akizungumza na wanahabari.
 
IKikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimekubaliana na umuhimu wa kupatikana katiba mpya kwa kuzingatia mazingira ya sasa hivyo kimeishauri Serikali kuona namna bora ya kufufua, kukwamua na kukamilisha mchakato wake kwa maslahi mapana ya Taifa na Watanzania wote.

====

1. Maridhiano ya kifaifa.
2. Kufufuliwa kwa mchakato wa Katiba kwa kuzingatia mazingira ya bora ya sasa.
"Chama cha Mapinduzi tunasisitiza umuhimu wa uwepo wa Katiba mpya kwa kuzingatia mazingira ya sasa na kuona namna bora ya kufufua, kukwamua na kukamilisha mchakato wa katiba mpya kwa masilahi mapana ya taifa na maendeleo kwa ujumla." ameeleza Ndg. Shaka Hamdu Shaka, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi ya Taifa - Itikadi na Uenezi wakati akizungumza na wanahabari.
Kama kweli vizuri sana,kama janja janja ilmuradi muda upite tutajua mapema Tena Muda muafaka
 
Halmashauri Kuu ya CCM iliyoketi Dodoma chini ya Mwenyekiti wake Mh Samia Suluhu Hassan , imekubaliana na kuona Umuhimu wa kuendelea tena na Mchakato wa kupatikana kwa Katiba Mpya , kwa kuzingatia Mahitaji ya sasa KWA MASLAHI MAPANA YA TAIFA .

Chanzo : MwanaHalisi Digital
 
Nchi ni ya Watanzania wote, Hakuna haja ya watu kujimilikisha Kipande. Nawaona waliokuwa wanaizodoa CHADEMA wakipiga U-turn Kali.
Kwani Kikwete si aliipeleka katiba mpya mpaka pale alipojikuta wale waliokuwa wakimpresha kumbe lao halikuwa maudhui ya katiba? Kwao lilikuwa kujiondolea vile walivyoona kama vikwazo kushinda uchaguzi na kuingia Ikulu.

Haya bana ngoja tuone huyu nahodha chombo atakifikisha wapi. Sisi yetu macho.
 
Acheni kupotosha kinachowapeleka ikulu ni time huru kama ingekua hiko ni kigezo si wangeendelea kubaki.

Changamoto mchakato ulikwamishwa na CCM walipokuja na Draft Yao na kutaka wa overwrite maoni ya warioba kitu ambacho kiliharibu neutrality na independence ya wajumbe hasa wa CCM.

Tyranny of numbers kiliua mchakato ule hakukuwa na concession Wala compromise ilikua ni ubabe kisa wengi ni CCM!!

Lakini kudai eti walitoka kisa waliwaza uchaguzi ni uongo, sasa muundo wa muungano ungewasaidia vipi CHADEMA kushinda Urais??
 
Mtihani wa kwanza utaanzia pale namna ya kuwapata wajumbe watakaoingia kwenye hilo bunge la Katiba, CCM kwa umiliki wake wa taasisi karibia zote nchi hii wanatakiwa waondoe ubinafsi, waweke maslahi ya taifa mbele kama kweli wana dhamira ya dhati.
 
Back
Top Bottom