CCM yaridhia Katiba Mpya, kwamba ni takwa la Wananchi, je itaafikiwa na Wananchi?

CCM yaridhia Katiba Mpya, kwamba ni takwa la Wananchi, je itaafikiwa na Wananchi?

Mama naona ana nia ya dhati, kama kina Mbowe nao watakubali kukosa mambo kadhaa Ili wapate mengine basi mchakato utafanikiwa. Ila Kila mtu akiingia kwa majadiliano wakiwa na hardliners basi utafia njiani na hautofufuliwa kamwe.
Kuna mambo ya msingi ambayo ni "irridusable".
Sitegemei pawepo na 'compromize' kwenye maswala kama hayo.

Kwa hiyo tusianze kuwalainisha mapema hivi waondokane na u'harliner' kwa jina la 'compromize' kungali mapema hivi.
 
Power is nothing without control, hayo yoote uliyosema maji madaktari etc , kama hakuna control ya uhakika hayatimii , tumeimba hayo toka tulipopata uhuru hatukufanikiwa kwa sababu ,katiba yetu inawafanya viongozi kuwa miungu watu .
Tunahitaji pa kuanzia na katiba ndo square one.

hiyo katiba mpya yenyewe inadeal na viongozi tu, raia wavivu, wezi, wazembe, fikra duni haina meno kwao?...
 
m

mimi sio CCM wala CDM naishi na misimamo yangu, atakayeangukia kwenye misimamo yangu kulingana na fikra zangu wakati huo utaniona niko naye...

Katiba ya zamani imezuia nini Watanzania wasipate umeme wa uhakika na maji safi na salama na Katiba mpya itakuja na uchawi gani watanzania wakavipata hivi kwa haraka?
Kaka
Katiba ya zamani ,ndio imefanya chato pajengwe international airport wakati hakukuwa na ulazima huo, ndo inafanya viongozi watembelee v8 za 400 mil plus ilhali hospitali hazina madawa ,
 
hiyo katiba mpya yenyewe inadeal na viongozi tu, raia wavivu, wezi, wazembe, fikra duni haina meno kwao?...
Tuna mengi ya kujifunza kutoka kwa jirani zetu wa kenya na katiba yao mpya ,
Jaji maraga alivunja matokeo na kuamuru uchaguzi urudiwe
Uhuru leo hii anamkana waziwazi deputy president Ruto , na bafala yake ana mu endorse Raila , kwa mara ya kwanza mkikuyu na mjaluo wanakaa kwenye common ground kwa maslahi ya taifa lao
Angalia bunge la kenya , utaona tofauti kubwa sana na bunge letu
 
Tuna mengi ya kujifunza kutoka kwa jirani zetu wa kenya na katiba yao mpya ,
Jaji maraga alivunja matokeo na kuamuru uchaguzi urudiwe
Uhuru leo hii anamkana waziwazi deputy president Ruto , na bafala yake ana mu endorse Raila mjaluo na mkikuyu hawajawahi kukaa pamoja
Angalia bunge la kenya , utaona tofauti kubwa sana na bunge letu

Hayo yoote yamesababishwa na katiba mpya huko Kenya? kachimbue vizuri siasa za Kenya....

utofauti wa Kenya na Tanzania kwenye siasa uko hapa, Siasa Kenya inafanywa na matajiri, Siasa Tanzania inafanywa na marofa na mambumbu.... Population kubwa Kenya ni smart kichwani, popilation kubwa Tanzania ni mbumbumbu hivyo hivyo kwenye siasa.
 
Kaka
Katiba ya zamani ,ndio imefanya chato pajengwe international airport wakati hakukuwa na ulazima huo, ndo inafanya viongozi watembelee v8 za 400 mil plus ilhali hospitali hazina madawa ,

kwahiyo ikija katiba mpya hayo hayatatokea?.... kwani Katiba ya Zamani inaruhusu hayo?
 
Nchi hii mpaka chama tawala kitake katiba mpya ndio itapatikana?!!!
Kwa mfumo wa katiba yetu hayo usemayo inaweza kuwa sahihi
Mwalimu nyerer aliwahi kusema upinzani utatokea ccm na hali halisi inaonekana
Them sukuma gang walishaonja sukari na wanampinga mama hadharani kweupe, mama naye ana team yake ambayo naamini watakopoona kushindwa kupambana wataangukia kwenye katiba mpya ili.kila mtu akose
Na ndio kinachotokea sasa
 
kwahiyo ikija katiba mpya hayo hayatatokea?.... kwani Katiba ya Zamani inaruhusu hayo?
Katiba ya zamani inampa mamlaka makubwa sana rais , hawa covid 19 uwepo wao umesababishwa na katiba mbovu.
Ukisikia mamlaka ya rais yamepunguzwa ni kama kule kenya ambapo jaji mkuu aliamuru uchaguzi urudiwe , na uhuru hakuwa na namna zaidi ya kufata matakwa ya muhimili huo.
Huku cag aliposema tu kuna matumizi mabaya ya pesa , akapoteza na kazi.
 
Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimekubaliana na umuhimu wa kupatikana katiba mpya kwa kuzingatia mazingira ya sasa hivyo kimeishauri Serikali kuona namna bora ya kufufua, kukwamua na kukamilisha mchakato wake kwa maslahi mapana ya Taifa na Watanzania wote
Kwa msoto ule walioupata kutoka kwa Mwensazake ningeshangaa kama wangeshupaza shingo.

Kwa mazingira ya sasa na maslahi mapana ukiacha wale akina( self feeders) ni hekima na busara kuwa na Katiba ambayo ni jibu kwa maswala mengi.

Pongezi nyingi kwa chama cha mapinduzi lakini pia kwa Mh Rais Samia Suluhu Hassan
 
Kifaifa = Kitaifa.

Katiba hata ibadilishwe kila mwaka haitasaidia kama uelewa wa watu utabakia kuwa huu huu.

Endeleeni kupinga hata hii, huko handeni mnakopelekwa ukija uongozi mwingine ukija mtapelekwa somalia,

Katiba mpya ni muhimu sana kwa nchi yetu kwa hapa tulipo fikia sasa hiv
 
Katiba ya zamani inampa mamlaka makubwa sana rais , hawa covid 19 uwepo wao umesababishwa na katiba mbovu.
Ukisikia mamlaka ya rais yamepunguzwa ni kama kule kenya ambapi jaji mkuu aliamuru uchaguzi urudiwe , na uhuru hakuww na namna zaidi ya kufata matakwa ya muhimili huo.
Huku cag aliposema tu kuna matumizi mabata ya pesa , akapoteza na kazi.

uchaguzi uliporudiwa nini kilitokea?
Umesahau Raila alijiapisha....

unayajua maoni ya Wakenya kwasasa kuhusiana na hiyo katiba mpya unayowsifia nayo?

Hivi unajua hiyo katiba mpya wakenya wa kawaida wameshaanza kuiona kero..
Hivi unajua Kenya pamoja na kuwa na katiba mpya bado mpaka leo wana migogoro ya kisiasa kila leo?.....
 
Endeleeni kupinga hata hii, huko handeni mnakopelekwa ukija uongozi mwingine ukija mtapelekwa somalia,

Katiba mpya ni muhimu sana kwa nchi yetu kwa hapa tulipo fikia sasa hiv

kwahiyo katiba mpya itazuia watu wasihamishwe, katiba ya zamani inaruhusu watu kuhamishwa....?
 
Hayo yoote yamesababishwa na katiba mpya huko Kenya? kachimbue vizuri siasa za Kenya....

utofauti wa Kenya na Tanzania kwenye siasa uko hapa, Siasa Kenya inafanywa na matajiri, Siasa Tanzania inafanywa na marofa na mambumbu.... Population kubwa Kenya ni smart kichwani, popilation kubwa Tanzania ni mbumbumbu hivyo hivyo kwenye siasa.
Population kubwa ya kenya ni smart kweli wala sio utani, wanna know why?
Wenzetu walikuwa mabepari toka zamani , ilhali sisi tuliongozwa kwa miaka 20 plus na mtu aliyeamini ujamaa,
To the best of my understanding hakuna system inayotengeneza wavivu na watu mbumbumbu kama system ya ujamaa.
 
uchaguzi uliporudiwa nini kilitokea?
Umesahau Raila alijiapisha....

unayajua maoni ya Wakenya kwasasa kuhusiana na hiyo katiba mpya unayowsifia nayo?

Hivi unajua hiyo katiba mpya wakenya wa kawaida wameshaanza kuiona kero..
Hivi unajua Kenya pamoja na kuwa na katiba mpya bado mpaka leo wana migogoro ya kisiasa kila leo?.....
Leo mtachanganyikiwa.

Harakati za Mbowe zimezaa matunda. Na Bado Rais Samia amedhamilia kuikomboa Tanzani nyie sukuma gang hamna chenu.
 
sisi tunaotaka katiba mpya kama raia tunatimiza wajibu wetu? kufanya kazi kwa bidii kujenga Taifa letu, kulipa kodi ipasavyo, kutoomba wala kupokea rushwa, kutii sheria za barabarani nk...
 
Back
Top Bottom