CCM yaridhia Katiba Mpya, kwamba ni takwa la Wananchi, je itaafikiwa na Wananchi?

CCM yaridhia Katiba Mpya, kwamba ni takwa la Wananchi, je itaafikiwa na Wananchi?

Halafu bado kuna wapuuzi wanadai kuwa Mbowe ameacha kudai katiba mpya kwa sababu amepewa pesa na Serikali.

Mbowe, na CHADEMA kwa ujumla, waliacha kuendeleza harakati za kudai katiba mpya kwa mikiki baada ya Rais kuridhia na kuahidi kushirikisha wadau wengine.

Mafanikio ya Mbowe na CHADEMA:

1) Serikali imekubali kuanza mchakato wa katiba mpya, CCM nayo imekubali

2) Serikali imekubali uwepo wa tume huru ya uchaguzi

3) Serikali imekubali kuwaachia huru wanachama wote wa CHADEMA waliowekwa mahabusu na magerezani na dikteta Magufuli, kwa kuonewa

4) Serikali imekubali kuwalipa stahili na fidia wanachama na viongozi wa CHADEMA ambao dikteta Magufuli aliwapora

5) Serikali imekubali kufanya maridhiano ili kuliponya Taifa, ombi ambalo dikteta Magufuli alilikataa, pale alipoombwa na Mbowe

CHADEMA, nimeamini ni makini sana, wenye akili tu ndio watalijua hilo.
 
CCM imekubali katiba mpya, more like CCM imeamua kuchezea hela za walipa kodi tena.

Kama issue ni muungano, Zanzibar wapewe kura ya maoni wasipoutaka uvunjwe huu ndio muda wa kuutazama muungano.

Katiba aina shida inahitaji amendments tu za kupunguza madaraka ya raisi.

Mtu analalamika CAG awezi enforce watu ku implement mapendekezo yake ya audit kumpa nguvu apewe mamlaka ya kikatiba kufanya ivyo; ndio moja ya argument yake ya kudai.

Kazi ya auditor ni ku reinforce mapendekezo kweli, ndio aina ya watu wanaoropoka kudai katiba ata issue za management zinatatuliwa vipi hawajui.

Wanaodai katiba mpya for the most ni waropokaji tu ata ukiwaambia wakutajie aspects za katiba awawezi.

Waste of taxpayers money.
 
Hiyo ni hatumia moja kati ya mia zinazifufuata, ila kwakuwa wameana hatua ya kwanza basi kwa njia yoyite tutawasukuma kukamilisha hatua zingine, najua haitakuwa rahisi
 
CCM imekubali katiba mpya, more like CCM imeamua kuchezea hela za walipa kodi tena.

Kama issue ni muungano, Zanzibar wapewe kura ya maoni wasipoutaka uvunjwe huu ndio muda wa kuutazama muungano.

Katiba aina shida inahitaji amendments tu za kupunguza madaraka ya raisi.

Mtu analalamika CAG awezi enforce watu ku implement mapendekezo yake ya audit kumpa nguvu apewe mamlaka ya kikatiba kufanya ivyo; ndio moja ya argument yake ya kudai.

Kazi ya auditor ni ku reinforce mapendekezo kweli, ndio aina ya watu wanaoropoka kudai katiba ata issue za management zinatatuliwa vipi hawajui.

Wanaodai katiba mpya for the most ni waropokaji tu ata ukiwaambia wakutajie aspects za katiba awawezi.

Waste of taxpayers money.
Hapana. Katiba Mpya ni takwa la wananchi na wananchi ndio walipa kodi, hivyo kuwapa wananchi kile watakacho haiwezi kuwa kuchezea pesa zao.

Amendments/viraka vilivyopo kwenye katiba ya sasa vinatosha, na huwezi kuweka kiraka juu ya kiraka, hiyo nguo haitashoneka.
 
Mungu ibariki Tanzania, naiona kesho yenye matumaini na faraja kwa watanzania. Naiona kesho yenye empathy kwa wenye majonzi na huzuni. Naiona kesho yenye kurudisha tumaini kwa waliokata tamaa. Upatikanaji wa katiba mpya ni ushindi kwa taifa letu.
 
Hawezi kukujibu
Ndio aina ya watu wanaodai katiba mpya.

Yaani ukisikiliza hoja zao unawaachia wenyewe.

Mwingine Zitto audit advise na reinforcement ya kikatiba wapi na wapi.

Au utasikia sijui itenge fungu la kununua mazao ya wakulima kwenye katiba.

For the most part akili zao zinawatosha wenyewe wakiwa huko Maria Space.
 
Halmashauri Kuu ya CCM iliyoketi Dodoma chini ya Mwenyekiti wake Mh Samia Suluhu Hassan , imekubaliana na kuona Umuhimu wa kuendelea tena na Mchakato wa kupatikana kwa Katiba Mpya , kwa kuzingatia Mahitaji ya sasa KWA MASLAHI MAPANA YA TAIFA .

Chanzo : MwanaHalisi Digital
Baada ya uchaguzi
 
Kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimekubaliana na umuhimu wa kupatikana katiba mpya kwa kuzingatia mazingira ya sasa hivyo kimeishauri Serikali kuona namna bora ya kufufua, kukwamua na kukamilisha mchakato wake kwa maslahi mapana ya Taifa na Watanzania wote.

====

1. Maridhiano ya kifaifa.
2. Kufufuliwa kwa mchakato wa Katiba kwa kuzingatia mazingira ya bora ya sasa.
"Chama cha Mapinduzi tunasisitiza umuhimu wa uwepo wa Katiba mpya kwa kuzingatia mazingira ya sasa na kuona namna bora ya kufufua, kukwamua na kukamilisha mchakato wa katiba mpya kwa masilahi mapana ya taifa na maendeleo kwa ujumla." ameeleza Ndg. Shaka Hamdu Shaka, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi ya Taifa - Itikadi na Uenezi wakati akizungumza na wanahabari.
View attachment 2269081
Ila CCM ni Wanafiq Jaman, khaaaa
 
m

mimi sio CCM wala CDM naishi na misimamo yangu, atakayeangukia kwenye misimamo yangu kulingana na fikra zangu wakati huo utaniona niko naye...

Katiba ya zamani imezuia nini Watanzania wasipate umeme wa uhakika na maji safi na salama na Katiba mpya itakuja na uchawi gani watanzania wakavipata hivi kwa haraka?
Utakaposhuhudia mradi wa JNHPP ukisuasua - kwa makusudi, vituo vya afya vikikosa watumishi, vitendea kazi na madawa - kwa makusudi ndipo utaelewa katiba bora ina kazi gani.

Unafikiri maelfu ya wananchi waliotoa maoni na mapendekezo ya kikatiba kwa Tume ya Warioba walikuwa wajinga?
 
Katiba ya 1977 imevest nguvu kubwa mno kwa mtu ambaye anakua Rais.

Akitokea tuu mtu mnafiki kama bwana yule ambaye wakati anaomba alikua pamoja na wenzie halafu akiipata nafasi hiyo anawageuka na kujiita jiwe mara sijui chuma huku akidai kushauriwa ni “ kuendeshwa” na mambo mengine mengi kama “ Mimi ndo Rais “ ni hatari sana na rahisi sana kuweza kuwa Dictator.

Inahitajika katiba ambayo italeta balance of powers kwenye mihimili yote mitatu kama Master mason, Senior warden na junior warden kwenye freemasonry.

Watu wenye akili hawawezi kuendelea na katiba ambayo inadai taifa hili ni la kijamaa ilihali watu wanaishi kibepari!!

State it clearly who are you?!
 
muda huo na gharama zake tungeutumia kuhakikisha kila kaya inakuwa na maji safi na salama.

Muda huo na gharama zake tungeutumia kuhakikisha kila kaya inapata umeme wa uhakika.

Muda huo na gharama zake tungehakikisha kila wilaya inakuwa na hospitali ya kubwa ya rufaa na vitanda cha kutosha..

Muda huo na gharama zake tungehakikisha pale muhimbiri tunatahini madaktari wa kutosha, mafamasia na manesi wa kutosha kuhakikisha tunapunguza gap la mgonjwa na daktari..

Hivyo navyo bila shaka vinahitaki katiba mpya, Katiba kwa sasa sio tatizo la msingi halipaswa kuwa kipaumbele cha Taifa, nikupoteza muda na rasilimali...
Hivi wewe hujui kuwa hivyo vyote ulivyovitaja, vinapatikana baada ya kupata Katiba mpya?

Unajua kuwa bila kuwa na Katiba mpya, huwezi kuwa na utawala bora, kwa hivyo vyote ulivyovitaja, kuvipata kwake ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu?
 
muda huo na gharama zake tungeutumia kuhakikisha kila kaya inakuwa na maji safi na salama.

Muda huo na gharama zake tungeutumia kuhakikisha kila kaya inapata umeme wa uhakika.

Muda huo na gharama zake tungehakikisha kila wilaya inakuwa na hospitali ya kubwa ya rufaa na vitanda cha kutosha..

Muda huo na gharama zake tungehakikisha pale muhimbiri tunatahini madaktari wa kutosha, mafamasia na manesi wa kutosha kuhakikisha tunapunguza gap la mgonjwa na daktari..

Hivyo navyo bila shaka vinahitaki katiba mpya, Katiba kwa sasa sio tatizo la msingi halipaswa kuwa kipaumbele cha Taifa, nikupoteza muda na rasilimali...
Vyote yawezekana vikafanyika kwa pamoja
 
Back
Top Bottom