LGE2024 CCM yashinda 98.83% Wenyeviti Serikali za Mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa amesema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepata ushindi wa viti 1,222 sawa na asilimia 0.53 katika nafasi ya wajumbe wa halmashauri za vijiji mbalimbali nchini huku Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikiibuka na ushindi wa viti 229,075 sawa na asilimia 99.

Mchengerwa amesema hayo leo Novemba 28, 2024 wakati akitoa matokeo ya jumla ya uchaguzi huo huku akitaja vyama vingine kama ifuatavyo;

Chama cha ACT Wazalendo kimepata viti 232 sawa na asilimia 0.1 Chama cha Wananchi CUF kimepata viti 105, sawa na asilimia 0.05 na chama cha NCCR Mageuzi viti 16 sawa na asilimia 0.01.
 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa amesema Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kimepata kiti kimoja katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa upande wa wenyeviti wa mitaa katika uchaguzi uliofanyika jana Novemba 27, 2024.

Mchengerwa amesema hayo leo Novemba 28, 2024 wakati akitoa matokeo ya jumla ya uchaguzi huo akikitaja Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuongoza kwa kupata jumla ya viti 4,213 sawa na asilimia 98.83 huku Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikishika nafasi ya pili kwa kupata viti 36 sawa na asilimia 0.84.

Mapema akizungumzia kwa upande wa wenyeviti wa vijiji, Mchengerwa amesema huko pia CCM imeongoza asilimia 99.01 ( viti 12,150) huku Chadema ikipata asilimia 0.79 (viti 97).
 
Kituoa wapiga kura hawajazidi 40 kwenye matokeo wanaonekana watu 340, very stupid
Dogo langu linaniambia kuwa kule aliko MBINGA DC hapakuwepo wagombea kutoka vyama vingine bali CCM tu lkn bado kura fake zilipelekwa vituoni ili kuepuka kura za HAPANA na kukosesha ushindi ambao ulikuwa fixed 98%.

Yaani dogo anasema mpaka Walimu wenzake waliopendekezwa kusimamia huo uchaguzi licha ya kuwa wengi wao wana kadi za CCM ila wizi huo umewastaajabisha mno.
Wanajuta kutendeshwa wizi huo.
 
Mwenyekiti mwenyewe ni yule anaeona watanzania tuna njaa ya ubwabwa..pathetic
 
Tulikuwa tunajfanya upuuzi siku ya J5
Wenye akili hatukushiriki huu upuuzi
 
uchaguzi ni mchakato endelevu ambao muhisika hatakuwi kumessup hata hatua moja...

haya ni matokeo ya uvuguvugu na mawenge ya upinzani, hususani chadema tangu uandikishaji πŸ’
Uchaguzi hata ccm wenyewe hawawezi kuufurahia,
Ccm hawana furaha, upinzani hawana furaha,

Hata mama yenu hana furaha
Tuko pabaya ingawa chawa hamuoni tatizo


Nchi yenye watu walio huzuni mioyoni hawezi endelea hata mkijilazimisha furaha
 
Ile haukuwa uchaguzi ni upuuzi tu
 
Uchaguzi hata ccm wenyewe hawawezi kuufurahia,
Ccm hawana furaha, upinzani hawana furaha,

Hata mama yenu hana furaha
Tuko pabaya ingawa chawa hamuoni tatizo


Nchi yenye watu walio huzuni mioyoni hawezi endelea hata mkijilazimisha furaha

Gentleman,
Furaha ya CCM ni kumaliza uchaguzi wa kihistoria kwa amani,
Furaha ya CCM ni kuwaletea wanainchi maendeleo , na siyo hayo makhalakhancha umeandika πŸ’
 
kila moja kavuna alichopanda kwa wanainchi.

Imani ya waTanzania imeamua uelekeo wa Taifa.
Hongera sana CCM kwa ushindi wa kishindo.

Shukrani sasa vyama vingine kwa kushiriki uchaguzi kwa amani.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi πŸ’
 
Kwani kulikuwa na uchaguzi au uchafuzi? Kungekuwa na uchaguzi Chadema wangeshinda sana tu kwa hali ilivyo. Maana, chawa huwa hawapigi kura.
 
kila moja kavuna alichopanda kwa wanainchi.

Imani ya waTanzania imeamua uelekeo wa Taifa.
Hongera sana CCM kwa ushindi wa kishindo.

Shukrani sasa vyama vingine kwa kushiriki uchaguzi kwa amani.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi πŸ’
Kidumu wewe uangamie hata leo mwanangu. Kwanini unajilaani kijinga hivi mwanangu?
 
Gentleman,
Furaha ya CCM ni kumaliza uchaguzi wa kihistoria kwa amani,
Furaha ya CCM ni kuwaletea wanainchi maendeleo , na siyo hayo makhalakhancha umeandika πŸ’
Dogo chawa. Kwa akili hizi nikubaliane na trump aliye waita waafrica shit holes,

Pia nikubaliane na watafiti wanasema waafrika binadamu ambao bado hawajakamilika bado Wana undergo revolution

Population kubwa ya supporter wa ccm ni shit holes
 
Sisi wengi Wetu humu jukwaani ni watu huru hatuna njaa, hatununuliki, na hatufungamani na vyama

Lakini upuuzi kama wa .kabla na siku ya j5 siku ya uchaguzi ni upuuzi
 
Wangeacha ngonjera utoto na upuuzi wangeshinda zaidi ya hivyo!
 
elezea kwa ufupi kwa faida ya wadau,
huenda wakakuhurumia japo fomu ya uteuzi ulishindwa kuhaza kwa usahihi gentleman πŸ’
Yaani kwa vigezo vyenu hapo ulipoandika "kuhaza" unaliwa kichwa
 
mbona mnatuchanganya haya matokeo yapo tofauti tofauti na mnasema ya jumla?
 

Attachments

  • 1732849390631.jpg
    244.2 KB · Views: 1
Binafsi kilichonishangaza ni jinsi CUF ni king'ang'anizi yaani pamoja na promo ya ACT Wazalendo lakini Bado CUF inawatesa yaani watu wanaikumbuka CUF kuliko ACT.

Ziti amefeli kama Chadema walivyofeli πŸ˜†πŸ˜†
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…