Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Matokeo ya jumla ya uchaguzi kutangazwa muda wowote kuanzia sasa.
Uandikishaji wa Wapiga Kura
Zoezi lolifanyika Octoba 11 mpaka 20, 2024 ambapo jumla ya wapiga kura Milioni 31,282,331 walijiandikisha, baada ya mapingamizi wananchi waliojiandikisha walikuwa Milioni 31,255,303
Kupiga Kura
Wananchi waliopiga kura Novemba 27, 2024 walikuwa milioni 26,963,182 ambayo ni sawa na 86.36% ya wananchi waliokuwa na sifa ya kupiga kura.
Uteuzi wa Wagombea
Tar 26 Oktoba mpaka 1 Novemba ilikuwa zoezi la wagombea kuchukua na kurejesha fomu kwaajili ya uteuzi wa nafasi za Uenyekiti wa Kijiji, Uenyekiti wa Kitongoji, Mwenyekiti wa Mtaa, Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji na Wajumbe wa Kamati za Mitaa
Wagombea Walioteuliwa
Jumla ya wagombea walioteuliwa baada ya mchakato wa rufani kwa kila nafasi katika vyama vyote 19 vyenye usajili kamili ni kama ifuatavyo
Mwenyekiti wa kijiji - 18340
Mwenyekiti wa Mtaa - 7545
Mwenyekiti wa Kitongoji - 85522
Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji kundi mchanganyiko - 160,371
Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji kundi la wanawake - 108,166
Wajumbe wa Kamati za Mitaa kundi mchanganyiko - 18552
Wajumbe wa Kamati za Mitaa Wanawake - 11762
Kampeni
Kampeni zilifanyika kwa siku 7 kuanzia Novemba 20, 2024 mpaka Novemba 27, 2024 kwa kuzingatia kanuni na miongozo ya serikali za mitaa, kampeni zilifanyika kwa amani na utulivu kwa kipindi chote cha kampeni kwenye maeneo mengi, kwa kuzingatia ratiba zilizoratibiwa na vyama vyote katika maeneo husika.
Matokeo ya Uchaguzi:
Ndugu Wanahabari, baada ya kukamilika kwa zoezi la kampeni, jana tarehe 27 Novemba, 2024 wananchi walitumia haki yao ya kikatiba kuchagua viongozi watakaowaongoza katika kipindi cha miaka mitano. Hivyo, naomba nitumie nafasi hii kuujulisha umma wa Watanzania kuhusu matokeo ya uchaguzi huo kwa mujibu wa nafasi zilizogombewa kama ifuatavyo:-
i) Nafasi za Mwenyekiti wa Kijiji:
Ndugu Wanahabari, maeneo yaliyofanya uchaguzi terehe 27 Novemba, 2024 kwa nafasi ya Mwenyekiti wa Kijiji ni 12,271 kati ya nafasi 12,280 zilizopaswa kufanya uchaguzi. Kati ya nafasi hizo, CCM imeshinda nafasi 12,150 sawa na asilimia 99.01, CHADEMA imeshinda nafasi 97 sawa na asilimia 0.79, ACT Wazalendo imeshinda nafasi 11 sawa na asilimia 0.09, CUF imeshinda nafasi 10 sawa na asilimia 0.08, NCCR Mageuzi imeshinda nafasi 1 sawa na asilimia 0.01, UMD imeshinda nafasi 1 sawa na asilimia 0.01 na ADC imeshinda nafasi 1 sawa na asilimia 0.01. Aidha, vijiji 9 havikufanya uchaguzi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo vifo vya wagombea baada ya uteuzi.
Kupata taarifa na matukio ya kimkoa kuhusu Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
ii) Nafasi za Mwenyekiti wa Mtaa:
Ndugu Wanahabari, maeneo yaliyofanya uchaguzi terehe 27 Novemba, 2024 kwa nafasi ya Mwenyekiti wa Mtaa ni 4,264 kati ya nafasi 4,264 zilizopaswa kufanya uchaguzi.
Kati ya nafasi hizo, CCM imeshinda nafasi 4,213 sawa na asilimia 98.83, CHADEMA imeshinda nafasi 36 sawa na asilimia 0.84, ACT Wazalendo imeshinda nafasi 9 sawa na asilimia 0.21, CUF imeshinda nafasi 4 sawa na asilimia 0.09 na CHAUMA imeshinda nafasi 1 sawa na asilimia 0.02.
Aidha, katika mtaa mmoja wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga hakupatikana mshindi kwa sababu kura za wagombea wawili zilifungana.
iii) Nafasi za Mwenyekiti wa Kitongoji:
Ndugu Wanahabari, maeneo yaliyofanya uchaguzi terehe 27 Novemba, 2024 kwa nafasi ya Mwenyekiti wa Kitongoji ni 63,849 kati ya nafasi 63,886 zilizopaswa kufanya uchaguzi. Kati ya nafasi hizo, CCM imeshinda nafasi 62,728 sawa na asilimia 98.26, CHADEMA imeshinda nafasi 853 sawa na asilimia 1.34, ACT Wazalendo imeshinda nafasi 150 sawa na asilimia 0.23, CUF imeshinda nafasi 78 sawa na asilimia 0.12, NCCR-Mageuzi imeshinda nafasi 10 sawa na asilimia 0.02, UDP imeshinda nafasi 6 sawa na asilimia 0.01, UMD imeshinda nafasi 2 sawa na asilimia 0.003 na ADC imeshinda nafasi 1 sawa na asilimia 0.002.
Aidha, vitongoji 37 havikufanya uchaguzi tarehe 27 Novemba, 2024. Kati ya hivyo, vitongoji 8 havikufanya uchaguzi kwa kuwa wagombea wake walifariki baada ya zoezi la uteuzi. Wagombea hao walitoka katika Halmashauri za wilaya za Kilwa (2), Nanyumbu (1), Itilima (1), Ikungi (1), Manyoni (1), Uyui (1) na Mbarali (1). Aidha, vitongoji 29 havikufanya uchaguzi kutokana na sababu mbalimbali.
Vitongoji 12 vitarudia uchaguzi kwa kuwa matokeo ya wagombea yalifungana. Vilevile, vitongoji 9 vitarudia uchaguzi kutokana na wagombea pekee kutopata kura za kutosheleza.
iv) Nafasi za Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji:
Ndugu Wanahabari, matokeo ya nafasi za Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji ni kama ifuatavyo, CCM imeshinda nafasi 229,075 sawa na asilimia 99.31, CHADEMA imeshinda nafasi 1,222 sawa na asilimia 0.53, ACT Wazalendo imeshinda nafasi 232 sawa na asilimia 0.1, CUF imeshinda nafasi 105 sawa na asilimia 0.05, NCCR Mageuzi imeshinda nafasi 16 sawa na asilimia 0.01, Demokrasia Makini imeshinda nafasi 3 sawa na asilimia 0.001, NLD imeshinda. nafasi 1 sawa na asilimia 0.0004 na ADC imeshinda nafasi 1 sawa na asilimia
v) Nafasi za Wajumbe wa Kamati ya Mtaa:
Ndugu Wanahabari, matokeo ya nafasi za Wajumbe wa Kamati ya Mtaa ni kama ifuatavyo, CCM imeshinda nafasi 21,148 sawa na asilimia 99.30, CHADEMA imeshinda nafasi 101 sawa na asilimia 0.47, ACT Wazalendo imeshinda nafasi 29 sawa na asilimia 0.14, CUF imeshinda nafasi 16 sawa na asilimia 0.08, NCCR Mageuzi imeshinda nafasi 2 sawa na asilimia 0.01, CCK imeshinda nafasi 1 sawa na asilimia 0.005 na ADC imeshinda nafasi 1 sawa na asilimia 0.005.
Ndugu Wanahabari, maeneo ambayo hayakufanya uchaguzi yatapaswa kuzingatia Kanuni ya 21 ya Tangazo la Serikali Na. 571, 573 na 574 na Kanuni ya 20 ya Tangazo la Serikali Na. 572 ili maeneo hayo yaweze kufanya uchaguzi na kupata viongozi wao. Kanuni hizo zinaelekeza endapo baada ya uteuzi kufanyika, mgombea wa nafasi husika atafariki, Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi ataahirisha uchaguzi wa nafasi husika na Chama cha Siasa kilichotoa mgombea aliyefariki kinaweza kuwasilisha jina la mwombaji mwingine ndani ya siku. arobaini tangu kuahirishwa kwa uchaguzi ili hatua za uteuzi wa mwombaji huyo zifanyike.
Aidha, kwa mujibu wa kanuni ya 37 ya Tangazo la Serikali Na. 571, 573 na 574 na Kanuni ya 36 ya Tangazo la Serikali Na. 572 endapo siku ya kupiga kura kutatokea jambo lolote litakalozuia upigaji kura kuendelea kufanyika, Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi ataahirisha upigaji kura hadi siku inayofuata au siku nyingine anayoona inafaa ambayo haitazidi siku saba tangu siku uchaguzi ulipoahirishwa.
Hivyo, ninawaelekeza Wasimamizi wa Uchaguzi kuzingatia Kanuni hizo katika maeneo yote ambayo hayakufanya uchaguzi siku ya tarehe 27 Novemba, 2024 kutokana na sababu mbalimbali.
Ndugu Wanahabari, nitumie nafasi hii kuwashukuru vyama vingine ambavyo vilishiriki vizuri kwa kunadi sera zao lakini havikuweza kufanikiwa kupata nafasi katika Uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa. Niendelee kuwasihi kuwa ukuaji wa demokrasia ni mchakato hivyo, waendelee kuwa wamoja na kushiriki katika chaguzi zijazo.
Ndugu Wanahabari, naomba nihitimishe taarifa yangu kwa kutoa shukrani za dhati kwa viongozi wakuu wote, vyombo vya ulinzi na usalama, vyama vya siasa, vyombo vya habari, taasisi za dini, viongozi wa kimila, asasi za kiraia, wasanii, watumishi wa umma na sekta binafsi na wananchi wote kwa ushirikiano mkubwa waliouonyesha katika kipindi chote cha mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa tunathamini na kutambua mchango wao.
Kipekee, napenda kuvishukuru vyama vyote 19 vya siasa vyenye usajli kamili ambavyo vimeonyesha ukomavu mkubwa wa kisiasa wa kudumisha demokrasia nchini kwa kushiriki kikamilifu mchakato mzima wa uchaguzi huu kuanzia kwenye maandalizi ya Kanuni za Uchaguzi, kuhamasisha na kutoa elimu kwa wananchi, kushiriki kampeni na kugombea nafasi hizo.
Nitumie fursa hii kuvitambua vyama hivyo ambavyo ni CCM, CUF CHADEMA, UMD, NCCR Mageuzi, NLD, UPDP, NRA, ADA-TADEA, TLP, UDP, Demokrasia Makini, DP, SAU, AAFP, CCK, ADC, CHAUMA na ACT-Wazalendo,
Vilevile, natoa shukrani zangu za dhati kwa Wagombea wote walioshiriki katika uchaguzi huu kwa kiwango kikubwa wameonyesha uzalendo mkubwa wa kuchukua fomu, kunadi sera za vyama vyao, kushiriki nafasi mbalimbali za uchaguzi na wengine kuibuka washindi siku ya jana yaani tarehe 27 Novemba, 2024. Niwakumbushe kuwa mwisho wa uchaguzi huu ni mwanzo wa maandalizi ya uchaguzi ujao hivyo waendelee kujiimarisha ili kushiriki chaguzi zijazo kwa ufanisi zaidi.
Ndugu Wanahabari, niwashukuru viongozi wote wa Serikali kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali kwa ushiriki wao katika mchakato wa uchaguzi huu. Nishukuru na kuwapongeza viongozi wenzangu na watumishi wote wa Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Viongozi wa Mikoa, Wilaya, Halmashauri, Tarafa, Kata, Vijiji na Mitaa pamoja na vitongoji vyote nchini kwa ushiriki wao katika kufanikisha uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa Mwaka, 2024.
Ndugu Wanahabari, niwashukuru Wananchi wote walioshiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa kwa mwaka, 2024. Wananchi wengi walijitokeza kujiandikisha, kugombea nafasi mbalimbali na kupiga kura kwa amani na utulivu. Huu ndio utamaduni wa watanzania na tunu tuliyoachiwa na waasisi wa Taifa letu.
Ndugu Wanahabari, kwa kuhitimisha napenda niwapongeze wagombea wote walioshinda kwenye nafasi zote za uongozi za Mwenyekiti wa Kijiji, Mwenyekiti wa Mtaa, Mwenyekiti wa Kitongoji, Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji na Wajumbe wa Kamati ya Mtaa.
Aidha, niwatakie utekelezaji mwema wa majukumu yao kwa kuzingatia utawala wa sheria katika kuwahudumia watanzania wote bila ubaguzi. Nichukue fursa hii kuwaelekeza Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha Viongozi wateule wanaapishwa ndani ya siku 14 baada ya siku ya uchaguzi na kupewa mafunzo kabla ya kuanza kutekeleza majukumu yao ikiwa ni pamoja na kukabidhiwa vitendea kazi muhimu.
Ndugu wanahabari, sasa nitamke rasmi kuwa, pazia la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwaka, 2024 limefungwa.
MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA
AHSANTE SANA KUNISIKILIZA
Mohamed O. Mchengerwa (Mb.)
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS
(TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA ΜΙΤΑΑ)