Baraka Mina
JF-Expert Member
- Sep 3, 2020
- 586
- 590
Hamashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) iliyokutana katika kikao chake cha kawaida makao makuu ya chama hicho jijini Dodoma leo Jumapili, Julai 9, 2023, chini ya Uenyekiti wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na mambo mengine imejadili mkabata wa makubaliano ya uwekezaji na uendelezaji wa bandari nchini.
Mkataba huo ni baina ya Serikali ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na Serikali ya Dubai kupitia Kampuni yake ya Dubai Port World ambao tayari Bunge la Tanzania limeridhia ushirikiano huo.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Sophia Mjema amewaambia waandishi wa habari kuwa, Halmashauri Kuu imepokea na kujadili kwa kina taarifa ya makubaliano ya uwekezaji na uendeshaji wa bandari na kuazimia ifuatavyo; uwekezaji na uendeshaji wa bandari ni kwa manufaa ya uchumi wa nchi.
Uwekezaji huo ni utekelezaji wa vitendo wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020–2025, ibara ya 59, ukurasa wa 92. Serikali iongeze kasi ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya uhalisia uliomo katika makubaliano ya uwekezaji na uendeshaji huo wa bandari,” amesema Mjema.
=====
Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC) imepokea na kujadili kwa kina taarifa ya makubaliano ya uwekezaji na uendeshaji wa bandari baina ya Serikali ya Tanzania na ya Dubai wakibariki mchakato huo.
Katika kikao chake kilichoketi makao makuu ya CCM, jijini Dodoma leo Jumapili Julai 9, 2023 chini ya Mwenyekiti wake, Rais Samia Suluhu Hassan, kikao hicho kimesema uwekezaji na uendeshaji wa bandari ni kwa manufaa ya uchumi wa nchi.
Taarifa fupi iliyosomwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Sophia Mjema mbele ya waandishi wa habari ilesema uwekezaji huo ni utekelezaji wa vitendo wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/25, Ibara ya 59, ukurasa wa 92.
Hata hivyo, Mjema amesema kikao kimekubaliana kuwa, Serikali iendelee kutoa elimu kwa kwa wananchi katika jambo hilo.
"Serikali iongeze kasi ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya uhalisia uliomo katika makubaliano ya uwekezaji na uendeshaji huo wa bandari," amesema Mjema.
Halmashauri hiyo ilifanyika baada ya kutanguliwa na kikao cha Kamati Kuu ambapo pia imezipongeza Serikali zote mbili za Chama Cha Mapinduzi, Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi.
Katika mkutano huo na waandishi, Mjema amesema siyo siku ya kujibu maswali kwani yeye amesoma kile ambacho wamekubaliana na Halmashauri na mambo mengine yasubiri wakati wake.
Habari zaidi, soma:
Mkataba huo ni baina ya Serikali ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na Serikali ya Dubai kupitia Kampuni yake ya Dubai Port World ambao tayari Bunge la Tanzania limeridhia ushirikiano huo.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Sophia Mjema amewaambia waandishi wa habari kuwa, Halmashauri Kuu imepokea na kujadili kwa kina taarifa ya makubaliano ya uwekezaji na uendeshaji wa bandari na kuazimia ifuatavyo; uwekezaji na uendeshaji wa bandari ni kwa manufaa ya uchumi wa nchi.
Uwekezaji huo ni utekelezaji wa vitendo wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020–2025, ibara ya 59, ukurasa wa 92. Serikali iongeze kasi ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya uhalisia uliomo katika makubaliano ya uwekezaji na uendeshaji huo wa bandari,” amesema Mjema.
=====
Katika kikao chake kilichoketi makao makuu ya CCM, jijini Dodoma leo Jumapili Julai 9, 2023 chini ya Mwenyekiti wake, Rais Samia Suluhu Hassan, kikao hicho kimesema uwekezaji na uendeshaji wa bandari ni kwa manufaa ya uchumi wa nchi.
Taarifa fupi iliyosomwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Sophia Mjema mbele ya waandishi wa habari ilesema uwekezaji huo ni utekelezaji wa vitendo wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/25, Ibara ya 59, ukurasa wa 92.
Hata hivyo, Mjema amesema kikao kimekubaliana kuwa, Serikali iendelee kutoa elimu kwa kwa wananchi katika jambo hilo.
"Serikali iongeze kasi ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya uhalisia uliomo katika makubaliano ya uwekezaji na uendeshaji huo wa bandari," amesema Mjema.
Halmashauri hiyo ilifanyika baada ya kutanguliwa na kikao cha Kamati Kuu ambapo pia imezipongeza Serikali zote mbili za Chama Cha Mapinduzi, Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi.
Katika mkutano huo na waandishi, Mjema amesema siyo siku ya kujibu maswali kwani yeye amesoma kile ambacho wamekubaliana na Halmashauri na mambo mengine yasubiri wakati wake.
Habari zaidi, soma:
- Sakata la DP WORLD: Rais Samia asema Serikali itatafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar, sasa kuchangia robo tatu ya bajeti ya nchi
- Dodoma: Bunge lapitisha azimio la kuunga mkono mkataba wa Tanzania na DP World
- DOKEZO - Malalamiko ya mkataba wa DP World yapelekwe CCM, Rais Samia hana makosa sababu anatekeleza sera za chama chake
- DP WORLD: Mkataba unaoongelewa sana huu hapa (Kiswahili)