Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tunasalitiwa na Watanganyika wenzetu. Disgusting
Bila katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi sihangaiki kwenda kunajisi nafsi yangu. Samia ni muuaji kbs.Kwani tumepinga mkataba au tumepinga upumbavu na ujuha wa kiwango cha lami uliopitishwa na wapewa rushwa huku wakiwa hawaangalii maslahi ya taifa
Comments reservedHamashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) iliyokutana katika kikao chake cha kawaida makao makuu ya chama hicho jijini Dodoma leo Jumapili, Julai 9, 2023, chini ya Uenyekiti wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na mambo mengine imejadili mkabata wa makubaliano ya uwekezaji na uendelezaji wa bandari nchini.
Mkataba huo ni baina ya Serikali ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na Serikali ya Dubai kupitia Kampuni yake ya Dubai Port World ambao tayari Bunge la Tanzania limeridhia ushirikiano huo.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Sophia Mjema amewaambia waandishi wa habari kuwa, Halmashauri Kuu imepokea na kujadili kwa kina taarifa ya makubaliano ya uwekezaji na uendeshaji wa bandari na kuazimia ifuatavyo; uwekezaji na uendeshaji wa bandari ni kwa manufaa ya uchumi wa nchi.
Uwekezaji huo ni utekelezaji wa vitendo wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020–2025, ibara ya 59, ukurasa wa 92. Serikali iongeze kasi ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya uhalisia uliomo katika makubaliano ya uwekezaji na uendeshaji huo wa bandari,” amesema Mjema.
Mwananchi
Endelea kusubiri hayo majibu, huku serikali ikiendelea na mishemishe zakoHoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa
1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)
2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?
3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?
4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!
6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
Povu kama lote!Hiyo kamati ya wajinga imekutana ikiongozwa na mawazo ya msaliti, ndio maana wamekuja na maazimio batili.
Kamati badala ituambie watanganyika, hayo manufaa ya uwekezaji wa bandarini yapo kwenye kifungu gani kwenye ule mkataba wa hovyo na waarabu, wanatuambia manufaa yapo kwenye ilani ya CCM, ibara ya 59, ukurasa wa 92!.
Kwani waarabu walisaini kwenye ilani ya CCM ya 2020-2025, au kwenye IGA?!
Halafu kuna wajinga wanaotaka hawa vilaza wakosolewe kwa sauti za kubembelezwa, Samia ni msaliti asiye na huruma na watanganyika.
Ndo washaamua sasaUjinga Pro Max ilani ya CCM siyo katiba ya Nchi
Tanganyika bila CCM inawezekana Bwashee😆😂 rudini kwenye TANU yenu.Sawa
Kwa katiba ipi. Hata hamfikirii tena issue za katiba wala tume ya uchaguzi.Utopolo! Ccm wametuzoea wananchi dawa yao ipo jikoni! 2025
Jibu hojaEndelea kusubiri hayo majibu, huku serikali ikiendelea na mishemishe zako
Wamekuibia nini mzeewezi wa taifa wez!i wa taifa! chama cha madalali.
😆😆😆 Si amekwambia ibara 59 ukurasa wa 92 wa ilani umeandikwa kwamba Bandari atapewa Mwarabu au haujamwelewa Sophia Mgema?,Mwenye taarifa kamili ya hiko kipengele cha ilani ya CCM kinachosema....Bandari igawiwe kwa Waarabu wakiweke hapa