CCM yatoa Baraka zote kwa DP World kufanya uwekezaji wa Bandari

Hiyo kamati ya wajinga imekutana ikiongozwa na mawazo ya msaliti, ndio maana wamekuja na maazimio batili.

Kamati badala ituambie watanganyika, hayo manufaa ya uwekezaji wa bandarini yapo kwenye kifungu gani kwenye ule mkataba wa hovyo na waarabu, wanatuambia manufaa yapo kwenye ilani ya CCM, ibara ya 59, ukurasa wa 92!.

Kwani waarabu walisaini kwenye ilani ya CCM ya 2020-2025, au kwenye IGA?!

Halafu kuna wajinga wanaotaka hawa vilaza wakosolewe kwa sauti za kubembelezwa, Samia ni msaliti asiye na huruma na watanganyika.
Ni Utumwa!
Picha hii chini inaonyesha na kusema ilipo CCM....ni Aibu kweli
20141018_MAP004_0.jpg
 
hongereni sana ccm mh Rais usisikileze kelele za wapigaji bandari hawa ni sawa na vita vya dawa za kulevya wauzaji wa madawa ukiwagusa tu kelele mwaka mzima
 
we utakuwa kada ama mtoto wa mama, nimefunga ukurasa.
Jibu hoja ,msingi wa hovyo kwako ni upi? Weka metrics hapa harafu useme unalinganisha na nani?

Sawa Mimi kada na wewe Pinga Pinga Kwa hiyo una shida zako binafsi kichwani.
 
Uelewa tu unakusumbua nenda Israel mwaka jana wao wameiuza kabisa bandari yao Haifa port kwa Adani group kwa bilioni 1.2 USD .unataka kuniambia waisraeli hawawezi kuijenga nchi yao?View attachment 2683361
Bado huja justify kwa nini waarabu wapewe makubaliano yasiyoisha, mind you hatujakataa uwekezaji, Ila uwekezaji wenye lengo la kunufaisha upande mmoja NO, Hafu usiniwekee link za kijinga Sio lazima tuwaige wao, kwa nini wasituige sisi,,,, mwisho Una ID ya kikristu halafu Sio mkristu tunawajua Nyie
 
Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
Nyie ni wajinga tu hoja zenu ni zile zile, mukiulizwa huo mkataba wa kupewa bandari zote uko wapi mna kenua tu meno, chuki mbaya sana ndo inao wasumbua.
 
Chadema tangu aondoke Dr Makene utoaji wao wa taarifa mbalimbali umekuwa wa kusuasua sana

Kamati kuu ya Chadema imeketi jana kujadili hali ya Kisiasa Nchini na mkataba wa DP World Lakini wametoka Kimya kimya

Wenzao CCM wameketi leo Jioni na taarifa wameshatoa

Chadema mnafeli sana!
 
Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
Hujibiwi. We endelea tu kusubiri
 
Chama Tawala CCM leo Julai 9, kimeketi kujadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa kauli juu ya makubaliano ya Uwekezaji na Uendeshaji wa Bandari nchini (IGA) baina Serikali ya Tanzania na Emirates of Dubai.
f2520d124f264398b8335dde54e37def.jpg
 
Kwani wewe unanihusu mpaka nisiongee ninayojisikia?
Kumbe waongeaongea tu unavyojisikia.
Mi si nlidhani na wewe wajipendekeza kuwa eti bandari yakuhusu. We endelea tu kusindikiza wenye bandari yao washaiuza
 
Yes naongea ninavyojisikia inakuuma kwani?!, bandari kaiuza Kumbe mnamtetea nini Huyo mama, soon na yeye ataenda kula urojo!
 
Back
Top Bottom