CCM Zanzibar yataka urais wa Muungano ugombewe kwa zamu kati ya Tanganyika na Zanzibar

CCM Zanzibar yataka urais wa Muungano ugombewe kwa zamu kati ya Tanganyika na Zanzibar

Kakke

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2010
Posts
1,883
Reaction score
1,483
ccm-kampeni-uzini-3-564x376.jpg


NAIBU KATIBU MKUU WA CCM ZANZIBAR VUAI ALI VUAI


Written by Harith - 12/01/2013



CHAMA CHA MAPINDUZI ZANZIBAR KIMEPENDEKEZA SUALA LA MGOMBEA WA NAFASI YA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWA TIKETI YA CHAMA HICHO KUWA YA KUPOKEZANA KATI YA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR.

HAYO YAMEELEZWA NA NAIBU KATIBU MKUU WA CCM ZANZIBAR VUAI ALI VUAI KWA MNASABA WA MAADHIMISHO YA MIAKA 49 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR AMBAYP KILELE CHAKE KIMEFIKIA LEO KATIKA UWANJA WA AMANI MJINI ZANZIBAR.

AIDHA KIONGOZI HUYO AMEONGEZA KUWA SUALA LA KUCHAGULIWA MWANASIASA KUTOKA ZANZIBAR KUPITIA MKUTANO MKUU WA CCM DODOMA ATAKAYEPEPERUSHA BENDERA YA CCM KATIKA UCHAGUZI WA RAIS WA ZANZIBAR LINAPASWA KUANGALIWA UPYA ILI WAZANZIBARI WAPENDEKEZE JINA LA MGOMBEA WAO WA URAIS WA ZANZIBAR WENYEWE.

MATAMSHI HAYO YA NAIBU KATIBU MKUU WA CCM (ZANZIBAR) YANAWEZA KUZUSHA MPASUKO NDANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI KUTOKANA NA KUANZA KAMPENI NA HARAKATI ZA CHINI KWA CHINI ZA BAADHI YA VIGOGO WA CHAMA HICHO UPANDE WA TANZANIA BARA ZAKUTAKA KUWANIA URAIS KATIKA UCHAGUZI MKUU UJAO WA MWAKA 2015.
 
Haya mapendekezo ya katiba ndiyo yataamsha mizimu yote ya mapungufu katika muungano. Nahisi kutakuwa na kutofautiana kwa kiwango kikubwa katika mapendekezo ya katiba kwa upande wa Visiwani na bara.
 
Hawa nao hawana kazi nyingine za kufanya? Kila siku ni Uzanzibari tu! Mara wanataka nchi yao, mara Uraisi wa kupokezana, Mara Muungano wa Mkataba. Hata hawajui wanalo litaka hawa Wagunya!!! Waishie zao CHUMBE kule!! Mbona SITAKI NATAKA kila kukicha????
 
Urais wa Muungano siyo taaluma ya kuandika mashairi
ya taarabu kama kina Mzee Yusufu na Alamba alamba
aaaaam tena alamaba aaaaam aaaaaam
 
Wazanzibar wamesema wamechoshwa na tabia ya CCM bara kuwapereka Dodoma na kuwachagulia Rais sasa wanataka wao kama CCM zanzibar watakuwa wanachagua wao Rais wamtakaye siyo kuburuzwa na CCM bara! Mimi naona sasa CCM imeishikwa pabaya sasa ndo mwanzo wakufa hiki chama! Na hawana ubavu wa kuwazuia ngoja tuone hii ngoma ninani ataicheza!
 
Wazanzibari acheni kuchekesha walionuna.Urais sio Kikombe cha ga-hawa;Watu makini wanachaguliwa kwa sifa walizonazo sio kwa upendeleo.Hii nafasi sio ya viti maalum.Nawashauri muombe kupendelewa Uspika maana zamu hii alipendelewa mwanamke huenda zamu ijayo mkapendelewa wazanzibari.
 
Ni Nyumba ya Mlevi tu ndio inayoweza kutimiza Matakwa haya.
 
Kama hivyo labda tuwe serikali 3 maana asaiv katiba inamruhusu mtu yoyote kua rais anaweza akawa anatoka Zanzibar au bara, ili mradi tuu asimamishwe na chama chake na achaguliwe na watu, na hawa CCM Zanzibar kama hawataki kuchaguliwa rais toka Dodoma si watakua wapo bega kwa bega na uamsho? Maana uamsho si wanataka zanzibar yenye kujiendesha yenyewe? Iweje leo CCM wagome kuchaguliwa rais toka Dodoma? Mi nahisi washaamka hawa.

Tukiwa na serikali ya Zanzibar, serikali ya Tanganyika na serikali ya muungano hapo watakua na haki ya kusema rais wa muungano awe kwa zamu, ila kwa sasa wasahau maana haijakatazwa raisi kutoka Zanzibar just apitishwe tuu na chama chao uchaguzi ufanyike na akipita basi atakua rais
 
Labda wapewe uraisi wa viti maalum!

znz haihitaji urais wa viti maalum, na wala haipaswi kung'ang'ania zamu ili kupata Urais wa jmt. inaye kiongozi wake anayechaguliwa kidemokrasia na waznz. La msingi ni kuweka mfumo utakaomuwezesha kiongozi huyu kuwa na mamlaka kamili kwa mambo yahusuyo znz na ku"share", mamlaka na udhibiti wa dola na usalama wa taifa letu, pamoja na viongozi wakuu wa jmt na tanganyika waliochaguliwa kidemokrasia. Ku share huko kunapaswa kuwepo muda wote. Sasa zamu ya nini hapo tena. Kama gwaride la heshima, wimbo wa taifa,kuweka hali ya vita kiongozi mznz si yatakuwa yanamhusu wakati wote tu badala ya kutegemea zamu.
 
Wanaota mchana.

Hili haliwezekani ikizingatiwa kuwa kuna watu wanaweza kulitumia kufanya mambo yao kama Salim na Karume walivyojaribu na kushindwa
 
zinawatosha wenyewe. watu milioni 45 wapeane zamu sawa na watu milioni 2? kichekesho kisicho chekesha.
 
Rais wa jamhuri akitoka huko huku hakuna atakaempigia kura. Maana upande mmoja utakuwa umetoa marais wawili. Rais wa jamhuri kwa mfano akitoka Zanzibar na rais wa Zanzibar atatoka wapi?
 
Rais wa jamhuri akitoka huko huku hakuna atakaempigia kura. Maana upande mmoja utakuwa umetoa marais wawili. Rais wa jamhuri kwa mfano akitoka Zanzibar na rais wa Zanzibar atatoka wapi?

Rais wa Zanzibar atatoka Zanzibar kwa kuchaguliwa na wazanzibari...kumbe Tanganyika ni Jamhuri? mm nilidhani imeshirikiana na Nchi jirani kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar?
 
zinawatosha wenyewe. watu milioni 45 wapeane zamu sawa na watu milioni 2? kichekesho kisicho chekesha.

kichekesho cha nini kwani watanganyika hamukuambiwa kama muliungana na chi jirani ya Zanzibar? na sheria za kuungano maanake kila kitu kinachohusu muungano ni kugawana sawa sawa kama nchi mbili tofauti mkuu😱hwell:
 
Back
Top Bottom