CCM Zanzibar yataka urais wa Muungano ugombewe kwa zamu kati ya Tanganyika na Zanzibar

CCM Zanzibar yataka urais wa Muungano ugombewe kwa zamu kati ya Tanganyika na Zanzibar

FJM, Jasusi, Nguruvi3, Mzee Mwanakijiji,

..I hope tume ya katiba italipuuza pendekezo hilo.

..kwanini wasipendekeze Uraisi tuwe tunapokezana kati ya wanaume na wanawake?

NB:

..halafu CDM hawana support ZNZ na hawatakiwi kabisa huko visiwani.

..labda huo ni ujanja wao wa kutaka kuungwa mkono ZNZ.

Maoni ya CCM hayajawekwa hadharani (I wonder why?) although inajulikana kuwa wanataka serikali mbili but hatujui kama wamependekeza urais upatikane kivipi? Lakini pia kuna dalili CCM Bara hawako kwenye ukarasa mmoja na CCM Zanzibar, na hapa ndipo kunaleta utata mwingine.
 
Nonda,

..ndiyo maana wengine tunapendekeza Tanganyika huru, na Zanzibar huru, zitakazokuwa na "muungano wa mkataba"/mashirikiano kupitia East African community.

..EAC ina secretariat ambayo inaongozwa na Katibu Mkuu, ambaye anapatikana kwa utaratibu wa kupokezana member states.

Hili ndio lipigiwe kampeni.

Kwa nini tunajichanganya kimawazo?

Hii kauli iwe kauli ya watanganyika na sio watanzania au watanzania bara.

Sijui kama tunazungumza lugha moja hapa.

CCM wanafanya "mazingaombwe yao" ambayo MMJ na Nguruvi3 wameyakumbatia.

CHADEMA mmeanza kuwalaumu na mko dissappointed nao kwa kauli yao.

Sasa tutokee wadanganyika wengi, tuseme, rudisha Tanganyika huru, rudisha Zanzibar huru. Kiini macho kitafikia ukomo siku hiyo.

Ratio 43:1

Nani anaendeleza kiini macho/mazingaombwe haya? Yet, we blame wala urojo!

Something is not right with us,wadanganyika!
 
Sidhani kama mapendekezo ya CDM mengine yamefikiriwa vizuri; inaonekana kama hayakufikiriwa kwa kina na hasa implications zake.
 
Nonda,

..ndiyo maana wengine tunapendekeza Tanganyika huru, na Zanzibar huru, zitakazokuwa na "muungano wa mkataba"/mashirikiano kupitia East African community.

..EAC ina secretariat ambayo inaongozwa na Katibu Mkuu, ambaye anapatikana kwa utaratibu wa kupokezana member states.
Nonda jibu hili hapa.
 
Hili ndio lipigiwe kampeni.

Kwa nini tunajichanganya kimawazo?

Hii kauli iwe kauli ya watanganyika na sio watanzania au watanzania bara.

Sijui kama tunazungumza lugha moja hapa.

CCM wanafanya "mazingaombwe yao" ambayo MMJ na Nguruvi3 wameyakumbatia.

CHADEMA mmeanza kuwalaumu na mko dissappointed nao kwa kauli yao.

Sasa tutokee wadanganyika wengi, tuseme, rudisha Tanganyika huru, rudisha Zanzibar huru. Kiini macho kitafikia ukomo siku hiyo.

Ratio 43:1

Nani anaendeleza kiini macho/mazingaombwe haya? Yet, we blame wala urojo!

Something is not right with us,wadanganyika!
Nonda hebu pitia nyuzi zangu vizuri, siku zote nimesema tukutane EAC hakuna njia ya mkato. Rekodi zaidi ya 100 zipo.

Bado nasema hakuna njia ila EAC. Mapendekezo yote ya bara hayakubaliwi na ZNZ. Njia muafaka ni EAC nakuhakikishia kwasababu hatutakubali kupokezana madaraka, wala kubeba mzigo wowote wa ZNZ. Tutaelimisha umma kila kipengele na implication zake na kuhamasisha kura ya kupinga. Hilo lipo na ZNZ hina uwezo wa kulizuia.
 
CCM ni wale wale hakuna cha bara wala visiwani....
Sawa lakni safari hii watashikana mashati kwakuwa wabara urais wanautaka na zanzibar wanautaka kitaeleweka!Na wa bara hawako tayari kwa hilo labda baada ya katiba mpya!
 
Mbona kwenye uchangiaji gharama hatutoi sawa?Hebu tujikumbushe;Kila upande umetoa Wajumbe sawa wa Tume ya Marekebisho ya Katiba.Je!Zanzibar imeshiriki kuwalipa?.Kwa mambo kama haya ndio maana Wazanzibar mnaonekana mnacheza ngoma ya kitoto.
Si mulipigania sarafu iwe ya muungano na mali asali basi hiyo ndio mpango wote pesa zote zitoke katika central bank ya Tanzania kwa kuiangalia nchi ya zanzibar na nchi ya tanganyika, upo mkuu?
kama hamutaki hivyo murudishe mabilioni ya pesa za zanzibar mulizochukua kwa kuanzisha benki kuu ya Tanzania:shut-mouth:
 
Waseme kwenye vikao halali,wakisemea nje inakuwa kama wameweka pamba masikioni,wapeleke hoja ili tuone kama kweli wako serious!
 
tusiwe wabinafsi na wapenda kutawala sisi tu. kwakuwa wako wachache mtu kutoka kule ashike baada ya vipndi 3 au 4 vya miaka 5. hii iwe kama hajatokea wa kuweza kupata urais kutoka zenj kwa kipind hicho mfululizo. tatizo kwetu urais ni kama umungu. kwahiyo tunaona hatuwez kuwapa umungu mtu wa zenj. turekebishe katiba yetu rais asiwe kama mungu then tutaona sawa tu hata akitoka zenj
 
Kwani rais wa muungano anatawala pia Zanzibar? Mbona mi naona kama rais wa Zanzibar anafanya kila kitu cha kule sanasana imebaki kwenye maandiko tu, kwamba kuna rais wa Muungano na wa Zanzibar. Hata kunapokuwa na sherehe kule Zanzibar huwa naona anatangulia kuingia rais wa muungano kisha anaingia mwenyekiti wa baraza la mapinduzi, hii Inaonesha kuwa wanapokuwa kule rais wa muungano ni wa Tanganyika na kwa hiyo anaenda kama mwalikwa tu, hivo analazimika kufika Kabila mwenye nchi hajafika. Sasa wanataka waongoze kote?
 
Moja ya swifa ya WaZnz ambayo wengi wa changangiaji humu barzani hususan kutoka upande wa pili wa mvungano wenu wanaseama WANALALAMKA sana jambo ambalo ni zuri kwa kustakabali wa taifa la Znz. na siku zote kunapotokea kutetea maslah ya Znz hapa hakuna siasa wote kitu kimoja.

Tatizo kubwa la watu kutoka Bara wao wanapenda KUNUNG'UNIKA kwa kila jambo jambo ambalo linaua mustakabali wa nchi yao ya Tanganyika. Hakika manung'uniko ni chanzo cha UNAFIKI na mwisho wa kunung'unika ni KUSONONEKA ambapo ni kukata tamaa na kufa kwa Taifa. Mola anusuru msifikie huko.

Hongera Znz kuweka mambo bayana.
 
Nonda jibu hili hapa.

Nguruvi3

Sasa mshawishi na dugu yako, MMJ aandae makala moja safi ya kuipigia debe, Tanganyika huru na Zanzibar huru.

Kama hili umelikubali basi safari imeanza.

Uache masimulizi ya Seif, Jussa wakati Tanganyika haina mtetezi.

Weka fikra pevu moja juu ya Tanganyika huru na Zanzibar huru.

Unajua Mkuu Nguruvi3, wewe na ndugu yako (yetu), MMJ mna kundi kubwa(wapenzi/wafuasi wengi) hapa JF lakini baada ya kutumia ushawishi huo wa kukubalika vizuri, mnaleta maneno mengi, mnawazingua watu hapa kama CCM inavyotuzingua wadanganyika.

Sasa tutumie ushawishi huo kuitetea Tanganyika...Tanganyika huru inawezekana ikiwa tu wadanganyika tutakubali kuiondoa "d" na kuweka "t" kutoka moyoni.

Ni lazima tuwe watanganyika ndio tutaweza kutetea haki/ masilahi ya Tanganyika. Vyenginevyo, tutakuwa tunakimbiza kivuli tu na kuwatupia lawama Seif na Jussa.

Jiangalie kwenye kioo leo, halafu anza kujiambia,tamka "mimi ni mtanganyika na nitatetea masilahi ya Tanganyika"

Najua itakuwa ngumu kujibadili kutoka mtanzania bara/ mbara uliyoizoea lakini safari ya maili elfu huanza kwa kupiga hatua ya mwanzo.

1,2,3 "Mimi si mdanganyika bali ni mtanganyika"

Jaribu tena...1,2,3 "Mimi Nguruvi3 ni mtanganyika" "Nitatetea masilahi ya Tanganyika"
 
Back
Top Bottom