CCM Zanzibar yataka urais wa Muungano ugombewe kwa zamu kati ya Tanganyika na Zanzibar

CCM Zanzibar yataka urais wa Muungano ugombewe kwa zamu kati ya Tanganyika na Zanzibar

Ndugu umenikosha kweli uliposema kuwa urais wa zanzibar apewe mtanganyika kama sisi tunataka kuongoza serikali ya muungano. Nafikiri hujui kama tanganyika hakuna serikali. Kaa kitako utambue kuwa serikali ya tanzania sio serikali ya tanganyika, hivo basi kwa definitiona kila mtanzania ana haki ya kugombea urais wa JMT, na serikali ya zanzibar ni ya wazanzibari, sio serikali ya muungano ile, serikali ile inatakiwa iendelee kuongozwa na mzanzibari TU! Soma tofauti kati ya JMT na SMZ!
usiweke conditions kuwa lazima ati kuwepo serikali ya Tanganyika ndo mtu agombee kiti cha urais Zanzibar.
Muundo uliopo tosha kabisa, kwa vile mwapenda kupewa kiti cha urais wa Muungano, wekeni rehani kiti cha urais Zanzibar ili mtanganyika aweze kugombea kwazamu zile zile mzipendazo.

Hapo ndo utatambua unafiki wa waZanzibari kujificha nyuma ya visingizio visivyoisha.
Wengi wanafikiri Muungano shamba la bibi.
 
Nguruvi3

CHADEMA; CUF wanataka serikali tatu.
Mjadala wa kupokezana urais wa serikali ya Muungano umeshika kasi.

Kuna watoa maoni huku Tanganyika pia wanadai serikali ya Tanganyika irudi.

Tusisahau juhudi za G55 na Rev. Mtikila.

Ni wazi, Tanganyika inarudi sio kwa sababu ya matwakwa ya Wazanzibari lakini ni kwa sababu tupo watanganyika ambao tunaelewa Muungano kama ulivyo leo ni "kiini macho".

Linapokuja suala la muungano ni wazi kuwa wabia huwa wanahitajiana/ huwa kuna masilahi fulani kwa kila upande unaojiunga katika Muungano. Kama Tanganyika iliona ni jambo jema kuingia katika muungano na Zanzibar 1964 basi kutokana na utete wa siasa ulivyo huku "Tanzania bara" siku Zanzibar ikitoka Muungano ndio tutaelewa umuhimu wake.

Kufikiria kuwa Tanganyika haihitaji Zanzibar, basi Mwalimu Nyerere angeruhusu G55 ilete serikali ya Tanganyika.

Hata wewe unaelewa vipi Zanzibar imesaidia kuifanya Tanganyika isimeguke. Kama hili hulielewi naomba ufanye utafiti. Au soma kwa makini au sikiliza kwa makini hotuba aliyotoa mwalimu kuhusu kuundwa kwa serikali ya Tanganyika na dhana ya ubaguzi.

Zanzibar imetusaidia sana katika kutuweka pamoja kama jamii moja.

Wanaoipenda Tanganyika na wanaoipenda Tanzania wanataka Kero/kiini macho cha muungano kipatiwe dawa.

Mada ya Mchambuzi https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/334649-tundu-lissu-na-kiini-macho-cha-muungano.html ni ya kuifanyia kazi.

Tutapata athari kubwa mbeleni kwa kuipuuza.
Nonda, Tanganyika ilipata uhuru mwaka 1961 na ikabaki kama taifa hadi 1964, si sahihi kusema ZNZ ndio imeleta gundi la utaifa wetu. phwee!

Umuhumi wa ZNZ katika muungano ni kwa ajili ya usalama wa dunia. Nchi za magharibi zitafanya kila liwezakanalo kuhakikisha kuwa ZNZ inakuwa katika muungano ili kuepusha Mali na Ageria nyingine.

Hakuna mtu au nchi nyingine itakayojisikia salama katika ukanda huu kwa ZNZ kuwa nje ya muungano.
ZNZ ni refractory and volatile land, it's a potential and breeding site .... which may trouble the world.

Huu utaratibu wa kudhani kuwa tunawhitaji ZNZ kufanya kazi huku ndio wameutumia miaka mingi ili kupata mradi wao.
Sisi kama taifa ni lazima ifike mahali tuwe na mipango na malengo yetu siyo kuazima hata wendawazimu ili kuziba ufa tunaoweza kuushugulikia.

Ni aibu kuendelea kulipia watu bili kwasababu zisizokuwepo. Tena niweke wazi, WZNZ ni sehemu ya tatizo.
Wakiondoka nafasi zao zitazibwa vema sana na watanganyika wa kabila na dini zote.

Mfano, Nahodha akiondoka kuna Watangayika kama 100 wenye elimu uwezo na busara zaidi wapo katika foleni.
Sioni kwanini tuwe na waziri kwasababu tu katoka ZNZ! C'ON!

Watanganyika wenye uwezo zaidi ya hao Wazanzibar ni wengi na wanahangaika hakuna sababu ya kuajiri mtu eti kwa jina lake na sio ufahamu.

Nyerere alisema ''kama ZNZ watataka kuondoka katika muungano hatawapiga mabomu''. Alifahamu kuwa Tanganyika haiwezi kuishi kwa kutegemea ZNZ. Tanganyika ilikuwepo kabla ya Sultan hajaondoka.

Tanganyika ilipotaka EA federation haikutaka hivyo kwa kutafuta suluhu. Ilifanya hivyo kama sehemu ya Pana Africanism.
Kwa bahati nzuri Karume aliihitaji na kwabahati nzuri usalama wa Tanganyika ulitegemea sana ZNZ.
Nasema ulitegemea sana ZNZ tofauti na sasa ambapo usalama wa dunia unategemea sana Tanganyika kwa kuiangalia ZNZ

Nonda, dhana ya kuwa Nyerere alikataa G55 kwasababu ya kulinda muungano inatafsiriwa vibaya sana.
Alichokataa Nyerere ni utaratibu wa kuwa na tatizo halafu bunge linajigeuza kuwa wananchi bila wananchii kuulizwa.
Bunge linajigeuza kuwa chama tawala.

Utaratibu alotaka kuutumia Msekwa haukuwa sahihi na kama ungeachwa basi nchi ingemeguka kwa utaratibu wa kundi fulani kuchukua hatua kwa kujifanya ni wananchi.

Nyerere aliwaambia, kama wana hoja kwanza watoke ndani ya chama kwasababu hiyo haikuwa sera ya chama.
Halafu akalaani utaratibu wa kutumia bunge kwa njia za mkato.

Kuhusu serikali 3 unayosema, nakuhakikishia kuwa hilo halitawezekana. Likiwezekana basi ZNZ yenye madaraka kamili haipo. Hakuna uwezekano kwasababu serikali ya tatu itakuwa na madaraka gani?
ZNZ inahitaji sana ulinzi na usalama, huoni hapo kuna kufunikwa.
Hakuna rais asiye miliki vyombo vya dola isipokuwa chini ya mwanvuli.

ZNZ wanataka kupokezana urais, Tanganyika wanasema hell no! ninyi ni nani na kwa uzuri na manufaa gani tuhitaji Rais kutoka ZNZ! . Kwa kiburi na dharau za ZNZ! yaani watu laki 5 maana laki 5 wanaishi kwetu ndio kweli wafikie mahali pa kutuendesha eti wanataka urais wa kupokezana! to hell, kama hamtaki rais wa Tanganyika twendeni EAC.Nani anaihitaji ZNZ! Nonda, ZNZ ya utumwa si ya leo!
Halafu mgombea mwenza itakuwaje!

Huyo rais Ceremonial wa CHadema atakuwa na mamlaka ya kitu gani, kwasababu ZNZ itakuwa na wake kama Tanganyika.
Endapo atakuwa commander in chief basi ZNZ haina chake maana haina jeshi, hakuna mamlaka kamili hakuna ZNZ huru.

Mimi nadhani WZNZ wanatakiwa wafikirie hatima yao sasa maana Tanganyika ikirudi hakuna uchochoro.
Mznz akikubali passport ya kijani hapo haijambo lakini atapoteza mamlaka kamili.
Akikataa basi huyo ni jirani kama Rwanda na Burundi au Malawi kwahiyo awapo Tanganyika ni mgeni tu!

Nonda, leo hii Mzanzibar hana pua ya kunyanyua mbele ya Tanganyika! ni ima akubali kivuli au aanze mbele kwa maumivu.Who cares! ZNZ?!
Zile kelele za miaka ya nyuma kwisha, sasa ni adabu mbele!
 
Nguruvi3

CHADEMA; CUF wanataka serikali tatu.
Mjadala wa kupokezana urais wa serikali ya Muungano umeshika kasi.

Kuna watoa maoni huku Tanganyika pia wanadai serikali ya Tanganyika irudi.

Tusisahau juhudi za G55 na Rev. Mtikila.

Ni wazi, Tanganyika inarudi sio kwa sababu ya matwakwa ya Wazanzibari lakini ni kwa sababu tupo watanganyika ambao tunaelewa Muungano kama ulivyo leo ni "kiini macho".

Linapokuja suala la muungano ni wazi kuwa wabia huwa wanahitajiana/ huwa kuna masilahi fulani kwa kila upande unaojiunga katika Muungano. Kama Tanganyika iliona ni jambo jema kuingia katika muungano na Zanzibar 1964 basi kutokana na utete wa siasa ulivyo huku "Tanzania bara" siku Zanzibar ikitoka Muungano ndio tutaelewa umuhimu wake.

Kufikiria kuwa Tanganyika haihitaji Zanzibar, basi Mwalimu Nyerere angeruhusu G55 ilete serikali ya Tanganyika.

Hata wewe unaelewa vipi Zanzibar imesaidia kuifanya Tanganyika isimeguke. Kama hili hulielewi naomba ufanye utafiti. Au soma kwa makini au sikiliza kwa makini hotuba aliyotoa mwalimu kuhusu kuundwa kwa serikali ya Tanganyika na dhana ya ubaguzi.

Zanzibar imetusaidia sana katika kutuweka pamoja kama jamii moja.

Wanaoipenda Tanganyika na wanaoipenda Tanzania wanataka Kero/kiini macho cha muungano kipatiwe dawa.

Mada ya Mchambuzi https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/334649-tundu-lissu-na-kiini-macho-cha-muungano.html ni ya kuifanyia kazi.

Tutapata athari kubwa mbeleni kwa kuipuuza.

Bwana Nondo, Mungu akubariki na ukuzidishie ujasiri wa kusema ukweli japokua wengi hapa unawakera....
 
Hivi nchi ya Tanzania Bara ndo nchi gani maana hata kabla ya muungano na Zanzibar kulikuwa na Tanganyika na hata Nyerere hakuwa Rais wa Tanganyika....sasa kila uchao nasikia Tanzania Bara na Zannzibar...tusipotoshe Historia na Ujinga wa maslahi ya wanasiasa wajinga wenye kuibua upuuzi kwa manufaa ya watu wachache wale washibe kwa siasa za Kinafiki...I will stand with anyone who will fight for the renewal of my historical nation that even Mkwawa died for "TANGANYIKA"
 
kama zanzibar inataka urais wa zamu ifute dola ya zanzibar. mbona muna serikali yenu zanzibar. usawa kwanza katiba itoa serikali tatu. hapo tutawaunga mkono hata mkishika serikali ya muungano awamu kumi. kwasasa munataka kutawala hata mambo yasiyo ya muungano kama elimu ya msingi afya, maji n.k. au vunjeni dola yenu kwanza ili tuwe na serikali moja. zanzibar itakuwa mkoa wa visiwani.
 
mimi natamani wazanzibar watawale tanganyika kwa kwa awamu ishirini. ila sisi tupewe tanganyika yetu kwanza. tena hatutataka kutawala muungano. au wazanzibar wavunje serikali yao ya mapinduzi ili tuwe na dola moja ya jamhuri ingawa wazanzibar bado wanajivunia uzanzibar bado. kila kukicha hata bungeni nikupigani zanzibar kana kwamba wanatawaliwa na wakoloni wakati wanafaidika zaidi ya watanganyika(wabara)
 
Nyerere ambaye ni baba wa Taifa alishasema hatutomchagua rais sababu ya dini,rangi,kabila,u tanganyika au u zanzbar. Tutamchagua kutikana na uwezo wake wa kuongoza Taifa la Tanzania. Mkitaka hayo basi Zanzbar nako kuwe na u rais wa kupokezana ili Zito,Nape,Mtatiro,Mnyika nk siku moja nao wawe marais wa Zanzbar!
 
Tunataka Serkali Moja Tu!

Inakuja serikali ya Afrika Mashariki. Jitayarishe/jipange vizuri tu. Rais wa serikali hiyo atakuwa Kagame au Museveni na makamu wa Rais atatoka Kenya.

Mchakato wa Kuiunganisha Afrika Mashariki (uk. 90-92)

d. Shirikisho la kisiasa lenye urais wa mzunguko ifi kapo 2010 na uchaguzi wa rais ifi kapo 2013

Waafrika Mashariki walikubaliana kwa kauli moja juu ya shirikisho la kisiasa.

Jisomee hapa http://www.kituochakatiba.org/index2.php?option=com_docman&task=doc_view&gid=1208&Itemid=27
 
Hivi Dola ya Tanzania ina mtazamaji katika Bunge dogo la visiwa vyake vya Zanzibar?
 
Yombayomba

Muabudu Nyerere...Umepotea.

Mtoto wa mtumwa mtumwa tu hata mawazo yake ya kitumwa. Mwenzetu unamwabudu mwenye masaburi laini (Sheikh Faridi) na bwana Jusa siyo au na yule fulani? ha ha ha ha
 
ccm-kampeni-uzini-3-564x376.jpg


NAIBU KATIBU MKUU WA CCM ZANZIBAR VUAI ALI VUAI


Written by Harith - 12/01/2013



CHAMA CHA MAPINDUZI ZANZIBAR KIMEPENDEKEZA SUALA LA MGOMBEA WA NAFASI YA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWA TIKETI YA CHAMA HICHO KUWA YA KUPOKEZANA KATI YA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR.

HAYO YAMEELEZWA NA NAIBU KATIBU MKUU WA CCM ZANZIBAR VUAI ALI VUAI KWA MNASABA WA MAADHIMISHO YA MIAKA 49 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR AMBAYP KILELE CHAKE KIMEFIKIA LEO KATIKA UWANJA WA AMANI MJINI ZANZIBAR.

AIDHA KIONGOZI HUYO AMEONGEZA KUWA SUALA LA KUCHAGULIWA MWANASIASA KUTOKA ZANZIBAR KUPITIA MKUTANO MKUU WA CCM DODOMA ATAKAYEPEPERUSHA BENDERA YA CCM KATIKA UCHAGUZI WA RAIS WA ZANZIBAR LINAPASWA KUANGALIWA UPYA ILI WAZANZIBARI WAPENDEKEZE JINA LA MGOMBEA WAO WA URAIS WA ZANZIBAR WENYEWE.

MATAMSHI HAYO YA NAIBU KATIBU MKUU WA CCM (ZANZIBAR) YANAWEZA KUZUSHA MPASUKO NDANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI KUTOKANA NA KUANZA KAMPENI NA HARAKATI ZA CHINI KWA CHINI ZA BAADHI YA VIGOGO WA CHAMA HICHO UPANDE WA TANZANIA BARA ZAKUTAKA KUWANIA URAIS KATIKA UCHAGUZI MKUU UJAO WA MWAKA 2015.
Hivi hii ni makusudi au kutokujua hebu soma hii '' MGOMBEA WA NAFASI YA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWA TIKETI YA CHAMA HICHO KUWA YA KUPOKEZANA KATI YA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR''. hiyo Tanzania bara ni ipi?!! upotoshaji wa makusudi kabisaa huu. Tanzania ni jina lililopatikana baada ya kuunga majina Mawili ya Tanganyika na Zanzibar. So unapotaja Tanzania bara na Zanzibar unapotosha. Huu muungano unaelekea ulikuwa na Malengo ya kuisaidia Zanzibar tuu ndio maana Zanzibar imeendelea ku-maintain its own Identity na Mzanzibar ana uhuru wa kuingia na kuisha sehemu yoyote ya Tanzania ila Mtanganyika hana uhuru kama huo katika ardhi ya Zanzibar. Hilo pendekezo la urais wa kupokezana vijiti nashindwa kuelewa hivi ukiwa mzanzibar huna uwezo wa kugombea urais Tanzania na ukashinda bila ya kubebwa?. Hiyo mambo hifai kabisa hasa katika enzi hizi za siasa za ushindani.

Nashindwa kuelewa hii hesabu. Ninavyoelewa mimi ili Rais ajaye atoke Zanzibar ina Maana moja vyama vyote lazima visimamishe mgombea uraisi Muungano ambaye ni Mzanzibar. Hii nayo itakuwa kali ya mwaka
 
Nonda, Tanganyika ilipata uhuru mwaka 1961 na ikabaki kama taifa hadi 1964, si sahihi kusema ZNZ ndio imeleta gundi la utaifa wetu. phwee!
Katika maandishi yangu nilisema Zanzibar ilisaidia nchi yetu isimeguke.Wewe umetumia msemo wa "ZNZ imeleta gundi"
Katika uzi huu (link)unazungumzia nini? Gundi? au urithi?
link https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...a-tanganyika-na-zanzibar-131.html#post5562551

Wapo wengine wanaoongelea kuhusu gundi link muunganowatanzania
pia link http://hakiforums.boardhost.com/viewtopic.php?id=433
Mkuu Nguruvi3
Tanganyika tuna tatizo/matatizo (changamoto nyingi). "Phwee!" au "kutokua na pua" hakutatatua matatizo yetu. Kikwete husema "ni upepo utapita" anafikiria matatizo hujitatua na hayahitaji kutatuliwa. Bila kutatua matatizo, matatizo hayo huzidi kukua na kufikia kuwa ni bomu linalosubiri kuripuka.
Umuhumi wa ZNZ katika muungano ni kwa ajili ya usalama wa dunia. Nchi za magharibi zitafanya kila liwezakanalo kuhakikisha kuwa ZNZ inakuwa katika muungano ili kuepusha Mali na Ageria nyingine.
Vipi Zanzibar ilitishia/inatishia usalama wa dunia?
Hakuna mtu au nchi nyingine itakayojisikia salama katika ukanda huu kwa ZNZ kuwa nje ya muungano.
ZNZ ni refractory and volatile land, it's a potential and breeding site .... which may trouble the world.
Je Zanzibar kama dola/serikali imeshawahi kupigana vita na nchi zilizo jirani? Auvipi ZNZ imetishia usalama wa nchi nyingine? Vipi ZNZ ilitishia/inatishia usalama wa Tanganyika?
Kuhusu serikali 3 unayosema, nakuhakikishia kuwa hilo halitawezekana. Likiwezekana basi ZNZ yenye madaraka kamili haipo. Hakuna uwezekano kwasababu serikali ya tatu itakuwa na madaraka gani?
Angalia video katika link hii https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ka-na-serikali-ya-tanganyika.html#post5591773
 
Nonda,

..ZNZ haisadii chochote kile ktk kutuweka wa-Tanganyika pamoja.

..wa-TGK tunaingia hasara kubwa sana ktk muungano huu.

..zile bil 32 alizopewa Dr.Bilal kwa ajili ya maendeleo ya ZNZ zingetumika kwa maendeleo ya Mtwara na Lindi zingetuepusha na vurugu zilizotokea ktk mikoa hiyo.

..kwa maoni yangu ZNZ ni tishio la usalama na uhai wa Tanganyika kwasababu tunawahudumia wa-Zanzibar at the expense ya wa-Tanganyika na matokeo yake kuna maeneo ya nchi hii yanajiona kama yametengwa. hali hiyo imeanza kuzua hasira na machafuko.

..naendelea kusisitiza kwamba tunataka TGK huru, na ZNZ huru, zinazoshirikiana kupitia EAST AFRICAN COMMUNITY.

cc: Nguruvi3.
 
Last edited by a moderator:
Imewekwa na hamed Mazrouy
Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa Cuf Juma Duni Haji akizungumza katika mkutano wa Hadhara wa Chama hicho.

Chama cha Wananchi CUF kupitia Mkurugenzi wake wa Habari Uwenezi na Mawasiliano ya Umma Mh:Salim Biman kimewataka wanachama wa chama hicho pamoja na wazanzibar wapenda maendele pamoja na Nchi yao kuwa watulivu pamoja na Mshikamano wa kuwa kitu kimoja sambamba na kuacha tofauti ya vyama vyao badala yake waangalie maslahi ya nchi yao kwanza kitu ambacho kitaikomboa Zanziba na kuwa na Mamlaka kamili.
Kauli hio ya Mh:Biman ametolewa leo katika Mkutano wa hadhara wa Chama hicho uliofanyika katika kiwanja cha Komba wapya ndani ya wilaya ya mjini Unguja na kuhudhuriwa na viongozi kadhaa wa juu ndani ya chama hicho pamoja na Wananchi mbali mbali waliokuwa wengi sana.
Nae mjumbe wa Baraza kuu Taifa CUF Mh:Ismail Jussa ambae pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe amesema kuwa anashangazwa na baadhi ya watu wanaotamka hadharani kuwa wao wanao mkata halisi wa Muungano wa mwaka 1964 uliosisiwa rasmI na Mzee Karume pamoja na Nyerere .
Amesema kuwa kama kuna Mtu yoyote yule ambae ana hati halisi ya Muungano japo kopi basi aioneshe hadharani ili iweze kuwatoa wasiwasi ambao kwa sasa umewajaa wazanzibar waliowengi sana kutokana na kudhulumiwa na Muungano huu uliopo hivi sasa ambao umeikandamiza Zanzibar kwa nyanja zote za kiuchumi.
Amefahamisha kuwa hapo miaka ya nyuma walijitokeza kundi la watu na kufungua kesi mahakamani ya kudai hati halisi ya muungano huu na Mahakama kukiri kuwa imeshindwa kuwa na hati halisi ya Muungano wala kopo yake ,lakini watu hao hawakuridhika ndipo walipoandikia barua UN kuwataka watoe uthibitisho wa kuwepo kwa muungano huu lakini na wao pia walijibu kuwa hawakuwa na uthibitisho wowote kuhusiana na muungano uliopo baina ya Zanzibar na Tanganyika hivo basi yanini kuendelea kuwepo kwa Muungano huu usiokuwa na uthibitisho wowote hule.
Nae Mjumbe wa Baraza kuu Taifa CUF ambae pia ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii MH:Juma Duni Haji amesema kuwa anashangazwa sana kuwaona Wazanzibar wachache wakitaka kuwepo kwa Muungano huu wakati Watanganyika wenyewe kwa sasa wanataka Zanzibar iwe na mamlaka kamili kitaifa na kimataifa iweje sisi wenyewe tusiungane na kuwa kitu kimoja kuitetea Nchi yetu.
Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe Ismail Jussa akihutubia katika mkutano wa hadhara

Pia amefahamisha kuwa katika kipindi cha nyuma ilikuwa hakuna mzanzibar yoyote yule ambae aliweza hata kusubutu kuzungumzia kuhusu suala la Muungano lakini kwa sasa hali nikinyume na kila mtu anaweza kusema analolitaka kuhusu Muungano huu dhalim Kwa Zanzibar na ndio maana tunasema hadharani kuwa Muunagano huu hautufai.
Kuhusu suala la katiba ya Tanzania amesemea kuwa katiba hio haiwahusu Wazanzibar kwani katiba hio uhalisia wake ni katiba ya Tanganyika hivo basi sisi Wazanzibar tuna katiba yetu iweje tuifate katiba ya kwao wakati ina katiba yake halisi.
Akizungumzia kuhusu suala la uendeshwaji wa Nchi hii ndani ya miaka mingi iliopita huko nyuma amesema kuwa nchi hii ilikuwa haiendeshwi kikatiba badala yake ilikuwa ikiendeshwa na Kanuni za Mwalimu Nyerere kwani alikuwa akiamua analolitaka yeye tu na sio kufuata katiba ambayo ndio ilitakiwa ifuatwe kama ilivosheria ya Nchi kuwa ni lazima katiba ndio iwe muongozo ndani ya nchi hayo yamethibitishwa na hata aliekuwa Spika mstaafu wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano Pius Msekwa.
Amefahamisha kuwa lilipokuja suala la kuanzisha Benk kuu ya Tanzania (BOT) Tanganyika walikwenda kudai pesa za kufungulia benk kwenye Umoja wa Afrika Mashariki ambapo wahusika walikataa kuzitoa kutokana na kuwepo kwa majina ya Nchi mbili tofauti nazo ni Zanzibar na Tanganyika hivo basi kulipaswa kuwe na makubaliano kabla kati ya pande hizo mbili ndio wao waweze kuzitoa pesa hizo.
Kutokana na masharti hayo waliopewa ndipo Tanganyika wakatumia ujanja wao wa kuingiza suala la Sarafu kuwa mambo ya Muungano kwa lengo la kuzichukua pesa za Zanzibar ili waweze kuongezea na kufungua Benk kuu ambapo uanzishwaji wa Benk hio Zanzibar ilikuwa na kiasi ya asilimia 11.2 leo hii tunaambiwa Zanzibar haihusikia na haina shea ndani ya benk hio.
Aidha Mh😀uni amesema kuwa Nyerere alikuwa akikiogopa sana chama kilichokuwepo Zanzibar (ASP) na ndio maana akakiingigiza chama cha Tanu kuwa ndio chama ambacho kitaendesha Serikali na ikapitishwa sheria bila ya Wazanzibar wenyewe kujua kuwa chama cha Tanu ndicho kinachoongoza Serikali ya Muungano.
Sambamba na hayo amesema kuwa wananchokifanya CUF sasa sio kuvunja Muungano bali ni kudai haki yao ya msingi kisheria kwani kama ni kuvunja muungano tayari ulishavunjwa na Nyerere tokea zamani na sasa wanachokifanya wao ni kudai Nchi yao tu sio kama wanavosema baadhi ya watu kuwa wanantaka kuuvunja Muungano.
Aliendelea kwa kusema ikiwa Nyerere ametufikisha hapa tulipo sasa Wazanzibar nataka niwaulize ninani mnadhani atakae kaa Rais Tanganyika na kutujali Wazanzibar kama sio sisi wenyewe kudai Nchi yetu na muda wenyewe wakudai ndio huu tulionao sasa.
Amebainisha kuwa katika chaguzi mkuu unaokuja inshallah tukiwa hai basi hatuwezi kwenda na mfumo huu uliopo sasa wa katiba isipokuwa tutakwenda tukiwa ndani ya Mkataba kwani ndio suluhishi pekee lililobaki kwa nchi yetu​
Jamani hivi hawa wenzetu wazanzibar wana akili za kutosha kweli.
Nasema hivi kwasababu ukisoma maneno ya viongozi wao utashangaa kama hawa ni viongozi wananchi wakoje.

Akina duni wanasema kuwa Nyerere aliweka sarafu moja ili kutaifisha pesa za Zanzibar.
Katika madai ya wazanzibar hata siku moja hawajawahi kudai uwepo wa safaru yao. Na wakidai nani atawazuia?

Wanadai katiba ya muungano ni ya Tanganyika. Stupd! Jusa alishawahi kuapa kuilinda, Duni alishawahi kuapa kuilinda, Maalim Seif alishawahi kuitumia katiba hiyo leo wanasema ni ya Tanganyika.

Stupid! kwasababu wabunge wa ZNZ ndani ya bunge la JMT hawajawahi kuzuiliwa kuja. Hawajawahi kumuita makamu wa Rais aliyechaguliwa kwa uzanzibar, kuna wafanyakazi wa muungano waliopata ajira si kwa sifa za elim bali uzanzibar wao, halafu leo hawa vihio wanasema hawaitambui katiba!

Nahodha, Nasor Moyo, Natepe, Mapuri, Salim Ahmed, na wengine wamewahi kuapa kuilinda katiba hiyo, leo genge la waarabu linataka kuuaminisha umma kuwa hilo halikutokea! hivi mtu akisema hawa jamaa ni nincompoop atakuwa amewatusi kweli.

Pili, wanasema shea 11.2% ndani ya BoT wanaambiwa hawana. Huu kama si ujinga ni wehu.
Kila mwezi wanapokea 7% ya pato la taifa ambalo ni kubwa mara 10 kuliko pato la Zanzibar kwa mwezi.
Bila pesa hiyo SMZ haiwezi kujiendesha. Itajiendesha vipi kwa uchumi wa mapato ya bilioni 120 kwa mwaka?

Halafu hawaambii watu wao kuwa mishahara yao ikiwa ni pamoja na ya Seif Hamad na matibabu yake India hawajui pesa zinatoka wapi. Kwa uchumi wa ZNZ kwenda kumtibu Seif ni pengo kubwa sana. Jamani uchumi wa ZNZ ni mdogo kuliko uchumi wa Manispaa ya Ilala na mdogo kuliko wa soko la kariakoo, ni mwehu gani atakayekwenda kuiiba nchi fukara kama hiyo?

Duni na Jusa hawawaelezi watu wao kuwa ulinzi na usalama haujawahi kuwa katika bajeti ya ZNZ kwa miaka 48.
Bajeti ya ulinzi tu ilkichukua bilioni 25 ni robo ya pato la ZNZ.

Duni na Jusa waelezeni watu wenu kuwa ule umeme wa vipaza sauti na wa kuchezea bao usiku wenzetu hawajui bei yao.

Duni na Jusa waelezeni wazanzibar kuwa ninyi mumesoma bila senti kutoka Zanzibar na sasa kuna division hakuna nao pia wanafaidi kama ninyi, sasa mnacholalamika kuonewa ni kipi? Kubebwa hamtaki kuteremeka mgongoni hamtaki.

Soma hiyo makala wao wanasema hawataki muungano, kwa unafiki wa kizanzibar wanataka mkataba.
Zanzibar! if you wanna stay with us you must be on your knee! period.

Kuna mambo mawili tu
Kuweni huru tukutane EAC
Msitiri dhiki na shida zenu mkae chini ya kivuli cha Tanganyika.

Hakuna short cut

We're extremely tired living with these creatures!

cc Jokakuu, Jasusi, mwanakijiji, Nonda, Takashi na wengine
 
Mtoto wa mtumwa mtumwa tu hata mawazo yake ya kitumwa. Mwenzetu unamwabudu mwenye masaburi laini (Sheikh Faridi) na bwana Jusa siyo au na yule fulani? ha ha ha ha

Mpelekeeni salamu Bwana Mungu wenu (Nyerere) kama wazanzibari wamebadilika siyo wale aliyowaache yeye .Zanzibar kwanza , Muungano baadae.
 
Jamani hivi hawa wenzetu wazanzibar wana akili za kutosha kweli.
Nasema hivi kwasababu ukisoma maneno ya viongozi wao utashangaa kama hawa ni viongozi wananchi wakoje.

Akina duni wanasema kuwa Nyerere aliweka sarafu moja ili kutaifisha pesa za Zanzibar.
Katika madai ya wazanzibar hata siku moja hawajawahi kudai uwepo wa safaru yao. Na wakidai nani atawazuia?

Wanadai katiba ya muungano ni ya Tanganyika. Stupd! Jusa alishawahi kuapa kuilinda, Duni alishawahi kuapa kuilinda, Maalim Seif alishawahi kuitumia katiba hiyo leo wanasema ni ya Tanganyika.

Stupid! kwasababu wabunge wa ZNZ ndani ya bunge la JMT hawajawahi kuzuiliwa kuja. Hawajawahi kumuita makamu wa Rais aliyechaguliwa kwa uzanzibar, kuna wafanyakazi wa muungano waliopata ajira si kwa sifa za elim bali uzanzibar wao, halafu leo hawa vihio wanasema hawaitambui katiba!

Nahodha, Nasor Moyo, Natepe, Mapuri, Salim Ahmed, na wengine wamewahi kuapa kuilinda katiba hiyo, leo genge la waarabu linataka kuuaminisha umma kuwa hilo halikutokea! hivi mtu akisema hawa jamaa ni nincompoop atakuwa amewatusi kweli.

Pili, wanasema shea 11.2% ndani ya BoT wanaambiwa hawana. Huu kama si ujinga ni wehu.
Kila mwezi wanapokea 7% ya pato la taifa ambalo ni kubwa mara 10 kuliko pato la Zanzibar kwa mwezi.
Bila pesa hiyo SMZ haiwezi kujiendesha. Itajiendesha vipi kwa uchumi wa mapato ya bilioni 120 kwa mwaka?

Halafu hawaambii watu wao kuwa mishahara yao ikiwa ni pamoja na ya Seif Hamad na matibabu yake India hawajui pesa zinatoka wapi. Kwa uchumi wa ZNZ kwenda kumtibu Seif ni pengo kubwa sana. Jamani uchumi wa ZNZ ni mdogo kuliko uchumi wa Manispaa ya Ilala na mdogo kuliko wa soko la kariakoo, ni mwehu gani atakayekwenda kuiiba nchi fukara kama hiyo?

Duni na Jusa hawawaelezi watu wao kuwa ulinzi na usalama haujawahi kuwa katika bajeti ya ZNZ kwa miaka 48.
Bajeti ya ulinzi tu ilkichukua bilioni 25 ni robo ya pato la ZNZ.

Duni na Jusa waelezeni watu wenu kuwa ule umeme wa vipaza sauti na wa kuchezea bao usiku wenzetu hawajui bei yao.

Duni na Jusa waelezeni wazanzibar kuwa ninyi mumesoma bila senti kutoka Zanzibar na sasa kuna division hakuna nao pia wanafaidi kama ninyi, sasa mnacholalamika kuonewa ni kipi? Kubebwa hamtaki kuteremeka mgongoni hamtaki.

Soma hiyo makala wao wanasema hawataki muungano, kwa unafiki wa kizanzibar wanataka mkataba.
Zanzibar! if you wanna stay with us you must be on your knee! period.

Kuna mambo mawili tu
Kuweni huru tukutane EAC
Msitiri dhiki na shida zenu mkae chini ya kivuli cha Tanganyika.

Hakuna short cut

We're extremely tired living with these creatures!

cc Jokakuu, Jasusi, mwanakijiji, Nonda, Takashi na wengine

Well, so do we... Wala bado mukichoka kweli mtaachia wenyewe na wala muda sio mrefu uliyobakia.
 
Back
Top Bottom