Nguruvi3
CHADEMA; CUF wanataka serikali tatu.
Mjadala wa kupokezana urais wa serikali ya Muungano umeshika kasi.
Kuna watoa maoni huku Tanganyika pia wanadai serikali ya Tanganyika irudi.
Tusisahau juhudi za G55 na Rev. Mtikila.
Ni wazi, Tanganyika inarudi sio kwa sababu ya matwakwa ya Wazanzibari lakini ni kwa sababu tupo watanganyika ambao tunaelewa Muungano kama ulivyo leo ni "kiini macho".
Linapokuja suala la muungano ni wazi kuwa wabia huwa wanahitajiana/ huwa kuna masilahi fulani kwa kila upande unaojiunga katika Muungano. Kama Tanganyika iliona ni jambo jema kuingia katika muungano na Zanzibar 1964 basi kutokana na utete wa siasa ulivyo huku "Tanzania bara" siku Zanzibar ikitoka Muungano ndio tutaelewa umuhimu wake.
Kufikiria kuwa Tanganyika haihitaji Zanzibar, basi Mwalimu Nyerere angeruhusu G55 ilete serikali ya Tanganyika.
Hata wewe unaelewa vipi Zanzibar imesaidia kuifanya Tanganyika isimeguke. Kama hili hulielewi naomba ufanye utafiti. Au soma kwa makini au sikiliza kwa makini hotuba aliyotoa mwalimu kuhusu kuundwa kwa serikali ya Tanganyika na dhana ya ubaguzi.
Zanzibar imetusaidia sana katika kutuweka pamoja kama jamii moja.
Wanaoipenda Tanganyika na wanaoipenda Tanzania wanataka Kero/kiini macho cha muungano kipatiwe dawa.
Mada ya Mchambuzi
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/334649-tundu-lissu-na-kiini-macho-cha-muungano.html ni ya kuifanyia kazi.
Tutapata athari kubwa mbeleni kwa kuipuuza.
Nonda, Tanganyika ilipata uhuru mwaka 1961 na ikabaki kama taifa hadi 1964, si sahihi kusema ZNZ ndio imeleta gundi la utaifa wetu. phwee!
Umuhumi wa ZNZ katika muungano ni kwa ajili ya usalama wa dunia. Nchi za magharibi zitafanya kila liwezakanalo kuhakikisha kuwa ZNZ inakuwa katika muungano ili kuepusha Mali na Ageria nyingine.
Hakuna mtu au nchi nyingine itakayojisikia salama katika ukanda huu kwa ZNZ kuwa nje ya muungano.
ZNZ ni refractory and volatile land, it's a potential and breeding site .... which may trouble the world.
Huu utaratibu wa kudhani kuwa tunawhitaji ZNZ kufanya kazi huku ndio wameutumia miaka mingi ili kupata mradi wao.
Sisi kama taifa ni lazima ifike mahali tuwe na mipango na malengo yetu siyo kuazima hata wendawazimu ili kuziba ufa tunaoweza kuushugulikia.
Ni aibu kuendelea kulipia watu bili kwasababu zisizokuwepo. Tena niweke wazi, WZNZ ni sehemu ya tatizo.
Wakiondoka nafasi zao zitazibwa vema sana na watanganyika wa kabila na dini zote.
Mfano, Nahodha akiondoka kuna Watangayika kama 100 wenye elimu uwezo na busara zaidi wapo katika foleni.
Sioni kwanini tuwe na waziri kwasababu tu katoka ZNZ! C'ON!
Watanganyika wenye uwezo zaidi ya hao Wazanzibar ni wengi na wanahangaika hakuna sababu ya kuajiri mtu eti kwa jina lake na sio ufahamu.
Nyerere alisema ''kama ZNZ watataka kuondoka katika muungano hatawapiga mabomu''. Alifahamu kuwa Tanganyika haiwezi kuishi kwa kutegemea ZNZ. Tanganyika ilikuwepo kabla ya Sultan hajaondoka.
Tanganyika ilipotaka EA federation haikutaka hivyo kwa kutafuta suluhu. Ilifanya hivyo kama sehemu ya Pana Africanism.
Kwa bahati nzuri Karume aliihitaji na kwabahati nzuri usalama wa Tanganyika ulitegemea sana ZNZ.
Nasema ulitegemea sana ZNZ tofauti na sasa ambapo usalama wa dunia unategemea sana Tanganyika kwa kuiangalia ZNZ
Nonda, dhana ya kuwa Nyerere alikataa G55 kwasababu ya kulinda muungano inatafsiriwa vibaya sana.
Alichokataa Nyerere ni utaratibu wa kuwa na tatizo halafu bunge linajigeuza kuwa wananchi bila wananchii kuulizwa.
Bunge linajigeuza kuwa chama tawala.
Utaratibu alotaka kuutumia Msekwa haukuwa sahihi na kama ungeachwa basi nchi ingemeguka kwa utaratibu wa kundi fulani kuchukua hatua kwa kujifanya ni wananchi.
Nyerere aliwaambia, kama wana hoja kwanza watoke ndani ya chama kwasababu hiyo haikuwa sera ya chama.
Halafu akalaani utaratibu wa kutumia bunge kwa njia za mkato.
Kuhusu serikali 3 unayosema, nakuhakikishia kuwa hilo halitawezekana. Likiwezekana basi ZNZ yenye madaraka kamili haipo. Hakuna uwezekano kwasababu serikali ya tatu itakuwa na madaraka gani?
ZNZ inahitaji sana ulinzi na usalama, huoni hapo kuna kufunikwa.
Hakuna rais asiye miliki vyombo vya dola isipokuwa chini ya mwanvuli.
ZNZ wanataka kupokezana urais, Tanganyika wanasema hell no! ninyi ni nani na kwa uzuri na manufaa gani tuhitaji Rais kutoka ZNZ! . Kwa kiburi na dharau za ZNZ! yaani watu laki 5 maana laki 5 wanaishi kwetu ndio kweli wafikie mahali pa kutuendesha eti wanataka urais wa kupokezana! to hell, kama hamtaki rais wa Tanganyika twendeni EAC.Nani anaihitaji ZNZ! Nonda, ZNZ ya utumwa si ya leo!
Halafu mgombea mwenza itakuwaje!
Huyo rais Ceremonial wa CHadema atakuwa na mamlaka ya kitu gani, kwasababu ZNZ itakuwa na wake kama Tanganyika.
Endapo atakuwa commander in chief basi ZNZ haina chake maana haina jeshi, hakuna mamlaka kamili hakuna ZNZ huru.
Mimi nadhani WZNZ wanatakiwa wafikirie hatima yao sasa maana Tanganyika ikirudi hakuna uchochoro.
Mznz akikubali passport ya kijani hapo haijambo lakini atapoteza mamlaka kamili.
Akikataa basi huyo ni jirani kama Rwanda na Burundi au Malawi kwahiyo awapo Tanganyika ni mgeni tu!
Nonda, leo hii Mzanzibar hana pua ya kunyanyua mbele ya Tanganyika! ni ima akubali kivuli au aanze mbele kwa maumivu.Who cares! ZNZ?!
Zile kelele za miaka ya nyuma kwisha, sasa ni adabu mbele!