CCM Zanzibar yataka urais wa Muungano ugombewe kwa zamu kati ya Tanganyika na Zanzibar

CCM Zanzibar yataka urais wa Muungano ugombewe kwa zamu kati ya Tanganyika na Zanzibar

Hili halitotokea; kanuni ya sasa iko very simple - Rais na Makamu wake hawawezi kutoka upande mmoja wa Muungano. Lakini ingepaswa kuwa Rais na makamo wake wasitoke mkoa mmoja!

Serikali moja? Hapana mkuu, tuuvunje tu muungano tugawane fito na mabati kila mmoja ajijue
 
Huwezi kuwa ceremonial president halafu uwe commander in chief. Nchini Israel commander in chief ni prime minister.
Halafu tutambue kwamba Zanzibar hawana jeshi. Lazima wajue hilo. Wataongozaje jeshi la nchi nyingine? Chadema katika hili naomba mjipange upya.
Umemaliza kila kitu, lakini pia umezidi ''kukoroga'' hii Chadema proposal
1. Mgombea binafsi itakuwaje?
2. ZNZ wanataka tushirikiane na Jeshi, nani commander in chief, yule executive wa Tanganyika yenye jeshi au executive wa ZNZ aliyeazima jeshi au Ceremonial Prez

Ceremonial prez hana mamlaka ya jambo lolote lile, yupo tu kuandaa dhifa za kitaifa tena si msemaji bali kukirimu wageni wasiborege. Leo CDM wanatuambia ndiye commander in chief!!!

Kwa hili la muungano Chadema hawana hoja! absolutely nothing.
Naifikiria picha ya siku walipokwenda kutoa maoni na matokeo ya maoni hayo! dissapointed!

CC
Kitila Mkumbo
Dr Slaa
Zito
J.J.Mnyika
Lissu Tundu
 
Pendekezo la kupokezana urais simply halina mantiki. Tukichukulia suala la uwiano tu basi Zanzibar tayari imeshapata nafasi nyingi za ama urais au umakamu tangu muungano na hakuna maeneo mengine ya Tanzania ambayo yamepata nafasi hiyo. Tukikubali na kama ilivyo sasa kuwa lazima makamu atoke upande mwingine wa Muungano basi Zanzibar inapendelewa kupita kiasi.

Kwanini tusiseme tu kama ilivyo Marekani kuwa Rais na Makamu wasitoke Mkoa mmoja - haijalishi kama mkoa huo uko bara au visiwani?

Mzee Mwanakijiji

Hapa ndio unafanya upotoshaji wa makusudi, tena mara nyingi.

Kauli ya ndugu yako,Nguruvi3 kuwa Zanzibar ni kisehemu tu kama Mafia au Ukerewe

Na kauli kama hii yako kuwa Zanzibar imepata urais au umakamu wa rais na hakuna maeneno mengine ya Tanzania ambayo yamepata nafasi hiyo.

Kauli yako ni tata na wakati huo huo inafafanua utata huo.

Je Zanzibar ni sehemu kama sehemu/eneo jengine la Tanzania?

Kwamba Zanzibar imepata urais na umakamu wa rais wa muungano, kama Zanzibar ni eneo tu kama eneo jengine la Tanzania ni kwa nini wamepata hizo nafasi?

Je kuna eneo jengine zaidi ya Zanzibar ambalo liliingia mkataba na Tanganyika kuunda Muungano wa mambo ya muungano 11?

Mkuu unawalisha dhana potofu wafuasi wako hapa JF.

Hili hutaki kuliweka wazi kuwa Zanzibar na Tanganyika walitia saini mkataba wa kuunganisha mambo 11 tu.

Hata jina la muungano huo uliitwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Kilichoendelea baada ya uwekaji wa saini mkataba huo ni "kiini macho cha Muungano"

Kwa mfano, yamebakia mambo yasio ya muungano ya Tanganyika , lakini usanii unasema, mambo yasiyo ya muungano ya Tanzania bara.

Jina Tanganyika limepotea na Tanzania bara au bara ndio usanii uliozoeleka.

Tanganyika haisemwi kuwa ni sehemu ya Tanzania lakini tumezoea kusikia kuwa Zanzibar ni eneo/sehemu ya Tanzania.

Lakini usanii wa juzi ni huu wa Pinda kwenda Zanzibar si nchi kuzungumza na serikali ya huko juu ya changamoto/kero za muungano. Hatusikii Pinda kwenda Mafia au Mtwara kuzungumzia kero au changamoto za muungano.

Je Zanzibar ni eneo la Tanzania kama eneo lingine lolote. Je Tanganyika ni eneo kama eneo lingine lolote la Tanzania?

Kuna tofauti yoyote kati ya Arusha na Tanzania bara(Tanganyika)?

Je Arusha ni eneo la Tanzania kama lilivyo eneo la Tanganyika katika Tanzania?

Je kuna tofauti yoyote kati ya Tanzania bara(Tanganyika) na Zanzibar?

Tuache kuwadanganya wadanganyika wenzetu, tuwaelezee kiini cha matatizo ya muungano.

Link https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/334649-tundu-lissu-na-kiini-macho-cha-muungano.html

Maeneo ya Tanzania katika lugha ya Muungano ni mawili tu, Tanganyika(wewe unapendelea jina la kisanii Tanzania bara) na Zanzibar.
 
Juzi kushinda jana maalim Seif kasema anataka mkataba hasa wa ulinzi. Sefi kasema koti likikuna na ubadilisha ''size'' hakusema unalivua.
Oktoba 6 2012, Nasor Moyo, Jusa, Himidi wamesema kuwa wanataka muungano kwa sababu za kijiografia, usalama na ulinzi.

Katika makundi yaliyotoa maoni ZNZ hakuna hata moja lililosema sasa basi, kila kundi ikiwemo CUF na UAMSHO wamesema wanataka muungano lakini....

Mkuu Takashi, mimi ni mwananchi tu wa kawaida kama alivyo mwingine hapa JF. Kabla hujahoji uwezo wangu, ningekushauri uhoji uwezo wa makamu wa rais wa nchi yako anayedai tatizo la muungano ni ajira za ubalozi.
Ningekushauri uhoji uwezo wa Profesa wako asiyejua katiba ya ZNZ na asemaye ni nchi ya kiislam.

Tuliza moyo na ghadhabu kwanza ili uweze kupambana na hoja. Nimeweka mahesabu hapo ni wajibu wako useme hapa ndio hapa sivyo. Matusi ni mzalendo.net hapa ni kisima cha fikra na ustaarabu. Mtihani wa matusi tulishafeli wengine.

Naweka hoja hapa tena.
Bajeti ya ZNZ ni bilioni 630. Mapato kwa mwezi ni bilioni 10, kwa mwaka ni bilioni 120.
Tofauti ya bilioni 510 inapatikana kutoka wapi?

Si kweli kuwa ving'ora vya Seif ni kutoka bara, maana Seif katika historia yake ya utumishi wa umma hajawahi kukaa katika meza hata siku moja kuandika au kujadili bajeti ya ulinzi na usalama.

Bajeti ya ulinzi na usalama ikiwa ni pamoja na ile ya mambo ya ndani ni zaidi ya trilioni 1, ikiwa ni mara 10 ya mapato ya ZNZ na mara mbili ya ''bajeti '' ya ZNZ. Uongo uko wapi hapo?

Je, si kweli kuwa WZNZ hawajui bei ya umeme kuanzia mkunazini hadi kiembe samaki, bwejuu hadi kwa mtipura, kisiwandui hadi kibanda maiti, mji mkongwe hadi mfereji maringo.
Je, ni uongo huo?

Je, si kweli kuwa ZNZ inapata mgao wake kutoka JMT pamoja na mishahara bure? Uongo uko wapi
Je, si kweli kuwa ada za mashirika ya SMZ nje ya nchi zinalipwa na JMT na siyo SMZ? uongo uko wapi?

Je, si kweli kuwa kuna watoto wa ZNZ wanaopata nafasi za upendeleo bila ushindani katika vyuo vya bara hata kama i kiwango duni? uongo uko wapi.

Je, si kweli kuwa Tanganyika imebeba WZN wengi kuliko taifa lolote dunia katika historia ya ulimwengu? Nimekosea wapi

Je, si kweli kuwa wanaotaka mkataba wa uswiss, Hong Kong, Ujerumani na Zimbwabwe ni WZNZ? wapi nimekosea

Je,si kweli kweli kuwa bajeti ya elimu ya juu, Seif na wasomi wa ZNZ hawajawahi kukaa kitako na kuiandika achilia mbali kuisoma? Wapi uongo

Zanzibar huru haitapatikana kama kuna kishikizo''attachment'' na Tanganyika.
Huo ni ukweli mchungu sana kwasababu utakuaje huru huku mlinzi anayekulinda hujui analipwa na nani?

Zanzibar huru haitapatika endapo inategemea watoto wasomeshwe na jirani kwa hisani.

Zanzibar huru haitapatikana kwa vile kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni inategemea uwepo wa Tanganyika.

Zanzibar huru ITAPATIKANA pale tu ZNZ itakapokutana na Tanganyika FIFA, AU, SADC au EAC.

Znz huru itapatikana pale itakapokuwa na bendera New York, kama ni ile nyeusi, bluu, kijani na njano hakuna ZNZ huru

ZNZ huru itapatikana kukiwa na HATI NYINGINE na si kupitia passport ya kijani.

Ndio maana tunasema, uwepo mkataba, serikali 3, tano n.k. mazingira ya kidunia yanalazimisha ZNZ ibaki katika kivuli mwanana cha Tanganyika, kwa hiari kwa lazima hiyo ndio natural justice isemavyo, si mimi.

Badala ya kutafuta kiambaza na uchochoro wa kusitiri shida zenu, kuna mambo mawili tu mbele yenu
1. Let ZNZ GO! tukutane FIFA, EAC n.k.
2. ZNZ ijishikize Tanganyika ikiwa ime surrender uhuru kamili. Itulie katika kivuli cha Tanganyika njema apendaye aje!

Let ZNZ go!!! hamna jıpya hapa bado nyimbo ni zile zile... Tunataka kuona Tanganyika inarudi na sio usanii wa kubadilisha maneno.
 
Pendekezo la kupokezana urais simply halina mantiki. Tukichukulia suala la uwiano tu basi Zanzibar tayari imeshapata nafasi nyingi za ama urais au umakamu tangu muungano na hakuna maeneo mengine ya Tanzania ambayo yamepata nafasi hiyo. Tukikubali na kama ilivyo sasa kuwa lazima makamu atoke upande mwingine wa Muungano basi Zanzibar inapendelewa kupita kiasi.

Kwanini tusiseme tu kama ilivyo Marekani kuwa Rais na Makamu wasitoke Mkoa mmoja - haijalishi kama mkoa huo uko bara au visiwani?
Kupokezana urais wa Tanzania utakuwa na maana kama vilevile urais wa Zanzibar ungeweza kupokezana na waTanganyika.
Hii itaboresha sana muungano na kama haliwezekani wazanzibari milioni moja waridhike tu kujitwala wao wenyewe na udogo wao.

Tumewabena vya kutosha kama wanaupenda urais bara basi waridhike urais wao ukiwekwa poni.
 
Let ZNZ go!!! hamna jıpya hapa bado nyimbo ni zile zile... Tunataka kuona Tanganyika inarudi na sio usanii wa kubadilisha maneno.
Hamtaki Zanzibar huru yenye mamlaka kamili!

Uwepo wa Tanganyika na ninyi kujihusisha na Tanganyika, hapo hakuna mamlaka au uhuru kamili.
Mtabaki chini ya kivuli cha Tanganyika.

Mnachoogopa kukutana EAC ni nini?
Makamu wa rasi wa ZNZ kama kawaida ameshindwa kujibu hoja kwanini ZNZ isikutane na Tanganyika huko EAC.
Amebaki kuomba ulinzi na usalama, well! hakuna msaada usio na masharti.
Sharti moja ZNZ itabaki kupumua chini ya bendera ya tangi za kijani, bluu, njano na nyeusi! passport iwe ya kijani.

As long as mnahitaji Tanganyika irudi, mnaiihitaji Tanganyika. period!
As long as mnahitaji ulinzi na usalama, basi kila mtu atakuwa raia wa Tanganyika.
Seif amesahau!
 
Kupokezana urais wa Tanzania utakuwa na maana kama vilevile urais wa Zanzibar ungeweza kupokezana na waTanganyika.
Hii itaboresha sana muungano na kama haliwezekani wazanzibari milioni moja waridhike tu kujitwala wao wenyewe na udogo wao.

Tumewabena vya kutosha kama wanaupenda urais bara basi waridhike urais wao ukiwekwa poni.

Mkuu

Unachanganya mambo hapa.

Serikali ya Muungano wa Tanzania na serikali ya Tanganyika ni kitu kimoja?

Serikali ya Tanzania ni ya muungano( serikali ya pamoja baina ya Tanganyika na Zanzibar)

Kuna mambo ya Muungano, haya yanatakiwa kusimamiwa na serikali ya Muungano

Kuna mambo yasiyo ya muungano ya Tanganyika(Jina la usanii ni Tanzania bara) haya yalipasa kushughulikiwa na serikali ya Tanganyika, pia kuna mambo yasiyo ya muungano ya Zanzibar ambayo yanasimamiwa na serikali ya Zanzibar.

Inayokosekana hapa ni serikali ya kusimamia mambo ya Tanganyika yasiyo ya muungano. Hakutakuwa na kupokezana katika kuongoza serikali ya Tanganyika. Wadanganyika hatujitambui na tunafanya ubabaishaji/ ujanja tu hata katika mambo ya msingi.

Kama ni ngumu kuelewa , soma hii mada: link https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/334649-tundu-lissu-na-kiini-macho-cha-muungano.html
 
Hamtaki Zanzibar huru yenye mamlaka kamili!

Uwepo wa Tanganyika na ninyi kujihusisha na Tanganyika, hapo hakuna mamlaka au uhuru kamili.
Mtabaki chini ya kivuli cha Tanganyika.

Mnachoogopa kukutana EAC ni nini?
Makamu wa rasi wa ZNZ kama kawaida ameshindwa kujibu hoja kwanini ZNZ isikutane na Tanganyika huko EAC.
Amebaki kuomba ulinzi na usalama, well! hakuna msaada usio na masharti.
Sharti moja ZNZ itabaki kupumua chini ya bendera ya tangi za kijani, bluu, njano na nyeusi! passport iwe ya kijani.

As long as mnahitaji Tanganyika irudi, mnaiihitaji Tanganyika. period!
As long as mnahitaji ulinzi na usalama, basi kila mtu atakuwa raia wa Tanganyika.
Seif amesahau!

Nguruvi3

CHADEMA; CUF wanataka serikali tatu.
Mjadala wa kupokezana urais wa serikali ya Muungano umeshika kasi.

Kuna watoa maoni huku Tanganyika pia wanadai serikali ya Tanganyika irudi.

Tusisahau juhudi za G55 na Rev. Mtikila.

Ni wazi, Tanganyika inarudi sio kwa sababu ya matwakwa ya Wazanzibari lakini ni kwa sababu tupo watanganyika ambao tunaelewa Muungano kama ulivyo leo ni "kiini macho".

Linapokuja suala la muungano ni wazi kuwa wabia huwa wanahitajiana/ huwa kuna masilahi fulani kwa kila upande unaojiunga katika Muungano. Kama Tanganyika iliona ni jambo jema kuingia katika muungano na Zanzibar 1964 basi kutokana na utete wa siasa ulivyo huku "Tanzania bara" siku Zanzibar ikitoka Muungano ndio tutaelewa umuhimu wake.

Kufikiria kuwa Tanganyika haihitaji Zanzibar, basi Mwalimu Nyerere angeruhusu G55 ilete serikali ya Tanganyika.

Hata wewe unaelewa vipi Zanzibar imesaidia kuifanya Tanganyika isimeguke. Kama hili hulielewi naomba ufanye utafiti. Au soma kwa makini au sikiliza kwa makini hotuba aliyotoa mwalimu kuhusu kuundwa kwa serikali ya Tanganyika na dhana ya ubaguzi.

Zanzibar imetusaidia sana katika kutuweka pamoja kama jamii moja.

Wanaoipenda Tanganyika na wanaoipenda Tanzania wanataka Kero/kiini macho cha muungano kipatiwe dawa.

Mada ya Mchambuzi https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/334649-tundu-lissu-na-kiini-macho-cha-muungano.html ni ya kuifanyia kazi.

Tutapata athari kubwa mbeleni kwa kuipuuza.
 
Mkuu

Unachanganya mambo hapa.

Serikali ya Muungano wa Tanzania na serikali ya Tanganyika ni kitu kimoja?

Serikali ya Tanzania ni ya muungano( serikali ya pamoja baina ya Tanganyika na Zanzibar)

Kuna mambo ya Muungano, haya yanatakiwa kusimamiwa na serikali ya Muungano

Kuna mambo yasiyo ya muungano ya Tanganyika(Jina la usanii ni Tanzania bara) haya yalipasa kushughulikiwa na serikali ya Tanganyika, pia kuna mambo yasiyo ya muungano ya Zanzibar ambayo yanasimamiwa na serikali ya Zanzibar.

Inayokosekana hapa ni serikali ya kusimamia mambo ya Tanganyika yasiyo ya muungano. Hakutakuwa na kupokezana katika kuongoza serikali ya Tanganyika. Wadanganyika hatujitambui na tunafanya ubabaishaji/ ujanja tu hata katika mambo ya msingi.

Kama ni ngumu kuelewa , soma hii mada: link https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/334649-tundu-lissu-na-kiini-macho-cha-muungano.html

Mkuu usisome maoni yangu juu juu bila tafakuri.
Kama Karume alijitoa, tena bila wanasheria kuingia moongano ambao umetufikisha hapa, leo wazanzibari wanalilia kuwaa kiti cha Muungano, bila aibu baada ya sakata la kupinga muungano huo, kuchoma makanisa na kwa jumla kuwabagua watanganyiks.

Leo anakuja kiongozi, tena toka CCM, anataka urais wa bure uende Zanzibar, wakati hata vidonda vya chokochoko havijapona sawasawa.

Ndio maana nasema kama mwapenda kutawala Muungano mupende nakuawaliwa na muungano vile vile.

Kwani Zanzibar ni peponi, Mtanganyika yeyote anaweza kuwa rais pale , kama ambavyo mnapendekeza mzanzibari awe rais wa muungano.

La sivyo kuwabagua waTanganyika halafu kutaka urais wa muungano ni unafiki wa hali ya juu, na sasa mnaumbuka kwa maoni yenu wenyewe.
 
Kama kuupiga muungano ingekuwa ni kitu kilichoruhusiwa katika mchakato wa Katiba mpya , sio wazanzibari tu wangetaka muungano ufikie ukomo. Watanganyika pia tungesema kwa kauli moja kuwa Muungano umetutosha, wazanzibari tumeshawachoka.

Tatizo nilionalo hapa ni kushindwa kwako kutofautisha, nini Tanganyika, nini Zanzibar, nini Tanzania.

Yepi mambo ya muungano, yepi mambo ya Tanganyika, yepi mambo ya Zanzibar.

Ukiweza kutofautisha haya ,wala hutapata maumivu ya kichwa.Pia utaweza kuelewa "mazingaombwe/kiini macho cha muungano.

Nakushauri uisome hiyo mada ya Mchambuzi kwa makini.link https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/334649-tundu-lissu-na-kiini-macho-cha-muungano.html
 
MkuuKama kuupiga muungano ingekuwa ni kitu kilichoruhusiwa katika mchakato wa Katiba mpya , sio wazanzibari tu wangetaka muungano ufikie ukomo. Watanganyika pia tungesema kwa kauli moja kuwa Muungano umetutosha, wazanzibari tumeshawachoka.Tatizo nilionalo hapa ni kushindwa kwako kutofautisha, nini Tanganyika, nini Zanzibar, nini Tanzania.Yepi mambo ya muungano, yepi mambo ya Tanganyika, yepi mambo ya Zanzibar.Ukiweza kutofautisha haya ,wala hutapata maumivu ya kichwa.Pia utaweza kuelewa "mazingaombwe/kiini macho cha muungano.Nakushauri uisome hiyo mada ya Mchambuzi kwa makini.link https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/334649-tundu-lissu-na-kiini-macho-cha-muungano.html
Mkuu sipati mchecheto wowote katika kutambua ni nini msusla ya Tanganika, Tanzania na Zanzibar.Tatio langu niwazanzibari waliopata steki ya muungano na bado wanataka kutawala Tanganika.Masuala ya muungano Tanganyika Zanzibar si misahafu twaweza kuibadilisha kwa matakwa ya kila pande inavyopenda. Na leo tukipiga kura kubadili hadidu za rejea katika mambo ya muungano nina hkika kiti cha urais Zanzibar kikiwekwa wazi Watanganyika wagombee kwa zamu, waTanganika milioni 43 wataafiki
 
hawa wa zenji kuna siku watataka wake zetu wawe wanakwenda zeji kila weekend.
Mkuu sipati mchecheto
wowote katika kutambua ni nini msusla ya Tanganika, Tanzania na
Zanzibar.Tatio langu niwazanzibari waliopata steki ya muungano na bado
wanataka kutawala Tanganika.Masuala ya muungano Tanganyika Zanzibar si
misahafu twaweza kuibadilisha kwa matakwa ya kila pande inavyopenda. Na
leo tukipiga kura kubadili hadidu za rejea katika mambo ya muungano nina
hkika kiti cha urais Zanzibar kikiwekwa wazi Watanganyika wagomee kwa
zamu, waTanganika milioni 43 wataafiki
 
Mkuu sipati mchecheto wowote katika kutambua ni nini msusla ya Tanganika, Tanzania na Zanzibar.Tatio langu niwazanzibari waliopata steki ya muungano na bado wanataka kutawala Tanganika.Masuala ya muungano Tanganyika Zanzibar si misahafu twaweza kuibadilisha kwa matakwa ya kila pande inavyopenda. Na leo tukipiga kura kubadili hadidu za rejea katika mambo ya muungano nina hkika kiti cha urais Zanzibar kikiwekwa wazi Watanganyika wagomee kwa zamu, waTanganika milioni 43 wataafiki

Kama hupati mchecheto wowote kutambua masuala/mambo ya muungano, masuala ya Tanganyika, masuala ya Zanzibar..maandishi yako yanakusuta (yanakueka uchi).

Kiti cha urais wa Zanzibar ni suala la Muungano? ni suala la Tanganyika? ni suala la Zanzibar?

Ukitoa jibu la hili suali, utapata suali moja la nyongeza. Kwa hiyo, fikiri vizuri, usikurupuke!
 
Principle ni ndogo tu mkuu, ukipenda kutawala , upende kutawaliwa-short and clear!
 
Principle ni ndogo tu mkuu, ukipenda kutawala , upende kutawaliwa-short and clear!

Kwa jibu hili inaonesha kweli wewe unajua bila mchecheto yepi mambo/masuala ya muungano, yepi mambo ya Tanganyika na yepi mambo ya Zanzibar.
 
Nonda,

..mapendekezo kwamba Uraisi wa muungano uwe wa kupokezana na kujaribu kuleta kiini macho kipya.

..tunataka Tanganyika huru, na Zanzibar huru. Ushirikiano wowote ule ufanyike kupitia jumuiya ya Afrika mashariki.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu usisome maoni yangu juu juu bila tafakuri.
Kama Karume alijitoa, tena bila wanasheria kuingia moongano ambao umetufikisha hapa, leo wazanzibari wanalilia kuwaa kiti cha Muungano, bila aibu baada ya sakata la kupinga muungano huo, kuchoma makanisa na kwa jumla kuwabagua watanganyiks.

Leo anakuja kiongozi, tena toka CCM, anataka urais wa bure uende Zanzibar, wakati hata vidonda vya chokochoko havijapona sawasawa.

Ndio maana nasema kama mwapenda kutawala Muungano mupende nakuawaliwa na muungano vile vile.

Kwani Zanzibar ni peponi, Mtanganyika yeyote anaweza kuwa rais pale , kama ambavyo mnapendekeza mzanzibari awe rais wa muungano.

La sivyo kuwabagua waTanganyika halafu kutaka urais wa muungano ni unafiki wa hali ya juu, na sasa mnaumbuka kwa maoni yenu wenyewe.

Ndugu umenikosha kweli uliposema kuwa urais wa zanzibar apewe mtanganyika kama sisi tunataka kuongoza serikali ya muungano. Nafikiri hujui kama tanganyika hakuna serikali. Kaa kitako utambue kuwa serikali ya tanzania sio serikali ya tanganyika, hivo basi kwa definitiona kila mtanzania ana haki ya kugombea urais wa JMT, na serikali ya zanzibar ni ya wazanzibari, sio serikali ya muungano ile, serikali ile inatakiwa iendelee kuongozwa na mzanzibari TU! Soma tofauti kati ya JMT na SMZ!
 
Huwezi kuwa ceremonial president halafu uwe commander in chief. Nchini Israel commander in chief ni prime minister.
Halafu tutambue kwamba Zanzibar hawana jeshi. Lazima wajue hilo. Wataongozaje jeshi la nchi nyingine? Chadema katika hili naomba mjipange upya.

Jeshi la nchi gani mkuu? Coz jeshi la tanzania sio la tanganyika, ni la tanzania, sasa ijue maana ya tanzania ndipo utakapotambua kama zanzibar wanahaki ya kutoa kiongozi wa jeshi kama sifa anazo
 
Pendekezo la kupokezana urais simply halina mantiki. Tukichukulia suala la uwiano tu basi Zanzibar tayari imeshapata nafasi nyingi za ama urais au umakamu tangu muungano na hakuna maeneo mengine ya Tanzania ambayo yamepata nafasi hiyo. Tukikubali na kama ilivyo sasa kuwa lazima makamu atoke upande mwingine wa Muungano basi Zanzibar inapendelewa kupita kiasi.

Kwanini tusiseme tu kama ilivyo Marekani kuwa Rais na Makamu wasitoke Mkoa mmoja - haijalishi kama mkoa huo uko bara au visiwani?

Tatizo mzee mwanakijiji, tanzania inaitambua serikali ya zanzibar. Pili, muungano wetu tangu mwanzo ni mkataba ambao sijamsikia mwanasheria wa serikali akasema anao. Tatu, zanzibar sio iringa, sio arusha, wala sio kama mkoa wowote kabisa kama wa tanganyika. Jengine, zanzibar iliwahi kuwa nchi yenye kutambulikana duniani, sijawahi kuskia mkoa wowote wa tanganyika wenye sifa huo.... Ushaelewa tofauti ya zanzibar na tanganyika?
 
Back
Top Bottom