CCM Zanzibar yataka urais wa Muungano ugombewe kwa zamu kati ya Tanganyika na Zanzibar

CCM Zanzibar yataka urais wa Muungano ugombewe kwa zamu kati ya Tanganyika na Zanzibar

Sidhani kama mapendekezo ya CDM mengine yamefikiriwa vizuri; inaonekana kama hayakufikiriwa kwa kina na hasa implications zake.

Mapendekezo yepi hayo ambayo unafikri hayakufikiriwa viruzi?

Na hizo "implifications" zake ni zipi kwa maoni yako, mkuu?

Wewe ungeshauri nini?

Mapendekezo yako kama "taasisi MMJ"ni yepi?
 
Nguruvi3

Sasa mshawishi na dugu yako, MMJ aandae makala moja safi ya kuipigia debe, Tanganyika huru na Zanzibar huru.

Kama hili umelikubali basi safari imeanza.

Uache masimulizi ya Seif, Jussa wakati Tanganyika haina mtetezi.

Weka fikra pevu moja juu ya Tanganyika huru na Zanzibar huru.

Unajua Mkuu Nguruvi3, wewe na ndugu yako (yetu), MMJ mna kundi kubwa(wapenzi/wafuasi wengi) hapa JF lakini baada ya kutumia ushawishi huo wa kukubalika vizuri, mnaleta maneno mengi, mnawazingua watu hapa kama CCM inavyotuzingua wadanganyika.

Sasa tutumie ushawishi huo kuitetea Tanganyika...Tanganyika huru inawezekana ikiwa tu wadanganyika tutakubali kuiondoa "d" na kuweka "t" kutoka moyoni.

Ni lazima tuwe watanganyika ndio tutaweza kutetea haki/ masilahi ya Tanganyika. Vyenginevyo, tutakuwa tunakimbiza kivuli tu na kuwatupia lawama Seif na Jussa.

Jiangalie kwenye kioo leo, halafu anza kujiambia,tamka "mimi ni mtanganyika na nitatetea masilahi ya Tanganyika"

Najua itakuwa ngumu kujibadili kutoka mtanzania bara/ mbara uliyoizoea lakini safari ya maili elfu huanza kwa kupiga hatua ya mwanzo.

1,2,3 "Mimi si mdanganyika bali ni mtanganyika"

Jaribu tena...1,2,3 "Mimi Nguruvi3 ni mtanganyika" "Nitatetea masilahi ya Tanganyika"
Unajua Nonda , siku zote tumesema LET ZNZ GO. Hii maana yake ni pana sana. Kurudi kwa Tanganyika ndio mwisho wa muungano.
Tanganyika ikirudi kutakuwa na serikali yake itakayoangalia mambo yake na hapo hapatakuwepo na uchochoro.

Ukisoma maoni ya CDM ardhi imeondolewa katika mambo ya muungano. Ingawa bado sikubaliani nao kwa mambo mengi ninachoshukuru ni kuwa mapendekezo yao yametoka 11 ya mwaka 1964 hadi 7. Hii ina maana kuna mambo 4 muhimu sana kwa ZNZ yameonolewa.

Hili la kupokezana Urais kwanza halitakubaliwa na Tanganyika. Muda muafaka ukifika kampeni itafanyika. Endapo litalazimishwa basi ZNZ inayotaka mamlaka kamili haitakuwa nayo. Kwanini nasema hivyo?

Rais wa Muungano atabeba bendera yenye rangi nyeusi, kijani, njano na bluu pale New York. Hakutakuwa na bendera ya karafuu wala jahazi. Balozi wa muungano atatoka Tanganyika.
Ikiwa Rais atatoka ZNZ bado atabeba bendera yenye kijani, nyeuism njano na bluu. Hapo ZNZ yenye mamlaka kamili itatoka wapi?

Kwa maneno mengine ZNZ itabaki katika kivuli cha Tanganyika itake isitake.
Kama inataka uhuru kamili njia ni moja tu kupitia EAC.

Ili kutopoteza muda sisi tunasema muungano ni EAC au ZNZ chini ya mwamvuli wa Tanganyika.
Hapa ni trick sana kwasababu ZNZ haitakuwa na jeshi, mamlaka kamili yatatoka wapi?

Rais wa ZNZ anaweza kuitwa Dodoma kama Jumbe na Salim au kusweka rumande kama Seif na wenye jeshi sio wenye ''mamlaka kamili''

Kwa namna yoyote itakavyouwa ZNZ yenye mamla kamili haitapatikana kwasababu njia zote muhimu za ustawi wa ZNZ ikiwa ni pamoja na za uchumi, kiusalama ni zao la Tanganyika. Itabaki kuwa katika kivuli hata kama ni muungano wa jambo moja.

Kwahiyo kuna mambo mawili, LET ZNZ GO! au ZNZ ibaki chini ya kivuli cha Tanganyika.

Think about that Nonda.
 
Nonda,

..ndiyo maana wengine tunapendekeza Tanganyika huru, na Zanzibar huru, zitakazokuwa na "muungano wa mkataba"/mashirikiano kupitia East African community.

..EAC ina secretariat ambayo inaongozwa na Katibu Mkuu, ambaye anapatikana kwa utaratibu wa kupokezana member states.
Hilo Wazanzibar hawalielewi. Tunawasidia wapate mamlaka kamili hawajui. Ukishakuwa na Tanganyika basi hakuna mamlaka kamili. Yatatoka wapi wakati huna chombo cha usalama?

Tukutane EAC kwasababu maoni ya wazanzibar na Watanganyika hayataafiakiana.
Sisi tulishasema Let ZNZ GO! haya yanayotokea yataishia huko. Kama sivyo hakuna ZNZ huru yenye mamlaka kamili.
Watapakatwa tu watake wasitake. Njia ni moja, out!
 
Hatuwezi kukubali tena huu ujinga. Minority can not rule Majority.
Milioni 45 ni kubwa kuliko milioni 2 nadhani:confused2:
 
Kwanini tuwe na kuachiana zamu na mtu wa nchi nyingine? Si wamesema wao ni nchi? Kama hivyo ndo wanataka basi na uraisi wa Zanzibar tugombee kwa zamu na Mtanganyika siku moja awe rais huko kwao. Hatuhitaji mtu toka nchi jirani kututawala.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Hawa jamaa kazi yao tupige gunzo tu, kucheza bao na kunywa kahawa, hiyo ndio biashara. Kero kwao haziishi. Siku zitakapokwisha wataanza kero za upemba na uunguja.
 
http://www.habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/8263-bunge-mahakama-wafunguka-kuhusu-katiba

Maalim Seif amesema kuwa anataka muungano lakini wa mkataba. Amemwambia Jaji Warioba kuwa katika mambo ya mkataba anataka ulinzi na usalama kwsababu ZNZ inahitaji sana hilo.

Kila siku tumekuwa tunasema, ZNZ tokea Sultan aondoke haina na haijawahi kuwa na bajeti ya Ulinzi.
Haijawahi kuchangia hata senti tano na wala haina uwezo wa kumudu bajeti ya ulinzi wa maana kwa mapato ya bilioni 120 kwa mwaka.

Kwa maana hiyo ZNZ inaihitaji Tanganyika kama alivyosema maalim na kama tunavyoelezea hapa jamvini kila siku.
Sasa hakuna ubishi kuwa muungano huu ni una masilahi kwa ZNZ pamoja na upuuzi na kejeli zao.

Hapa kinatokea nini? Kinachotokea ni kuwa Tanganyika ndiyo yenye upper hand katika muungano na maamuzi mengi yatazingatia hilo. Kwa mantiki hiyo zile kauli za ZNZ huru na yenye mamlaka kamili sasa zimekufa.
Huwezi kuwa huru na mamlaka kamili ukiwa unategemea ulinzi wa jirani.

Maana yake ni kuwa iwe iwavyo ZNZ itabaki katika kivuli cha Tanganyika.
Hilo ni moja kati ya yale manne ambayo Tanganyika ikiyaweka mezani hakuna mzanzibar atakayegungua kinywa.
Maalim Seif kasalim amri, nani amebaki !!

Njia rahisi ni EAC, kinyume chake ni bendera na wimbo tuu chukwani na Bwejuu, nje ya hapo passport ya kijani, bendera yenye nyeusi, njano, bluu na kijani mkononi, wimbo Taanzania tanzania nakupenda kwa moyo wote...... Period!

cc Mwanakijiji, Jokakuu, Jasusi, Ghibuu,
 
MR RAPHERL hapo haupo sawa kusema hivyo na kama upo sawa basi utakua unamaanisha na wewe ushaanza kuonyesha kwamba wewe mdini na unataka watu sasa waanze kutoa maoni yao humu kwa udini,kuchomwa kanisa hamna hata raisi au mtu mmoja aliefanya au kusababisha alie katika selikari hii,kwani kanisa yamechomwa kwa sababu wanaozijua wachomwaji,na usiwe unaongelea mambo ya kuchomwa makanisa ukaacha pia miskiti imeharibiwa wanajeshi wameingia na mbwa mskitini,qur an zinakojolewa zinatoswa chooni,juzi tu hapo kiwanda cha kuchapishw vitab vya kiislam kimechomwa na kimya mpaka leo,please acha hayo bwana tuachie wahusika(serikali na mahakama)wafanye yalio sawa,
 
Nguruvi3 Sasa mshawishi na dugu yako, MMJ aandae makala moja safi ya kuipigia debe, Tanganyika huru na Zanzibar huru. Kama hili umelikubali basi safari imeanza. Uache masimulizi ya Seif, Jussa wakati Tanganyika haina mtetezi. Weka fikra pevu moja juu ya Tanganyika huru na Zanzibar huru. Unajua Mkuu Nguruvi3, wewe na ndugu yako (yetu), MMJ mna kundi kubwa(wapenzi/wafuasi wengi) hapa JF lakini baada ya kutumia ushawishi huo wa kukubalika vizuri, mnaleta maneno mengi, mnawazingua watu hapa kama CCM inavyotuzingua wadanganyika. Sasa tutumie ushawishi huo kuitetea Tanganyika...Tanganyika huru inawezekana ikiwa tu wadanganyika tutakubali kuiondoa "d" na kuweka "t" kutoka moyoni. Ni lazima tuwe watanganyika ndio tutaweza kutetea haki/ masilahi ya Tanganyika. Vyenginevyo, tutakuwa tunakimbiza kivuli tu na kuwatupia lawama Seif na Jussa. Jiangalie kwenye kioo leo, halafu anza kujiambia,tamka "mimi ni mtanganyika na nitatetea masilahi ya Tanganyika" Najua itakuwa ngumu kujibadili kutoka mtanzania bara/ mbara uliyoizoea lakini safari ya maili elfu huanza kwa kupiga hatua ya mwanzo. 1,2,3 "Mimi si mdanganyika bali ni mtanganyika" Jaribu tena...1,2,3 "Mimi Nguruvi3 ni mtanganyika" "Nitatetea masilahi ya Tanganyika"
Nonda, nafikiri utatumia muda mwingi kuwaelewesha na siku zote watakusumbua sana. Kwani unatakiwa kujua maana halisi ya maneno haya KULALAMIKA NA KUNUNG'UNIKA na mwisho KUSONONEKA. Siku zote mtu mmbora ni yule anayelalamika kwani huyu anatoa na kupaza sauti kuelezea madhila anayopata. Hilo ndilo linalotumiwa na waZanzibar. hawaoni aya wala soni kuzungumzia madhila wanayopata kutokana na muungano wenu. Kunung,unika ni njia inayotumiwa na jirani zenu kutoka Bara. wao hawawezi kutumia njia rasmi za kutoa malalamiko yao bali wanabaki kujisemeza pake yao kimya kimya bila kupaza sauti. Hakika hakuna dhambi mbaya kuliko dhambi ya kunung'unika. Kusononeka ni njia ambayo WaBara wanaelekea huko. Kusononeka ni kujisemeza ndani ya moyo wako bila kutoa sauti. Hili ni jambo la kukata tamaa ya maisha kabisa na kwa Taifa ni kuuwa kabisa nchi. sasa ujue unabishana na watu wanaonung'unika na sio kulalamika.
 
kwa kuepuka hizo dhulma ndio maana wazanzibar tunataka tugawane mbao tutakutana east africa comunity . Tutapanga na kupangua kule kila mmoja akiwa huru . TANGANYIKA NA ZANZIBAR
 
Badala ya kurukia mambo ya Muungano ambayo ni MAJI MAREFU kwa ZNZ, kwanini huyu Vuai Ali Vuai asipendekeze URAIS wa SMZ wa kupokezana KIJITI kati ya visiwa vya Unguja na Pemba?!
 
........................,
Kila siku tumekuwa tunasema, ZNZ tokea Sultan aondoke haina na haijawahi kuwa na bajeti ya Ulinzi.
Haijawahi kuchangia hata senti tano na wala haina uwezo wa kumudu bajeti ya ulinzi wa maana kwa mapato ya bilioni 120 kwa mwaka.

Kwa maana hiyo ZNZ inaihitaji Tanganyika kama alivyosema maalim na kama tunavyoelezea hapa jamvini kila siku.
Sasa hakuna ubishi kuwa muungano huu ni una masilahi kwa ZNZ pamoja na upuuzi na kejeli zao.
..........,
Maana yake ni kuwa iwe iwavyo ZNZ itabaki katika kivuli cha Tanganyika. .............

Mkuu Nguruvi3

Hii thread uliipitia? Link https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/334649-tundu-lissu-na-kiini-macho-cha-muungano.html

Bado unaelekeza nguvu zako katika maneno mengi, maneno mareefu!mkuu.

Kwa nini hatupigi kampeni ya Tanganyika huru? Tukiwa na Tanganyika huru, sio Tanzania bara, tutaitetea Tanganyika na masilahi ya Tanganyika. Wakati huo huo tutatatua tatizo la "uniqueness";kiini macho cha muungano.

Hapo nilipoweka rangi nyekundu katika mchango wako, unazungumzia zaidi ushabiki kuliko ushahidi. Kuna siku ilikuja thread ya Jussa amtukana Sitta https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...tta-nyerere-na-wa-tz-bara-11.html#post3069359

link 2.https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...tta-nyerere-na-wa-tz-bara-13.html#post3069803

Link 3 https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...tta-nyerere-na-wa-tz-bara-18.html#post3071438

link 4 https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...tta-nyerere-na-wa-tz-bara-18.html#post3071464

Rafiki yako Seif ameibuka na haya:

Uchangiaji katika gharama za Muungano na mgawanyo wa mapato yanayotokana na Muungano

Je,mtu anaposema Zanzibar haichangii gharama za uendeshaji wa vyombo na taasisi za Muungano kwa sababu tu Serikali ya Zanzibar haitoi fungu la fedha na kuliingizakatika Serikali ya Muungano, Tanganyika ambayo hata Serikali haina inachangiavipi na kiasi gani? Ikiwa mchango wake unatolewa na Serikali ya Muungano, kwani hii siyo serikali ya shirika ambapo Zanzibar ni mbia? Vipi basi Zanzibar itakiwe ichangie mara mbili kwa kutumia hadhi mbili tofauti? Na ikichangia(iwapo itachangia), ina uhakika upi kwamba itakachotoa hakitatumiwa na Serikaliya Muungano kwa shughuli za Tanganyika zisizo za Muungano ikitumia mamlaka yake kwa madhumuni hayo? Vivyo hivyo kwa mapato yatokanayo na vyombo na taasisi zaMuungano, tunajua Zanzibar inapata mgao wake na kiasi chake kimewekwa wazi (ingawa kwa sasa ni mapato ya TRA yanayokusanywa Zanzibar; na pia gawio kutoka Benki Kuu(BOT) ambalo nalo kiwango chake hakikubaliki kwa Wazanzibari). Zipo mamlaka nyengine za Kimuungano zinazoingiza mapato na ambazo Zanzibar haipewi chochote kutoka kwake zikiwemo TCRA, TCAA, TPC, TTCL, na TPDC kwa kutaja chache. Masuala zaidi yanakuja: Yale mapato yanayobaki katika Serikali ya Muungano, kuna kipicha kuonyesha mpaka wa matumizi yake kwa Muungano na kwa shughuli za Tanganyika zisizo za Muungano? Uadilifu na uwajibikaji wa matumizi yatokanayo na mgao huu wa mapato utaonekana vipi?

Ukweli hasa kuhusiana na suala la uchangiaji katika gharama za Muungano na mgawanyo wamapato yanayotokana na Muungano ulipatikana kufuatia kuundwa kwa Tume ya Pamojaya Fedha (Joint Finance Commission) ambayo iliajiri wataalamu (consultantskutoka taasisi inayoheshimika duniani ya PriceWaterhouseCoopers kuangalia sualahilo. Ripoti ya Wataalamu ilitolewa Agosti 2006 na kufanyiwa kazi na Serikaliya Mapinduzi ya Zanzibar lakini hadi leo imekaliwa na Serikali ya Muungano bilashaka baada ya kutoa picha isiyopendeza kwa upande wa Tanganyika kuhusiana nahali halisi ya vipi uendeshaji wa Muungano ulivyo. Wataalamu wa Kampuni yaPriceWaterhouseCoopers walifanya uchambuzi halisi wa mambo yepi ni ya Muunganona yepi ni ya Tanganyika na yepi ni ya Zanzibar na gharama za uendeshaji wakila moja. Baada ya orodha kupatikana, watafiti wakatafuta matumizi halisi yabajeti ya vifungu hivyo kwa muda wa kiasi cha miaka 10 iliyopita. Watafiti hao walikwenda mbali zaidi ya hapo na kukusanya mapato yote kwa kila kifungu cha mambo ya Muungano halisi. Mwishowe, wakalinganisha iwapo mapato yanakidhi matumizi au yana nakisi (upungufu)?

Kilichojitokezani kwamba kwa mwaka wa fedha 2003/2004 pekee, matumizihalisi kwa vifungu vya Muungano yalikuwa Shs. 537,258.4 bilioni ambayo ni asilimia20 tu ya bajeti yote ya Serikali ya Muungano kwa mwaka huo. Mapato halisi yavyanzo vya mapato vinavyotokana na mambo ya Muungano kwa mwaka huo yalikuwa niShs. 1,030,826.1 bilioni. Tofauti ya vifungu hivyo vimetoa ziada ya Shs.493,567.7 bilioni kwa mwaka huo. Ziada hii haiingizi mapato yanayotokana na misaada kutoka nje au mikopo. Ziada hii hutumika kwa shughuli za Tanganyika zisizo za Muungano.

Ukweli huu unaonyesha hata kama kungekuwa na Serikali tatu kusingekuwa na haja yoyotekwa Serikali ya Zanzibar na ile ya Tanganyika kulipia fedha za ziada kamawahusika watatunza na kuweka kumbukumbu sahihi za mapato na matumizi ya mamboya Muungano halisi badala ya yale ya Tanganyika kuchanganywa na ya Muungano.Mambo yasiyokuwa ya Muungano ya Tanganyika yalipotengwa nje ya yale ya Muungano, gharama za mambo ya Muungano zimejidhihirisha wazi bila ya kujificha na kuonesha kwamba zinaweza kulipiwa kupitia mapato ya mambo ya Muungano pekee na ziada kubaki. Lakini hili limekuwarahisi kwa kukubali ukweli kwamba kuna mafungu matatu ya mapato na matumizi katika Serikali zetu mbili. Mafungu hayo ni la SMZ kwa mambo yake yasiyo mamboya Muungano, la Serikali ya Muungano kwa mambo ya Muungano, na la Serikali ya Muungano inayofanya kazi za Tanganyika kwa mambo yasiyokuwa ya Muungano.

Inapatikana yote hapa ZanziNews : Warka wa Maalim Seif kwa tume ya kuratibu maoni ya katiba

Kama unaweza kuipata hiyo ripoti, au kama kuna mtu /invisible ataipata aimwage hapa JF, hii itasaidia kuona hali halisi ya muungano wa mazingaombwe unavyoendeshwa na tutaacha kutegemea ushabiki na jazba tunapojadili suala nyeti la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kiini macho/ mazingaombwe/ usiri na ubabaishaji,usanii na ujanja kilichodumu kwa miaka 48.
 
Nonda,
Huyu ndiye Seif aliyesema tatizo la muungano ni ajira chache kwa waznz katika balozi!! sishangai kama atakuja na kituko kingine maana mzee wetu umri,political pressure hasa ya Urais vinamtafuna sana.

Alichokiweka hapo juu ni upuuzi kwasababu Seif lazima kwanza aangalie kuwa bajeti ya ZNZ ni Bilioni 630, mapato ya ZNZ ni bilioni 120. Tofauti ya bilioni 510 zinatoka wapi.

Seif kabla hajaongelea muungano ni lazima aelewe kuwa mshahara wake kama ulivyo wa Wawakilishi na wabunge wa ZNZ unatoka wapi.

Seif anajifanya zezeta asiyejua kuwa umeme anaotumia yeye na wacheza bao wote wa ZNZ haulipiwi na SMZ na unatoka Tanganyika.

Hesabu za Seif na jamii inayomhusu ni za kipekee . Viongozi wote wa CUF na SMZ pamoja na UAMSHO wamesoma bure bila senti tano. Kuna mamia ya watoto waliopata division mbovu kutoka ZNZ waliosajiliwa kwa mgongo wa ZNZ na wasiolipa hata senti tano wapo bara.

Bajeti ya wizara ya elimu ya juu tu kama itakuwepo ZNZ maana yake ni robo ya mapato ya bilioni 120, sijui kiatatokea nini

Seif lazima aelewe kuwa ZNZ haijawhi kuwa na bajeti ya ulinzi na amekiri juzi kuwa ni muhimu sana kwake.
Kwa bajeti ya bilioni 900 ambayo ni bilioni 300 zaidi ya ile ya ZNZ na bilioni 800 zaidi ya kipato cha ZNZ, ZNZ ina kitu gani inaweza kusema itachangia au inadhulumiwa.

Seif na Nonda lazima waelewe kuwa si gawio la BoT tu, mshahara wa mfanyakazi wa SMZ unatoka Dar kuanzia Ofisi ya Rais hadi mfagizi ofisi ya Seif. Ndege anayotumia Seif na Viong'ora haviwezi kuhimiliwa na bajeti inayotegemea mapato ambayo ni madogo kuliko kusanyo la siku moja la Tanganyika.

Seif hajui kuwa usalama wake na familia yake havilipiwi na ZNZ kwasababu kwa mapato ya bilioni 120 chache kuliko bajeti ya akina mama na watoto, ZNZ inatoa wapi pesa za kumlipa askari hata kama ni mzee wa kimakonde.
Kwahiyo anapoandika lazima atumie na akili za zaida kama za darasani zinaleta tabu.

JMT inakusanya bilioni 790 kwa mwezi mmoja, ZNZ inakusanya Bilioni 10 kwa mwezi. Ni ujinga kama si hesabu za ZNZ kudhani kuwa uwepo wa serikali ya tatu utaweza kuhudumiwa na taifa lisiloweza kulipa polisi, jeshi au mshahara wa mfanyakazi.

Tumemweleza Seif kuwa Tanganyika ikirudi kila kitu mezani. Tayari mambo yamependekezwa kutoka 11 hadi 7 na pengine yatabaki 2 au 1, hapo Wazanzibar watasaga meno.

Nonda, Seif si anataka Zanzibar huru yenye mamlaka, kwanini ang'ang'anie tena serikali 3 au mkataba.
Kwa vyovyote vile ndani au nje ya muungano, ustawi wa ZNZ ni chini ya kivuli cha bendera ya njano, nyeusi, kijani na bluu. Ustawi wa mzanzibar unategemea passport ya kijani.period. Hakuna ZNZ huru ndani ya kivuli cha Tanganyika.

Laki 500 wameshatambua hilo! ndio maana wapo huku, Seif haelewi kuwa hilo linaongeza mzigo wa huduma kwa wakimbizi wa ndani kama wale wa burundi, tofauti ikiwa ni passport.

Kuna mambo mawili
Let ZNZ GO iwe huru na mamlaka tukutane EAC
ZNZ ibaki chini ya mwamvuli mwanana wa Tanganyika.
 
Hilo Wazanzibar hawalielewi. Tunawasidia wapate mamlaka kamili hawajui. Ukishakuwa na Tanganyika basi hakuna mamlaka kamili. Yatatoka wapi wakati huna chombo cha usalama?

Tukutane EAC kwasababu maoni ya wazanzibar na Watanganyika hayataafiakiana.
Sisi tulishasema Let ZNZ GO! haya yanayotokea yataishia huko. Kama sivyo hakuna ZNZ huru yenye mamlaka kamili.
Watapakatwa tu watake wasitake. Njia ni moja, out!

LET ZNZ GO!...Zanzibar huru haizuiliki tena, utamueleza nini Baba wako wa Taifa?
 
labda upokezane na uraisi wa zanzibar...hivi mnafikiri uraisi ni taarabu ama??
 
Nonda,
Huyu ndiye Seif aliyesema tatizo la muungano ni ajira chache kwa waznz katika balozi!! sishangai kama atakuja na kituko kingine maana mzee wetu umri,political pressure hasa ya Urais vinamtafuna sana.

Alichokiweka hapo juu ni upuuzi kwasababu Seif lazima kwanza aangalie kuwa bajeti ya ZNZ ni Bilioni 630, mapato ya ZNZ ni bilioni 120. Tofauti ya bilioni 510 zinatoka wapi.

Seif kabla hajaongelea muungano ni lazima aelewe kuwa mshahara wake kama ulivyo wa Wawakilishi na wabunge wa ZNZ unatoka wapi.

Seif anajifanya zezeta asiyejua kuwa umeme anaotumia yeye na wacheza bao wote wa ZNZ haulipiwi na SMZ na unatoka Tanganyika.

Hesabu za Seif na jamii inayomhusu ni za kipekee . Viongozi wote wa CUF na SMZ pamoja na UAMSHO wamesoma bure bila senti tano. Kuna mamia ya watoto waliopata division mbovu kutoka ZNZ waliosajiliwa kwa mgongo wa ZNZ na wasiolipa hata senti tano wapo bara.

Bajeti ya wizara ya elimu ya juu tu kama itakuwepo ZNZ maana yake ni robo ya mapato ya bilioni 120, sijui kiatatokea nini

Seif lazima aelewe kuwa ZNZ haijawhi kuwa na bajeti ya ulinzi na amekiri juzi kuwa ni muhimu sana kwake.
Kwa bajeti ya bilioni 900 ambayo ni bilioni 300 zaidi ya ile ya ZNZ na bilioni 800 zaidi ya kipato cha ZNZ, ZNZ ina kitu gani inaweza kusema itachangia au inadhulumiwa.

Seif na Nonda lazima waelewe kuwa si gawio la BoT tu, mshahara wa mfanyakazi wa SMZ unatoka Dar kuanzia Ofisi ya Rais hadi mfagizi ofisi ya Seif. Ndege anayotumia Seif na Viong'ora haviwezi kuhimiliwa na bajeti inayotegemea mapato ambayo ni madogo kuliko kusanyo la siku moja la Tanganyika.

Seif hajui kuwa usalama wake na familia yake havilipiwi na ZNZ kwasababu kwa mapato ya bilioni 120 chache kuliko bajeti ya akina mama na watoto, ZNZ inatoa wapi pesa za kumlipa askari hata kama ni mzee wa kimakonde.
Kwahiyo anapoandika lazima atumie na akili za zaida kama za darasani zinaleta tabu.

JMT inakusanya bilioni 790 kwa mwezi mmoja, ZNZ inakusanya Bilioni 10 kwa mwezi. Ni ujinga kama si hesabu za ZNZ kudhani kuwa uwepo wa serikali ya tatu utaweza kuhudumiwa na taifa lisiloweza kulipa polisi, jeshi au mshahara wa mfanyakazi.

Tumemweleza Seif kuwa Tanganyika ikirudi kila kitu mezani. Tayari mambo yamependekezwa kutoka 11 hadi 7 na pengine yatabaki 2 au 1, hapo Wazanzibar watasaga meno.

Nonda, Seif si anataka Zanzibar huru yenye mamlaka, kwanini ang'ang'anie tena serikali 3 au mkataba.
Kwa vyovyote vile ndani au nje ya muungano, ustawi wa ZNZ ni chini ya kivuli cha bendera ya njano, nyeusi, kijani na bluu. Ustawi wa mzanzibar unategemea passport ya kijani.period. Hakuna ZNZ huru ndani ya kivuli cha Tanganyika.

Laki 500 wameshatambua hilo! ndio maana wapo huku, Seif haelewi kuwa hilo linaongeza mzigo wa huduma kwa wakimbizi wa ndani kama wale wa burundi, tofauti ikiwa ni passport.

Kuna mambo mawili
Let ZNZ GO iwe huru na mamlaka tukutane EAC
ZNZ ibaki chini ya mwamvuli mwanana wa Tanganyika.

Huo ndio uchambuzi wa mtanganyika maarufu katika mtandao huu... Huyu ndie anaeaminika hapa katika masuala ya Muungano. Anakuja na pumba kama hizi ! Hawa wengine wataleta nini?

Zanzibar tunawapa mishahara , Zanzibar tunawabeba , Zanzibar...Blah...blah....
Chakujiulza hapa, hivi nani analazimisha Muungano? Kauli ya wa ZNZ walioo wengi inaeleweka kwamba hawataki Muungano. Hili liko wazi, anaesema anataka mkataba au serikali 3, hii ni kukidhi matakwa ya kisiasa.

Kwa katiba ambayo bado unatumika hivi sasa haimpi uhuru mwana siasa kuukataa Muungano...Hili liko wazi. Ni sawa na kusema Muungano unakataliwa katika njia za kikatiba na kisheria...Sisi ambao sio wana siasa hatutafuni maneno, tumechoka na dhuluma za watanganyika, na tunakoelekea ni kubaya.

Nchi hii itageuka uwanja wa fujo, chonde chonde.
 
Unaandika misitari mingi lakini bado ni masimulizi tu.

Ripoti hiyo iliyotajwa hajaitayarisha Jussa wala Seif, hajaitayarisha Nonda au Nguruvi3.

La muhimu ni kuitafuta au kuiomba kutoka kwa Pinda au Bunge ili iwekwe hadharani. Wananchi wapate kuisoma na kujionea usanii wa muungano. Lissu/ Zitto tupatieni hii ripoti tajwa.

Hili ndio litaweka mjadala wa nani anafaidika, nani anadhulumiwa kwenye mwanga.

Unasema bajeti/mapato ya Zanzibar ni madogo. Hilo ni sawa ukilinganisha na Bajeti/mapato ya Tanganyika lakini pia unasahau matumizi kulingana na idadi ya watu/wananchi wa Tanganyika na wale wa Zanzibar.
Sensa ya juzi kama haikuchakachuliwa imeweka 43 milioni Tanganyika na 1.3milioni Zanzibar.(Tanzania 44 milioni kuelekea 45milioni)

Nilivyofahamu mimi ni kuwa kuna shughuli/mambo ya muungano ambayo yanaingiza mapato na pia yanahitaji matumizi. Sasa kama hesabu alizoziweka rafiki yako Seif ni sahihi basi misitari unayoiandika itakuwa haina maana yoyote zaidi ya kuonesha kukerwa tu na matamshi na kauli za wacheza bao na huyo rafiki yako, Seif.

Seif amebainisha kuwa kuna mambo ya Tanganyika, kuna mambo ya pamoja/Tanzania na kuna mambo ya Zanzibar na kila kundi/fungu lina mapato na matumizi yake.

Sisi wengine, tunataka kuona hiyo ripoti na sio kauli tatanishi au utamu wa maneno yako. Naamini unaandika kwa kujiamini kuwa uko sahihi na pengine unaamini kuwa usemayo ni kweli/ukweli lakini ripoti hiyo ikiwekwa hadharani ndio itakayotoa jibu sahihi, pia itakayothibitisha kama uko sahihi au unaandika riwaya tu kufurahisha umati.
 
Kilicho nyuma ya pazia ni kwamba wanataka rais ajaye awe Muislam tena ili waendelee kupendelewa kama anavyofanya JK. Wakristo tuwe makini na kauli kama hizi.
 
Huo ndio uchambuzi wa mtanganyika maarufu katika mtandao huu... Huyu ndie anaeaminika hapa katika masuala ya Muungano. Anakuja na pumba kama hizi ! Hawa wengine wataleta nini?

Zanzibar tunawapa mishahara , Zanzibar tunawabeba , Zanzibar...Blah...blah....
Chakujiulza hapa, hivi nani analazimisha Muungano? Kauli ya wa ZNZ walioo wengi inaeleweka kwamba hawataki Muungano. Hili liko wazi, anaesema anataka mkataba au serikali 3, hii ni kukidhi matakwa ya kisiasa.

Kwa katiba ambayo bado unatumika hivi sasa haimpi uhuru mwana siasa kuukataa Muungano...Hili liko wazi. Ni sawa na kusema Muungano unakataliwa katika njia za kikatiba na kisheria...Sisi ambao sio wana siasa hatutafuni maneno, tumechoka na dhuluma za watanganyika, na tunakoelekea ni kubaya.
Nchi hii itageuka uwanja wa fujo, chonde chonde.
Juzi kushinda jana maalim Seif kasema anataka mkataba hasa wa ulinzi. Sefi kasema koti likikuna na ubadilisha ''size'' hakusema unalivua.
Oktoba 6 2012, Nasor Moyo, Jusa, Himidi wamesema kuwa wanataka muungano kwa sababu za kijiografia, usalama na ulinzi.

Katika makundi yaliyotoa maoni ZNZ hakuna hata moja lililosema sasa basi, kila kundi ikiwemo CUF na UAMSHO wamesema wanataka muungano lakini....

Mkuu Takashi, mimi ni mwananchi tu wa kawaida kama alivyo mwingine hapa JF. Kabla hujahoji uwezo wangu, ningekushauri uhoji uwezo wa makamu wa rais wa nchi yako anayedai tatizo la muungano ni ajira za ubalozi.
Ningekushauri uhoji uwezo wa Profesa wako asiyejua katiba ya ZNZ na asemaye ni nchi ya kiislam.

Tuliza moyo na ghadhabu kwanza ili uweze kupambana na hoja. Nimeweka mahesabu hapo ni wajibu wako useme hapa ndio hapa sivyo. Matusi ni mzalendo.net hapa ni kisima cha fikra na ustaarabu. Mtihani wa matusi tulishafeli wengine.

Naweka hoja hapa tena.
Bajeti ya ZNZ ni bilioni 630. Mapato kwa mwezi ni bilioni 10, kwa mwaka ni bilioni 120.
Tofauti ya bilioni 510 inapatikana kutoka wapi?

Si kweli kuwa ving'ora vya Seif ni kutoka bara, maana Seif katika historia yake ya utumishi wa umma hajawahi kukaa katika meza hata siku moja kuandika au kujadili bajeti ya ulinzi na usalama.

Bajeti ya ulinzi na usalama ikiwa ni pamoja na ile ya mambo ya ndani ni zaidi ya trilioni 1, ikiwa ni mara 10 ya mapato ya ZNZ na mara mbili ya ''bajeti '' ya ZNZ. Uongo uko wapi hapo?

Je, si kweli kuwa WZNZ hawajui bei ya umeme kuanzia mkunazini hadi kiembe samaki, bwejuu hadi kwa mtipura, kisiwandui hadi kibanda maiti, mji mkongwe hadi mfereji maringo.
Je, ni uongo huo?

Je, si kweli kuwa ZNZ inapata mgao wake kutoka JMT pamoja na mishahara bure? Uongo uko wapi
Je, si kweli kuwa ada za mashirika ya SMZ nje ya nchi zinalipwa na JMT na siyo SMZ? uongo uko wapi?

Je, si kweli kuwa kuna watoto wa ZNZ wanaopata nafasi za upendeleo bila ushindani katika vyuo vya bara hata kama i kiwango duni? uongo uko wapi.

Je, si kweli kuwa Tanganyika imebeba WZN wengi kuliko taifa lolote dunia katika historia ya ulimwengu? Nimekosea wapi

Je, si kweli kuwa wanaotaka mkataba wa uswiss, Hong Kong, Ujerumani na Zimbwabwe ni WZNZ? wapi nimekosea

Je,si kweli kweli kuwa bajeti ya elimu ya juu, Seif na wasomi wa ZNZ hawajawahi kukaa kitako na kuiandika achilia mbali kuisoma? Wapi uongo

Zanzibar huru haitapatikana kama kuna kishikizo''attachment'' na Tanganyika.
Huo ni ukweli mchungu sana kwasababu utakuaje huru huku mlinzi anayekulinda hujui analipwa na nani?

Zanzibar huru haitapatika endapo inategemea watoto wasomeshwe na jirani kwa hisani.

Zanzibar huru haitapatikana kwa vile kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni inategemea uwepo wa Tanganyika.

Zanzibar huru ITAPATIKANA pale tu ZNZ itakapokutana na Tanganyika FIFA, AU, SADC au EAC.

Znz huru itapatikana pale itakapokuwa na bendera New York, kama ni ile nyeusi, bluu, kijani na njano hakuna ZNZ huru

ZNZ huru itapatikana kukiwa na HATI NYINGINE na si kupitia passport ya kijani.

Ndio maana tunasema, uwepo mkataba, serikali 3, tano n.k. mazingira ya kidunia yanalazimisha ZNZ ibaki katika kivuli mwanana cha Tanganyika, kwa hiari kwa lazima hiyo ndio natural justice isemavyo, si mimi.

Badala ya kutafuta kiambaza na uchochoro wa kusitiri shida zenu, kuna mambo mawili tu mbele yenu
1. Let ZNZ GO! tukutane FIFA, EAC n.k.
2. ZNZ ijishikize Tanganyika ikiwa ime surrender uhuru kamili. Itulie katika kivuli cha Tanganyika njema apendaye aje!
 
Nonda,

..kuna kitu Maalim Seif anaficha.

..kama ZNZ wangekuwa wanachangia, nakuhakikishia Maalim asingesita kutoa takwimu hizo.

..zaidi, kama Maalim anadai kuna mapato yanayotokana na vyanzo vya muungano, kwanini asibainishe kwa upande wa ZNZ vyanzo hivyo ni vipi na vinachangia kiasi gani??

..katika bunge la bajeti lililopita Dr.Bilal amepewa sh bil 32 kwa ajili ya maendeleo ya ZNZ. sasa mapesa hayo yangeweza kujenga shule 15 za kisasa kwa wananchi wa Lindi na Mtwara ambao wanadai wametengwa na wa-Tanzania wenzao.

..Tunataka Tanganyika huru, na Zanzibar huru, zenye mashirikiano kupitia Jumuiya ya Afrika Mashariki.

cc: Nguruvi3
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom