CCM Zanzibar yataka urais wa Muungano ugombewe kwa zamu kati ya Tanganyika na Zanzibar

CCM Zanzibar yataka urais wa Muungano ugombewe kwa zamu kati ya Tanganyika na Zanzibar

Maalim Seif mwenyewe hana nyumba Zenj badala yake ni mkazi wa Dar city centre, Upanga! Kaazi kweli kweli
Kama ni kweli usemayo, basi huyu rafiki ya Nguruvi3 ni mtu anaefaa kupewa dhamana ya kuongoza nchi. Si fisadi.Viongozi wenzake wote ni kujenga mahekalu na kuweka akiba ya "vijisenti " katika mabenki ya nje.
 
Jokakuu, mwanakijiji na wadau wote, kuna point hapa naiona. Endapo wazanzibar wanataka kupokezana urais (kama itatokea maana uwezekano ni karibu na hakuna) basi kwanza tuwatake watuonyeshe mfano wa kugawa madaraka kati yao na asilimia 1 ya wazanzibar wakristo.

Kama wanasema wingi wa waislam ndio kigezo, basi kwanini wingi wa Watangayika usiwe kigezo.
They must walk the talk.

mambo mawili tu mbele yao
1. Uhuru kamili na mamlaka ndani ya EAC
2. Mkataba, serikali 3 ndani ya kivuli mwanana na maridhawa cha Jamhuri ya watu wa Tanganyika.

Kuna mchangiaji alisema haya ya waislamu na wakristo kupokezana.link https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-ya-tanganyika-na-zanzibar-5.html#post5470775

Nguruvi3

Bado unawatatiza wasomaji wengi.

Ujanja tulioufanya ndio unatuletea matatizo.

Tungekuwa na mfumo wa shirikisho (serikali tatu), hizi kelele za leo za wazanzibari zingekuwa hazina nafasi.

Ingekuwepo serikali ya Tanganyika, serikali ya Tanzania(muungano) na serikali ya Zanzibar.

Nani angeongoza serikali ya Tanganyika, muislamu, mkristo, muabudu dini za asili au pagani ingekuwa ni utaratibu wa ndani wa Tanganyika. Hivyo hivyo ingekuwa kwa upande wa Zanzibar wangeamua wenyewe na sio kwa matwakwa yetu au vile Nonda na Nguruvi3 wanataka.

Linapokuja nani ataongoza serikali ya Tanzania(muungano), mimi Nonda naona kuna mantiki kwa wanaosema iwe ni kwa kupokezana baina ya Rais wa Tanganyika na Rais wa Zanzibar/ mtanganyika na Mzanzibari.

Kushindwa kwetu kutofautisha baina ya serikali ya Muungano na serikali ya Tanganyika ndio inayotuletea kuandika vitu vya ajabu.
Sasa tukubali kuwa tulifanya kosa kuifuta serikali ya Tanganyika na tusawazishe kosa hilo. Huu ndio muda mwafaka wa kufanya hivyo. Kuna katiba mpya inaandaliwa, kwa umoja wetu wadanganyika tudai iwepo serikali na katiba ya Tanganyika.

Tanzania (muungano) kama itakuwepo basi naungana na mawazo ya mambo 7 ya muungano, rafiki yako seif ameweka mambo 4.
Tulianza na muundo mbovu wa muungano, serikali mbili, mamlaka tatu(mambo ya muungano (Tanzania), mambo yasiyo ya muungano kwa Tanganyika, mambo yasiyo ya muungano kwa Zanzibar). Baadae tukaondoa Rais wa Zanzibar kuwa makamu wa rais wa Muungano(Tanzania).Na sasa tunadai serikali moja,taifa moja, nchi moja.

Kila siku zinavyosonga mbele ndio tunazidisha utata na kero za muungano lakini tunapiga kelele kuwa ni wazanzibari ndio wanalalamika tu. Watanganyika tunajidanganya, tunajichanganya.

Kama ulivyosema Zanzibar ni kisehemu tu kama Mafia au Ukerewe sioni ni kwa nini tupate tabu ya kukiachia ili tupate kushughulikia mahitaji ya watu milioni 43.6

Tuache usanii, wadanganyika wenzangu, tudai Tanganyika yetu...kwa kung'ang'ania Tanzania ni kukubali kupata maumivu. Tanzania ni ya wote.Tanganyika ni kwa watanganyika tu.
 
Huo ndio uchambuzi wa mtanganyika maarufu katika mtandao huu... Huyu ndie anaeaminika hapa katika masuala ya Muungano. Anakuja na pumba kama hizi ! Hawa wengine wataleta nini?

Zanzibar tunawapa mishahara , Zanzibar tunawabeba , Zanzibar...Blah...blah....
Chakujiulza hapa, hivi nani analazimisha Muungano? Kauli ya wa ZNZ walioo wengi inaeleweka kwamba hawataki Muungano. Hili liko wazi, anaesema anataka mkataba au serikali 3, hii ni kukidhi matakwa ya kisiasa.

Kwa katiba ambayo bado unatumika hivi sasa haimpi uhuru mwana siasa kuukataa Muungano...Hili liko wazi. Ni sawa na kusema Muungano unakataliwa katika njia za kikatiba na kisheria...Sisi ambao sio wana siasa hatutafuni maneno, tumechoka na dhuluma za watanganyika, na tunakoelekea ni kubaya.

Nchi hii itageuka uwanja wa fujo, chonde chonde.

Takashi usitutishe wala usifikiri tunawaogopa nyie kupe mmezoea kunyonya sawa na yule mdudu anaitwa mnyula anaenyonya kwa kugandiana mwilini mwa binadamu hadi ashibe
Hatutaki muungano wa kuwabeba umeme mnatumia bure,elimu mnalipiwa hata wasio na sifa za kulipiwa,mnafanya biashara bara halafu leo mnaongea dharau? Hamtusaidii kitu chochote huo muungano na ufe tu enzi ya kubebwa imepitwa na wakati na mandevu yenu kweeeeeeenda
 
Kuna mchangiaji alisema haya ya waislamu na wakristo kupokezana.link https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-ya-tanganyika-na-zanzibar-5.html#post5470775

Nguruvi3

Bado unawatatiza wasomaji wengi.

Ujanja tulioufanya ndio unatuletea matatizo.

Tungekuwa na mfumo wa shirikisho (serikali tatu), hizi kelele za leo za wazanzibari zingekuwa hazina nafasi.

Ingekuwepo serikali ya Tanganyika, serikali ya Tanzania(muungano) na serikali ya Zanzibar.

Nani angeongoza serikali ya Tanganyika, muislamu, mkristo, muabudu dini za asili au pagani ingekuwa ni utaratibu wa ndani wa Tanganyika. Hivyo hivyo ingekuwa kwa upande wa Zanzibar wangeamua wenyewe na sio kwa matwakwa yetu au vile Nonda na Nguruvi3 wanataka.

Linapokuja nani ataongoza serikali ya Tanzania(muungano), mimi Nonda naona kuna mantiki kwa wanaosema iwe ni kwa kupokezana baina ya Rais wa Tanganyika na Rais wa Zanzibar/ mtanganyika na Mzanzibari.

Kushindwa kwetu kutofautisha baina ya serikali ya Muungano na serikali ya Tanganyika ndio inayotuletea kuandika vitu vya ajabu.
Sasa tukubali kuwa tulifanya kosa kuifuta serikali ya Tanganyika na tusawazishe kosa hilo. Huu ndio muda mwafaka wa kufanya hivyo. Kuna katiba mpya inaandaliwa, kwa umoja wetu wadanganyika tudai iwepo serikali na katiba ya Tanganyika.

Tanzania (muungano) kama itakuwepo basi naungana na mawazo ya mambo 7 ya muungano, rafiki yako seif ameweka mambo 4.
Tulianza na muundo mbovu wa muungano, serikali mbili, mamlaka tatu(mambo ya muungano (Tanzania), mambo yasiyo ya muungano kwa Tanganyika, mambo yasiyo ya muungano kwa Zanzibar). Baadae tukaondoa Rais wa Zanzibar kuwa makamu wa rais wa Muungano(Tanzania).Na sasa tunadai serikali moja,taifa moja, nchi moja.

Kila siku zinavyosonga mbele ndio tunazidisha utata na kero za muungano lakini tunapiga kelele kuwa ni wazanzibari ndio wanalalamika tu. Watanganyika tunajidanganya, tunajichanganya.

Kama ulivyosema Zanzibar ni kisehemu tu kama Mafia au Ukerewe sioni ni kwa nini tupate tabu ya kukiachia ili tupate kushughulikia mahitaji ya watu milioni 43.6

Tuache usanii, wadanganyika wenzangu, tudai Tanganyika yetu...kwa kung'ang'ania Tanzania ni kukubali kupata maumivu. Tanzania ni ya wote.Tanganyika ni kwa watanganyika tu.
Nonda, hivi Seif amependekeza mambo gani?
unayo orodha tafadhali
 
Rutashubanyuma, GEORGE jinasa, Kiranga, Nguruvi3, Nyani Ngabu, Kitila Mkumbo, Mzee Mwanakijiji, wana JF,

..nimeshangaa CHADEMA na CCM wanakubaliana ktk hoja hii.

..hii dhana ya kupokezana inakwenda kinyume na suala zima la uraia wa MUUNGANO/TANZANIA.

..uraia ni mmoja, hakuna uraia wa Tanzania-Tanganyika, au uraia wa Tanzania-Zanzibar.

..kwa msingi huo, haki raia wa Tanzania ya kuchaguliwa na kuchagua itakuwa inapokwa[?] ikiwa tutaamua kwamba nyakati fulani wananchi wa upande mmoja wa muungano hawawezi kupata haki ya kuchaguliwa kwa misingi ya upande wanapotokea.

..zaidi, kwanini inapendekezwa ktk nafasi ya Uraisi tu, na siyo nafasi nyingine ktk serikali ya muungano kwa mfano:Jaji Mkuu, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Gavana wa BOT, Kamishna mkuu wa TRA, Katibu wa Baraza la mitihani, Mabalozi ktk nchi mbalimbali, etc etc??

cc: Molemo, Pasco, Sikonge, Jasusi, Mikael P Aweda

Kwani kuna sehemu CDM tumesema tunauunga mkono ujuha huu?
 
Nonda, hivi Seif amependekeza mambo gani?
unayo orodha tafadhali
Mkuu Nguruvi3

Umenichekesha kidogo lakini .....

Niliweka kiungo(link) hapa https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-ya-tanganyika-na-zanzibar-4.html#post5459412
Ukiingia huko utasoma maoni yake kwa tume ya Warioba na nini anataka/ anapendekeza.

Orodha unayotaka pia iko huko.

Ukiona hii, ujue ndio link itakupa yote ya rafiki yako, Magazeti huwa yanaandika kuuza toleo.
Inapatikana yote hapa ZanziNews : Warka wa Maalim Seif kwa tume ya kuratibu maoni ya katiba

Pia iko hii AUDIO | DW.DE

Au hii Mitazamo tafauti juu ya Muungano haijaigawa SMZ - Seif | Masuala ya Jamii | DW.DE | 15.01.2013

Huyu rafiki yako naona anatusaidia tupate Tanganyika yetu. Sisi wadanganyika wenyewe ndio tunapiga usingizi.
 
Kwani kuna sehemu CDM tumesema tunauunga mkono ujuha huu?
Kitila Mkumbo,

..kuna summary ya mapendekezo ya katiba yaliyotolewa na CDM.

..soma kipengele # 6 kuhusu raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba (kulia) wakiongozwa na Dkt. Salim Ahmed Salim wapokea maoni kuhusu Katiba Mpya kutoka kwa uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ulioongozwa na Mwenyekiti wake Ndg. Freeman Mbowe katika Ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam leo Januari 7, 2013.

A. JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA MUUNDO WAKE
1. Kutakuwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo itakuwa ni shirikisho lililoundwa na nchi ya Tanganyika na nchi ya Zanzibar.
2. Kutakiwa na haki kamili ya kila nchi inayounda Jamhuri ya Muungano kujitoa katika Muungano lakini haki hiyo itatumiwa kwa masharti kwamba uamuzi wa kujitoa katika Jamhuri ya Muungano lazima upate ridhaa wa upande husika kwa kura ya maoni (referendum/plebiscite) kwa idadi isiyopungua theluthi mbili ya kura zote halali.
3. Kutakuwa na Serikali ya Muungano ambayo itakuwa na madaraka juu ya mambo ya Muungano pekee. Mambo ya Muungano yatakuwa yafuatayo:
(a) Mambo ya nje yanayohusu masuala ya diplomasia lakini yasiyohusu ushirikiano wa kimataifa;
(b) Ulinzi na usalama isipokuwa kwa masuala ya polisi na magereza;
(c) Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano (Supreme Court of the United Republic);
(d) Uraia na uhamiaji;
(e) Sera za fedha na sarafu;
(f) Sera za biashara ya kimataifa na masuala ya forodha;
(g) Masuala ya ithibati ya elimu ya juu.
4. Kutakuwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano ambaye atakuwa Mkuu wa Serikali ya Muungano, Mkuu wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Ulinzi ya Jamhuri ya Muungano.
5. Rais wa Jamhuri ya Muungano atachaguliwa na Wajumbe wote wa Bunge la Muungano, Bunge la Tanganyika, Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wenyeviti, mameya na magavana wote.

6. Rais wa Jamhuri ya Muungano atachaguliwa kwa kipindi kimoja cha miaka mitano na anaweza kuchaguliwa kwa kipindi kingine kimoja cha miaka mitano, na atachaguliwa kwa msingi wa kuachiana zamu ya kushikilia madaraka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano Kati ya nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano.

cc: Nguruvi3, Nonda
 
Nonda,
Niliangalia hiyo link, nilidhani ameibuka na kitu kipya maana kila uchao anabadili position
Thanks
 
Mkuu Jokakuu,
Tumeangalia baadhi ya mambo yaliyopotoshwa na maalimu kama gharama za muungano.
Tumeacha baadhi ya vichekesho.

Maalim anasema tuwe na muungano wa mkataba. Moja ya faida zake ni kuvutia nchi nyingine zijiunge.
Makamu wa Rais ana tatizo la ufahamu. Hivi sasa kuna SADC, AU, EAC n.k. sasa anataka tumvutie nani tena.

Pili, anasema maeneo ya ushirikiano ni kama utabiri wa hali ya hewa! please! yaani alichokiona Seif kama tatizo la pande mbili ni utabiri wa hali ya hewa. Jamani!

Halafu anasema eneo lingine la ushirikiano ni rasilimali watu! hapa anataka uchochoro wa biashara, ajira na ardhi.
Anataka ulinzi na usalama ili akwepe najeti kama alivyokwepa tangu kuzaliwa.

Ameulizwa vipi tusiende EAC, jibu lake halilingani na la makamu wa rais aliyewahi kuwa waziri kiongozi.
Naogopa kujadili hoja zake, ni aibu tupu.

Mwisho anasema muungano wa sasa hauna faida kwa Zanzibar! Huu kama si mtindio wa ubongo ni ujinga uliotopea.
Kama muungano hauna faida kwanini usiondoke anataka mkataba tena!

Jokakuu hilo la kupokezana Urais Chadema wanalikana sasa hivi? real!

Mwanakijiji, Jasusi,
 
Nguruvi3,

..kwa kweli mimi nimekata tamaa na hili suala la muungano.

..naona vyama vyote vya siasa vimeamua kuunusuru kwa kupendekeza serikali tatu.

..kwa mtizamo wangu naona bora hata hayo mapendekezo ya Maalim Seif kwasababu yanatoa nafasi kwa Tanganyika kujitoa wakati wowote ule.

..ila pendekezo la CDM la kupokezana Uraisi wa muungano, kwa kweli limeniacha hoi.
 
Last edited by a moderator:

Chadema hawana ground katika masuala ya katiba. Udhaifu wao ni kuogopa kuudhi mtu au watu. Si unaona jinsi walivyoitwa Ikulu, baada ya kunywa chai they have nothing, absolutely nothing to say!

Mimi nina matumaini sana na hali ya baadaye kwasababu muungano unafikia kikomo.
Maalim anataka kiti UN, na katika vitu anavyotaka viwe vya muungano ni ulinzi na usalama. Sioni ni jinsi gani kila upande utaridhika na hapo ndipo nasema twende EAC.

Safari ya huko nayo ina matatizo, Seif hataki kwenda peke yake anataka akienda huko amebebwa kiaina.
All in all hakuna common ground which is fair kwangu kwasababu Tanganyika haiihitaji ZNZ kwa lolote.
 
Kitila Mkumbo,

..kuna summary ya mapendekezo ya katiba yaliyotolewa na CDM.

..soma kipengele # 6 kuhusu raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.

[/COLOR][/B][/B]
cc: Nguruvi3, Nonda
[/FONT][/I][/FONT][/COLOR]

Hii ni kama Rais wa JMT hatakuwa mkuu wa serikali bali mkuu wa nchi tu, yaani atakuwa ceremonial president kama ilivyo Ufaransa, Israel, n.k. Ikibaki kama ilivyo hakuna kitu kama hicho. Proposal ya CDM ni kuwa na two executives kwa Zanzibara na Tanganyika, then non executive president wa JMT. Ikiwa hivyo sioni tatizo la rotation.
 
Je huu ufafanuzi uliotoa hapa haukinzani na pendekezo nambari 4 la CHADEMA?
Au hata pendekezo namba 3? link https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-ya-tanganyika-na-zanzibar-6.html#post5479024
 
Hii ni kama Rais wa JMT hatakuwa mkuu wa serikali bali mkuu wa nchi tu, yaani atakuwa ceremonial president kama ilivyo Ufaransa, Israel, n.k. Ikibaki kama ilivyo hakuna kitu kama hicho. Proposal ya CDM ni kuwa na two executives kwa Zanzibara na Tanganyika, then non executive president wa JMT. Ikiwa hivyo sioni tatizo la rotation.
Kitila Mkumbo,

..lakini hapo kwenye kipengele # 4 CDM wanaelekeza kwamba Raisi wa muungano ni mkuu wa serikali ya muungano, mkuu wa nchi, na amiri jeshi mkuu. mimi sina ujuzi na mambo ya katiba, lakini naona kama huyo Raisi ni zaidi ya "ceremonial president."

..ni sababu zipi zimewafanya muone kwamba Uraisi wa muungano unapaswa kuwa wa zamu kati ya ZNZ na TGK, badala ya kuwa ni haki ya raia yeyote yule wa Tanzania mwenye vigezo vya kupiga na kupigiwa kura?

..zaidi, CDM mmeelekeza kwamba kutakuwa na URAIA ni suala la muungano. kwa msingi huo hakutakuwa na raia wa Tanganyika, au raia wa Zanzibar. Je, hamuoni utata hapo kuhusu suala la kupokezana Uraisi??

..Lengo haswa la pendekezo hili ni nini??

cc: Mzee Mwanakijiji, Jasusi, Kiranga, Nguruvi3
 
Brilliant!
Jokakuu CDM labda watueleze kama kuna ceremonial president, tunahitaji wa nini? Kwanini kila nchi isiende kivyake.
Kuna umuhimu gani wa kuwa na rais asiye na kazi kwasababu ceremonial ni kuwa hana executive power! why do we need that kind of person.

Halafu tumuulizae Kitila kuwa kama kuna rotation ya urais, vipi suala la wagombea binafsi wanaliweka katika mizani gani.
 
Nguruvi3,

..There is something I don't understand here.

..Raisi akiwa ndiye mkuu wa serikali, mkuu wa nchi, and commander in chief, bado anaweza kuwa "ceremonial president"?

..halafu na hiyo issue ya WAGOMBEA BINAFSI ndiyo inazidi kuchanganya akili.

cc😡Kitila Mkumbo
 
Huwezi kuwa ceremonial president halafu uwe commander in chief. Nchini Israel commander in chief ni prime minister.
Halafu tutambue kwamba Zanzibar hawana jeshi. Lazima wajue hilo. Wataongozaje jeshi la nchi nyingine? Chadema katika hili naomba mjipange upya.
 
Linapokuja nani ataongoza serikali ya Tanzania(muungano), mimi Nonda naona kuna mantiki kwa wanaosema iwe ni kwa kupokezana baina ya Rais wa Tanganyika na Rais wa Zanzibar/ mtanganyika na Mzanzibari.

Kushindwa kwetu kutofautisha baina ya serikali ya Muungano na serikali ya Tanganyika ndio inayotuletea kuandika vitu vya ajabu.

Tanzania (muungano) kama itakuwepo basi naungana na mawazo ya mambo 7 ya muungano, rafiki yako seif ameweka mambo 4.

Zanzibar ni kisehemu tu kama Mafia au Ukerewe sioni ni kwa nini tupate tabu ya kukiachia ili tupate kushughulikia mahitaji ya watu milioni 43.6
Sasa kama Zanzibar ni kisehemu tu kama Mafia na Ukerewe kwa nini unapoteza nguvu kujaribu kufikiria jinsi ya kugawana madaraka ya urais, mamlaka, n.k. na kakisiwa kama Ukerewe?

Hapo ndio huwa nashindwa kuelewa kabisa, kana nini hako kakisiwa? Tanganyika kuna kitu wanavuna kutoka Zanzibar, haiwezekani kabisa Watanganyika wakasema Zanzibar ni kama Mafia au Ukerewe halafu ukapoteza miaka 50 ya national attention kwenye swala la Muungano na "Ukerewe." Haiwezekani. Aidha Watanganyika wana siri kubwa, kuna visima vya mafuta vya siri Zanzibar vinavyo support Tanzania, au vinginevyo sisi Watanganyika tuna turkey stuffing vichwani. Haiwezekani kabisa kabisa!
 
Pendekezo la kupokezana urais simply halina mantiki. Tukichukulia suala la uwiano tu basi Zanzibar tayari imeshapata nafasi nyingi za ama urais au umakamu tangu muungano na hakuna maeneo mengine ya Tanzania ambayo yamepata nafasi hiyo. Tukikubali na kama ilivyo sasa kuwa lazima makamu atoke upande mwingine wa Muungano basi Zanzibar inapendelewa kupita kiasi.

Kwanini tusiseme tu kama ilivyo Marekani kuwa Rais na Makamu wasitoke Mkoa mmoja - haijalishi kama mkoa huo uko bara au visiwani?
 
Back
Top Bottom