#COVID19 CDC imeshauri watu kuachana na chanjo ya J&J kwani inasababisha kuganda kwa damu kwenye ubongo, watumie Moderna ama Pfizer

msifikiri tunapendwa sana aliwahi sema mzee mmoja mfupi wa Chato
 
Mkuu haya masuala ya chanjo ni very sensitive, unapoyafungulia uzi kama hivi jitahidi uwe na taarifa nyingi na za uhakika.

Mimi nilichanjwa mwezi wa saba mpaka leo ni miezi mitano imepita sijakutana na hiyo habari ya kuganda kwa damu.

Rais Samia alichanjwa hii hii Johnson mpaka leo anadunda mikoani akifanya kazi kama kawaida.
 
Tokea Corona ije duniani nime amini kua Tanzania hatuna vyuo bali tuna Secondary zinazo jiita vyuo. Hakuna tafiti. Kazi kusifia chanjo za Wazungu.

Ana bahati huyo Mama hakuchoma J&J ali igiza!!
 
Samia alichanjwa vipi bila bomba la Sindano kuvuta dawa? Ali igiza tu.
 
Ndio maana nimekuwa slow sana kufanya maamuzi baada ya kuchoma J&J
Duh kwa hiyo wanatusaidiaje.... Maana sisi tunawategemea wao... Wasitufanyie hivyo

Huu ndio unyama sasa
Batch ya kwanza ya J&J ya 1.3 millioni imekwisha Tanzania na hakuna madhara yaliyo ripotiwa, acha hofu
 
Sasa watatufidiaje, maana walitulazimisha kuchanja hyo j&j. tunataka fidia!
 
Wazungu hata kama tunawachukia lakini wao sio wajinga kiasi hicho eti watoe chanjo ambayo hawana uhakika nayo tena wanawapa na RAIA wao, nakataa never on earth hawawezi wakafanya ujinga huo !!
Hakuna anayemchukia mzungu. Lakini hatupaswi kuwa wapumbavu kwamba basi kila jambo linalotoka kwao basi ndio sahihi, kila wanachokisema ni kweli na kila wanachokifanya tuige. Ni kwa vile tu hawa wenzetu wamejaliwa economic muscles na PR machine ya kulazimisha kila ajenda yao, kila wazo lao na kila utashi wao upenye kotekote duniani. Hata hivyo tunashukuru tu Mungu kumjalia kila mtu akili yake binafsi na utashi wake binafsi wa kuamua kuchambua mbivu ni ipi na mbichi ni ipi. Ila wanapofika hata kutaka kumlazimisha mtu afanye watakavyo wao hata kwa nguvu hapo patachimbika.
 
Ninyi mnaodunda mkuu ni vijana MNA nguvu mko fit lakini wazee na wenye magonjwa sugu ndio wahanga wa huu ugonjwa !!
Hujasikia Marekani wanachanja hadi watoto? Kwa nini, kwa sababu baadhi ya watoto wao wameonekana kuathirika na covid. Huku kwetu sina uhakika sana kama kuna watoto nao wamefikwa na covid. Maana kuna namna ambavyo covid imeathiri watu kwa namna tofauti kidemographia na kijiografia. Kwa mfano nchi za kiafrika hazijaathirika sana na covid ukilinganisha na kwingineko. You can't say kwamba nchi zetu hizi zinaunderestimate actual cases kwa vile hatupimi au kuregister vifo inavyostahili. Maana hata South Africa wanakopima na kuregister vifo kama wanavyofanya Ulaya total cases za vifo tangu corona ianze haijafika hata laki moja. Lakini ukisikia walioshikilia remote wanavyozungumzia kuhusu chanjo ya corona utabaki kushangaa. Utadhani yaani bila chanjo kufika Afrika basi tunakufa na tutakufa kama inzi wafavyo.

Yaani hapa la msingi ni kutambua ajenda halisi ya kilicho nyuma ya pazia: yaani ni kuteka fikra za watu wote duniani na kuwatazamisha na kututumainisha kwamba maisha na future ya binadamu itategemea ufumbuzi utakaotokana na elimu yao, maarifa yao, teknolojia yao na dawa zao kutoka Marekani na Ulaya. Huo mfumo hasa ukiwa mtu unayejitambua ni mfumo hatari na haukubaliki. Ni utumwa pure version 2.
 
Acha kumfariji na kujifariji,hiyo Ni slow process,wait you will see
 
Usijifarishi,kitengo kikubwa Cha kuidhinisha matumizi ya dawa kimesema inasababisha damu kuganda wewe unakuja kujifariji kupitia koment ya mtu asiye na utaalamu.

Hii inaenda taratibu,siyo Leo Wala kesho ,but wait
 
Acheni blah blah toeni ushahidi wa kisayansi, mwenzenu Gwajima askofu alishindwa kutoa ushahidi wa kisayansi mpaka Leo ametulia TULIIII !!
Wewe subiri ,sijui sayansi Wala kienyeji utazijua Mara baada ya kuanza kuona madhara ya hizi chanjo,my friend naona hofu imekujaa sana
 
Ndio maana nakufahamisha haya kwa sababu nimeshafanya utafiti wa kutosha na nimejiridhisha kuwa chanjo haina madhara kabisa, isipokuwa kwa baadhi ya watu wachache sana ambao wanaweza kupata side effect kidogo tu
Utafiti gani wewe mtanzania wa mabwepande umefanya,hata kutengeneza barakoa umeshindwa Leo hii ujifanye mtaalamu wa kuchunguza vilivyotenezwa na mabeberu,

Huku kijijini kwangu hivi karibuni Kuna mwalimu kastaafu na kupewa mafao yake,ili ayale vizuri akaenda kuchanja J&J,Leo hii warithi wake wanayafaidi huku yeye tumesha mwimbia barapanda litalia

Endelea na utafiti wako
 
Tatizo ni kwamba uongo huwa unaenea na kukubaliwa haraka sana kuliko ukweli, hata hiyo bado watakataa tu kwa kuwa walishalishwa matango pori !!
Umetumwa kuja kutetea huu upuuzi kwa kutumia huo utafiti wako?
 
Sio kweli takwimu zako
Waliochanjwa Kwa J&J ni 7m
Walionyesha kudhuruwa Kwa kuganda damu ni 5079
Kati ya hao 98 wameng'oa
Waliobaki hapo wameachwa na magonjwa ya yatakayowaua polepole hakuna haraka

Umechu
Sio kweli takwimu zako
Waliochanjwa Kwa J&J ni 7m
Walionyesha kudhuruwa Kwa kuganda damu ni 5079
Kati ya hao 98 wameng'oa
Waliobaki hapo wameachwa na magonjwa ya yatakayowaua polepole hakuna haraka



Hiyo ni mpaka Aug kwa USA pekee ilikuwa 14 MπŸ‘† Najua naloongea nipo kwenye helthcare hapa US
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…