Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tatizo ni kwamba uongo huwa unaenea na kukubaliwa haraka sana kuliko ukweli, hata hiyo bado watakataa tu kwa kuwa walishalishwa matango pori !!Pfizer na Moderna wapo kwenye vita kubwa ya kuchumi na JANSSEN (J&J)
WHO wametoka kuipitia juzi hapa huiyo J&J na kuikubali kabisa iendelee kutumika . soma hap: Interim recommendations for the use of the Janssen Ad26.COV2.S (COVID-19) vaccine
Mkuu haya masuala ya chanjo ni very sensitive, unapoyafungulia uzi kama hivi jitahidi uwe na taarifa nyingi na za uhakika.Taasisi ya kudhibiti magonjwa ya Marekani, CDC imeshauri watu kupata chanjo za Pfizer ama Moderna kuliko J&J.
CDC imefikia uamuzi huo baada ya kushauriwa na wataalamu wa afya kwamba hizo chanjo ni salama zaidi kuliko J&J.
Sababu kubwa ya kupendekeza hivyo ni kwamba J&J inasababisha matatizo ya kuganda kwa damu kwenye ubongo hivyo watu waiepuke kadri inavyowezekana.
CDC wamesema kama mtu atataka mwenyewe kwa sababu zake mwenyewe chanjo ya J&J basi apewe ila zaidi watu watumie hizo chanjo mbili za Moderna na Pfizer.
![]()
Everything to know about Johnson & Johnson's COVID vaccine
A booster shot means a second shot for those who got J&J, but people living in San Francisco can get a third.www.cnet.com
Samia alichanjwa vipi bila bomba la Sindano kuvuta dawa? Ali igiza tu.Mkuu haya masuala ya chanjo ni very sensitive, unapoyafungulia uzi kama hivi jitahidi uwe na taarifa nyingi na za uhakika.
Mimi nilichanjwa mwezi wa saba mpaka leo ni miezi mitano imepita sijakutana na hiyo habari ya kuganda kwa damu.
Rais Samia alichanjwa hii hii Johnson mpaka leo anadunda mikoani akifanya kazi kama kawaida.
Batch ya kwanza ya J&J ya 1.3 millioni imekwisha Tanzania na hakuna madhara yaliyo ripotiwa, acha hofuNdio maana nimekuwa slow sana kufanya maamuzi baada ya kuchoma J&J
Duh kwa hiyo wanatusaidiaje.... Maana sisi tunawategemea wao... Wasitufanyie hivyo
Huu ndio unyama sasa
J&j ni chanjo salama, Usidanganyike ndugu !!Sasa watatufidiaje, maana walitulazimisha kuchanja hyo j&j. tunataka fidia!
Hakuna anayemchukia mzungu. Lakini hatupaswi kuwa wapumbavu kwamba basi kila jambo linalotoka kwao basi ndio sahihi, kila wanachokisema ni kweli na kila wanachokifanya tuige. Ni kwa vile tu hawa wenzetu wamejaliwa economic muscles na PR machine ya kulazimisha kila ajenda yao, kila wazo lao na kila utashi wao upenye kotekote duniani. Hata hivyo tunashukuru tu Mungu kumjalia kila mtu akili yake binafsi na utashi wake binafsi wa kuamua kuchambua mbivu ni ipi na mbichi ni ipi. Ila wanapofika hata kutaka kumlazimisha mtu afanye watakavyo wao hata kwa nguvu hapo patachimbika.Wazungu hata kama tunawachukia lakini wao sio wajinga kiasi hicho eti watoe chanjo ambayo hawana uhakika nayo tena wanawapa na RAIA wao, nakataa never on earth hawawezi wakafanya ujinga huo !!
Hujasikia Marekani wanachanja hadi watoto? Kwa nini, kwa sababu baadhi ya watoto wao wameonekana kuathirika na covid. Huku kwetu sina uhakika sana kama kuna watoto nao wamefikwa na covid. Maana kuna namna ambavyo covid imeathiri watu kwa namna tofauti kidemographia na kijiografia. Kwa mfano nchi za kiafrika hazijaathirika sana na covid ukilinganisha na kwingineko. You can't say kwamba nchi zetu hizi zinaunderestimate actual cases kwa vile hatupimi au kuregister vifo inavyostahili. Maana hata South Africa wanakopima na kuregister vifo kama wanavyofanya Ulaya total cases za vifo tangu corona ianze haijafika hata laki moja. Lakini ukisikia walioshikilia remote wanavyozungumzia kuhusu chanjo ya corona utabaki kushangaa. Utadhani yaani bila chanjo kufika Afrika basi tunakufa na tutakufa kama inzi wafavyo.Ninyi mnaodunda mkuu ni vijana MNA nguvu mko fit lakini wazee na wenye magonjwa sugu ndio wahanga wa huu ugonjwa !!
Acha mchecheto wewe. Ukifa, Mungu ndio kapanga ufe.Duh natoa wosia sasa tukifa waliokua wanashadadia wawajibike.
Acha kumfariji na kujifariji,hiyo Ni slow process,wait you will seeWala usiwe na wasiwasi hakuna shida yeyote, Mimi nimechanja na ndugu zangu wengi tu wamechanja tena wa umri tofauti tangu ilipoingia hiyo chanjo hakuna shida yeyote tuliyopata wala kusikia tatizo lolote kutoka kwa watu wengine waliochanja, MTU anaweza akafa kwa matatizo mengine lakini watu wakazusha eti kafa kwa sababu ya chanjo, USIAMINI FAKE NEWS ! WANASEMAGA LIES SPREAD FASTER THAN THE TRUTH !!
Usijifarishi,kitengo kikubwa Cha kuidhinisha matumizi ya dawa kimesema inasababisha damu kuganda wewe unakuja kujifariji kupitia koment ya mtu asiye na utaalamu.Shukrani!
Siku nimetoka Kuchanja, nikawahi kurudi nyumbani....
Nikaanza kusubiri kuumwa kichwa, mapigo ya moyo kwenda mbio, Uchovu Kama ambavyo nilisoma post kadhaa za watu waliosema wamechanja..,
But Sikusikia kichwa kuuma, Wala Uchovu, sikuhisi shida yoyote mpaka sasa!
Wewe subiri ,sijui sayansi Wala kienyeji utazijua Mara baada ya kuanza kuona madhara ya hizi chanjo,my friend naona hofu imekujaa sanaAcheni blah blah toeni ushahidi wa kisayansi, mwenzenu Gwajima askofu alishindwa kutoa ushahidi wa kisayansi mpaka Leo ametulia TULIIII !!
Utafiti gani wewe mtanzania wa mabwepande umefanya,hata kutengeneza barakoa umeshindwa Leo hii ujifanye mtaalamu wa kuchunguza vilivyotenezwa na mabeberu,Ndio maana nakufahamisha haya kwa sababu nimeshafanya utafiti wa kutosha na nimejiridhisha kuwa chanjo haina madhara kabisa, isipokuwa kwa baadhi ya watu wachache sana ambao wanaweza kupata side effect kidogo tu
Umetumwa kuja kutetea huu upuuzi kwa kutumia huo utafiti wako?Tatizo ni kwamba uongo huwa unaenea na kukubaliwa haraka sana kuliko ukweli, hata hiyo bado watakataa tu kwa kuwa walishalishwa matango pori !!
Sio kweli takwimu zako
Waliochanjwa Kwa J&J ni 7m
Walionyesha kudhuruwa Kwa kuganda damu ni 5079
Kati ya hao 98 wameng'oa
Waliobaki hapo wameachwa na magonjwa ya yatakayowaua polepole hakuna haraka
Sio kweli takwimu zako
Waliochanjwa Kwa J&J ni 7m
Walionyesha kudhuruwa Kwa kuganda damu ni 5079
Kati ya hao 98 wameng'oa
Waliobaki hapo wameachwa na magonjwa ya yatakayowaua polepole hakuna haraka