Hivi nani aliamua kuwa ukivaa gwanda unakuwa mnyama?
Mbona wajeda duniani tunapishana nao kama hawapo vile
Na raia wamezidi woga pia
Kuna siku kashuka mwanajeshi kwenye lorry, fala mmoja akaropoka ooh huyo peke yake anaweza akawapiga watu 10 tena bila silaha
Nilibaki nacheka tu na kusononeka pamoja
Yaani wamekuwa SAS sasa
Yaani dereva daa
Acheni kuwapa vichwa hao
Mkuu wa majeshi atoe tamko ni marufuku mjeda kwenda kupiga raia kisa kavaa gwanda na marufuku kuitana kisa mmoja wao kalewa au kazidiwa kete na dume kwa mwanamke halafu anaenda analia kambini na kuja na battalion kama wanaingia vitani