CDF Mkunda apongeza Shirika la Mzinga lililo chini ya ya JWTZ kwa kuanzisha mradi wa kokoto

CDF Mkunda apongeza Shirika la Mzinga lililo chini ya ya JWTZ kwa kuanzisha mradi wa kokoto

kyagata

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2016
Posts
13,966
Reaction score
26,220
Wakati wenzetu marekani wameanzisha jeshi la anga za juu yani us space force.
Sisi lijeshi letu bado liko karne ya 5 huko.eti cdf anafurahia mradi wa kokoto,serious?

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF), Jenerali Jacob Mkunda, amelipongeza Shirika la Mzinga lililo chini ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kuanzisha mradi wa Kokoto mkoa wa Arusha uliopo chini ya kampuni tanzu ya shirika hilo.

Akizungumza wakati wa uwekaji wa jiwe la Msingi leo Mei 03, 2025 la mradi huo uliopo eneo la Nanja Wilayani Monduli Jenerali Mkunda amewataka wasimamizi wa mradi huo kuwa makini na kutanguliza maslahi ya shirika na kuuendesha kwa faida mradi huo wa kimkakati ili uwe shamba darasa kwa miradi mingine.

Akitoa taarifa ya mradi huo Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo, Luteni Jenerali Samwel Ndomba (Mstaafu) amemhakikishia CDF Mkunda kuwa mradi huo utasimamiwa kwa umakini sana ili uwe na tija na kuchangia uchumi wa Taifa.

Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa Shirika hilo, Brigedia Jenerali Seif Athumani Hamisi amesema mitambo katika mradi huo iliyofungwa ni ya kisasa na itakuwa na uwezo wa kuzalisha Kokoto tani mia tatu (300) kwa saa moja.

Screenshot_20250503_205457_Opera Mini.jpg
 
Hivi tunavyolalamika, kukosoa na kudogosha kila kilichochetu huwa tunategemea nani abadilishe tunavyolalamikia na kudogosha!!!
 
Ujenzi ni muhimu,tusijifanye tuko mbali kama wao,bado sana.
 
kuna aina ya maisha wabongo wanaish as if wako peke yao dunaniani😅😅😂😂
Yaaani anajisifia kabisa mradi wa kokoto wakati Jeshi la Ethiopia limefungua mradi wa kiwanda cha kutengeneza drones.

Kazi za kufanywa na Wawekezaji wa Kitanzania kuongeza mzunguzo wa pesa kwa Wananchi ndo wanajisikia kuzifanya. Kazi zao za msingi kwa Ulinzi wa Taifa letu katika dunia ya Sayansi ya Teknolojia hawazifanyi.

Ujinga ni kipaji Tanzania.
 
Hivi tunavyolalamika, kukosoa na kudogosha kila kilichochetu huwa tunategemea nani abadilishe tunavyolalamikia na kudogosha!!!
Mkuu samahani.
Mimi pia hii nimeiona kwenye taarifa ya habari, nikajiuliza kwani ni lazima kila idara ifanye biashara?
Katika nchi ambayo karibu kila kitu ndani ya jeshi kinatoka nje, hivi crusher inaongeza nini kwenye security ya nchi?
 
Back
Top Bottom