CDF Mkunda apongeza Shirika la Mzinga lililo chini ya ya JWTZ kwa kuanzisha mradi wa kokoto

Hivi tunavyolalamika, kukosoa na kudogosha kila kilichochetu huwa tunategemea nani abadilishe tunavyolalamikia na kudogosha!!!
Mkuu..kwa Karne hii huwezi kujivunia jeshi kutengeneza kokoto...mabadiliko yanawezekana vzuri tu tatizo mifumo imekaliwa na watu wajinga ambao wapo Tyr kuchukua maisha ya yeyote anaeitakia nchi hii mabadiliko chanya(positive)...
 
Kwahiyo huoni tatizo hapo jeshi kufungua miradi ya kokoto..!
Ninachojua Jeshi lina miradi mingi huo ukiwa ni mmoja wapo...
Ipo miradi ya kilimo (mbogamboga, matunda, mahindi, maharage)

Ipo miradi ya ujenzi inasimamiwa na suma jkt

Miradi ya tofali.

Ipo miradi ya muziki ikiwemo live bands

Bar, guests, hostels nk.

Kuna miradi ya shule (makongo nk)

Kuna miradi ya ufugaji (kuku, kware, ng'ombe nk)

Siioni unashangaa nini kuhusu kokoto ........

NB.

Hakuna Jeshi Tz lisilo na miradi labda zimamoto na uhamiaji. TISS Ndo usiseme wana hadi maduka ya rejareja na vibanda vya popcon.
 
Idara ya investment jeshini kwetu hawajafanya majukumu yao kwa usahihi. Investment zao ni kokoto,frame, maduka ya vinywaji nk. Pamoja na kua na maeneo ya muhimu sana ya ya kibiashara lakini wanaishia kujenga frame tu. Mfano Kawe pale Lugalo, Maji chumvi nk.
Kwenye nchi za wenzetu technology nyingi zinavumbuliwa majeshini. Yani huko ndio kuna vichwa. Huku kwetu nadhani mifumo bado haijakaa sawa
 
Ninachojua Jeshi lina miradi mingi huo ukiwa ni mmoja wapo...
Ipo miradi ya kilimo (mbogamboga, matunda, mahindi, maharage)

Ipo miradi ya ujenzi inasimamiwa na suma jkt

Miradi ya tofali.

Ipo miradi ya muziki ikiwemo live bands

Bar, guests, hostels nk.

Kuna miradi ya shule (makongo nk)

Kuna miradi ya ufugaji (kuku, kware, ng'ombe nk)

Siioni unashangaa nini kuhusu kokoto ........

NB.

Hakuna Jeshi Tz lisilo na miradi labda zimamoto na uhamiaji. TISS Ndo usiseme wana hadi maduka ya rejareja na vibanda vya popcon.
Kwahiyo ww unaona wapo sawa Jeshi la wananchi (JWTZ) kuinvest kwenye hizo petty businesses kwenye Karne hii ya 21.
 
Kwenye nchi za wenzetu technology nyingi zinavumbuliwa majeshini. Yani huko ndio kuna vichwa. Huku kwetu nadhani mifumo bado haijakaa sawa
Asilimia kubwa ya jeshi ni form IV & VI leavers inategemea nn sasa..!?
 
Wakati wenzetu marekani wameanzisha jeshi la anga za juu yani us space force.
Sisi lijeshi letu bado liko karne ya 5 huko.eti cdf anafurahia mradi wa kokoto,serious?

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF), Jenerali Jacob Mkunda, amelipongeza Shirika la Mzinga lililo chini ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kuanzisha mradi wa Kokoto mkoa wa Arusha uliopo chini ya kampuni tanzu ya shirika hilo.

Akizungumza wakati wa uwekaji wa jiwe la Msingi leo Mei 03, 2025 la mradi huo uliopo eneo la Nanja Wilayani Monduli Jenerali Mkunda amewataka wasimamizi wa mradi huo kuwa makini na kutanguliza maslahi ya shirika na kuuendesha kwa faida mradi huo wa kimkakati ili uwe shamba darasa kwa miradi mingine.

Akitoa taarifa ya mradi huo Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo, Luteni Jenerali Samwel Ndomba (Mstaafu) amemhakikishia CDF Mkunda kuwa mradi huo utasimamiwa kwa umakini sana ili uwe na tija na kuchangia uchumi wa Taifa.

Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa Shirika hilo, Brigedia Jenerali Seif Athumani Hamisi amesema mitambo katika mradi huo iliyofungwa ni ya kisasa na itakuwa na uwezo wa kuzalisha Kokoto tani mia tatu (300) kwa saa moja.

View attachment 3323848
Mi mwanzoni nikajua SUMA-JKT!
 
Hawa hswa wanajeshi wa mzinga wanaokata mabomu yaliyokwisha muda na kuuza kama screpa! Aisee hivi yule mkuu wa kambi amesalimika kweli?
 
Ndiyo uwezo ,akili zao zilipoishia
Kutoka maframa,kumbe za kukodi harusi,kuuza kokoto

Ova
 
Wakati wenzetu marekani wameanzisha jeshi la anga za juu yani us space force.
Sisi lijeshi letu bado liko karne ya 5 huko.eti cdf anafurahia mradi wa kokoto,serious?

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF), Jenerali Jacob Mkunda, amelipongeza Shirika la Mzinga lililo chini ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa kuanzisha mradi wa Kokoto mkoa wa Arusha uliopo chini ya kampuni tanzu ya shirika hilo.

Akizungumza wakati wa uwekaji wa jiwe la Msingi leo Mei 03, 2025 la mradi huo uliopo eneo la Nanja Wilayani Monduli Jenerali Mkunda amewataka wasimamizi wa mradi huo kuwa makini na kutanguliza maslahi ya shirika na kuuendesha kwa faida mradi huo wa kimkakati ili uwe shamba darasa kwa miradi mingine.

Akitoa taarifa ya mradi huo Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo, Luteni Jenerali Samwel Ndomba (Mstaafu) amemhakikishia CDF Mkunda kuwa mradi huo utasimamiwa kwa umakini sana ili uwe na tija na kuchangia uchumi wa Taifa.

Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa Shirika hilo, Brigedia Jenerali Seif Athumani Hamisi amesema mitambo katika mradi huo iliyofungwa ni ya kisasa na itakuwa na uwezo wa kuzalisha Kokoto tani mia tatu (300) kwa saa moja.

View attachment 3323848
Kokoto? na mitambo imetoka China hizi ndio akili za Waafrica
 
Magufuri alimpiga marufuku bakresa kuuza mandazi na vitumbua, kwa maana hiyo ni kazi ya akina mama wa chini yeye auze ngano tu

Sasa hawa wavunja matofari wao wanakuja kuingilia kazi ya mahustle, wapambanaji wa kitaa

Hii siyo poa
 
Back
Top Bottom