Hii nchi tuna shida sana, UDSM tu pale kuna maprofessor sio chini ya 100!! Ila tatizo la maji halina ufumbuzi mpaka leo. Unakuta wanajua changamoto ila wakuongea nani? Hakuna wa kusolve? Yote ili kulinda vyeo tu alafu wakitoka ndio wanaanza kueleza changamoto!!
Hii nchi sijui tumerogwa
Huu ni mjadala unaohitaji kujadiliwa kwa kina; lakini najuwa JF siku hizi haya mambo hayana nafasi mbali ya kuwa machawa, n.k.
Lakini labda kwa kifupi tu nami nichangie nikitofautiana kidogo na lawama zinakoelekezwa; kwa mfano kwa hao maProfesa wa UDSM.
Nitakupa mfano wa China, ambako ndiko CCM yetu imeundwa kwa kutumia 'model' ya Communist Party ya China.
Communist Party ya China nayo ingegeuka na kuwa kama ilivyo CCM siku hizi, nakuhakikishia taifa hilo lingekuwa tofauti sana na lilivyo leo.
Kwenye miaka ya nyuma kidogo; ukitazama yaliyosimamiwa na CCM; hata huko kwenye vyuo vikuu yaliwafikia, na jitihada zilifanyika hata hao ma-profesa unaowasema leo walijipanga kutimiza hata kwenye mazingira magumu sana ya kiuchumi na mengineyo.
Kwa hiyo, moyo na juhudi hata huko kwenye vyuo yalikuwepo. Huko kwenye kitivo cha engineering, mipango ilikuwepo..
CCM ilipoanza kulegea na kufanya siasa kuwa mtaji wa watu kunufaika nao kibinafsi; maprofesa hao hao ndio wakawa mstari wa mbele kutafuta fursa; kwa sababu siasa ndiyo ilikuwa inalipa.
Na kwa kweli siyo huko vyuoni tu, ambako wahusika walikatishwa tamaa ya kuwa wajenzi wa taifa hili. Ni nani asiyejuwa juhudi za wafanyakazi wa TRC kuunda na kufufua mabehewa yaliyokuwa yametelekezwa.
COSTEC ilianzishwa kusimamia na kuongoza juhudi za wabunifu wa taifa hili. Nyumbu, magari yalitengenezwa.
Kwa hiyo tunaweza kusema mipango na moyo wa kuyafanya mambo haya toka awali vilikuwepo. Mazingira ya hali ya kiuchumi, siyo Tanzania pekee ni mchango mkubwa uliosambaratisha juhudi hizo; lakini kubwa ya yote, ni mabadiliko yaliyoikumba CCM; ikatoka kwenye msimamo wake kama ule wa 'model' ya kichina, na kuwa chama cha chukua chako mapema.
Samia mapema kabisa alipoingia, kaenda China kukutana na Xi JinPing; kaambiwa wachina wanao uhitaji mkubwa sana wa Soya kila mwaka; mwanamke karudi hapa na humsikii hata akikumbuka alichoambiwa kule; ila rahisi zaidi ni kugawa Bandari za Tanganyika na kugawa Gesi na raslimali nyinginezo ambazo mTanzania mkulima wa Ruvuma manufaa yake kama yapo, ni baada ya akina Nchemba madilu kuweka mabasi yao barabarani!
Na sasa CCM (kasha), limetuvusha hadi kuondoa uhai wa waTanzania ili hao hao akina Madilu. KabutiKalamaganda na Samia wao wabaki madarakani!
Mabeyo namsikitikia sana. Pamoja na "msamaha" anaoomba, yeye mwenyewe moyoni mwake atakuwa anajilaumu sana; pamoja na kwamba aliyofanya yalikuwa ni kufuata utaratibu unaoeleweka.
Maneno yake ni mazuri sana, na mimi naamini tukipata viongozi wenye utashi; hayo aliyoyaelezea ni mambo yanayotekelezeka vizuri kabisa.
Kamwe siwezi kuikatia tamaa Tanzania. 'Prospcts' zake ni nzuri sana.