Kwa kipindi hiki cha kwanza timu zote mbili zimecheza zikiwa na tension.....Uoga mwingi na butua butua nyingi......
Beki ya Simba imeonekana kutulia wakati wote kuanzia mwanzo wa mchezo mpaka dakika ya 45....Kwa upande wa Yanga wao beki yao ilionekana kutokuelewana katika dakika 25 za mwanzo......baada ya hapo ilitulia na kuanza kucheza vizuri,Nsajigwa bado hajatulia,anaonekana kuikamia sana mechi,hope atabadilika 2nd half..
Kwa upande wa kiungo Simba walianza vizuri sana wakiwa na Mwinyi Kazimoto lakini baada ya Mwinyi kuumia na kutoka na kuingia Mohammed Banka kiungo kimepooza na kuwaacha Yanga waanze kuelewana pale kati,Banka inabidi abadilike pale kati....Kiungo cha Yanga kimeanza kuelewna baada ya kutoka Kazimoto.....Juma Seif na Nurudin Bakari wanaelewana vizuri pale kati japo hawajacheza mpira wa kuvutia..
Kwa upande wa safu ya ushambuliaji ya Simba bado ipo butu,Simba hawana washambuliaji kabisa....Mussa Hassan,Haruna Moshi,Shija Mkina na Ulimboka Mwakinge wamepooza sana kule mbele,ni wazembe,hawawezi kumalizia...Simba wangekuwa na safu nzuri ya ushambuliaji wangeweza hata kufunga magoli matatu half hii ya kwanza.......Kwa upande wa Yanga nao licha ya kuwa na safu nzuri ya ushambuliaji ya Mwape,Hamis Kiiza,Taita na Tegete nao wameshindwa kufunga,hawajaleta kashikashi langoni mwa Simba....
Ngoja tuangalie kipindi cha pili ambacho kinaanza sasa...