CECAFA KAGAME CUP 2011 Finals in Tanzania

CECAFA KAGAME CUP 2011 Finals in Tanzania

Bila kumsahau mtangazaji Ahmed Jongo!
Mh unanikumbusha mbali sana. Nawakumbuka Yanga hii.1. Sahau Kambi2. Fredy Felex Minziro3. Keneth Mkapa4. Godwin Aswile 5. Salum Kabunda Ninja6. Isa Adhuman 7. Thomas kipese8. Athumani China9. Justine Ntekele10. Sanifu lazaro Tingisha11. Edibili Lunyamila
 
Asanteni wadau kwa updates, ila leo BUNDI kalala JANGWANI..........

Leo Yanga akishinda ntashangaa, kwa kweli Simba leo wameupiga mno, Yanga wangu sijui wamechoka? Wako wazito na hawafiki mbele kabisa! Kazi tunayo wana kandambili!
 
natafakari msukumo uliopo sasa hivi wa soka uwanja mzuri ungewakuta enzi zile akina ramadhani lenny hussein aman masha edward chumila malota soma masatu george mwameja lunyamila mohamed hussein fundi method mogella ken mkapa HAMIS THOBIAS GAGARINO nadhani tungekuwa km nigeria.
Malota Soma "Ball zozo",
 
Leo Yanga akishinda ntashangaa, kwa kweli Simba leo wameupiga mno, Yanga wangu sijui wamechoka? Wako wazito na hawafiki mbele kabisa! Kazi tunayo wana kandambili!
Shida ya SIMBA ni pumzi.....watulie na kupata ushindi mapema, vinginevyo katika dakika 30 za nyongeza MAGAMBA watatutundika goli......
 
Kwa kipindi hiki cha kwanza timu zote mbili zimecheza zikiwa na tension.....Uoga mwingi na butua butua nyingi......

Beki ya Simba imeonekana kutulia wakati wote kuanzia mwanzo wa mchezo mpaka dakika ya 45....Kwa upande wa Yanga wao beki yao ilionekana kutokuelewana katika dakika 25 za mwanzo......baada ya hapo ilitulia na kuanza kucheza vizuri,Nsajigwa bado hajatulia,anaonekana kuikamia sana mechi,hope atabadilika 2nd half..

Kwa upande wa kiungo Simba walianza vizuri sana wakiwa na Mwinyi Kazimoto lakini baada ya Mwinyi kuumia na kutoka na kuingia Mohammed Banka kiungo kimepooza na kuwaacha Yanga waanze kuelewana pale kati,Banka inabidi abadilike pale kati....Kiungo cha Yanga kimeanza kuelewna baada ya kutoka Kazimoto.....Juma Seif na Nurudin Bakari wanaelewana vizuri pale kati japo hawajacheza mpira wa kuvutia..

Kwa upande wa safu ya ushambuliaji ya Simba bado ipo butu,Simba hawana washambuliaji kabisa....Mussa Hassan,Haruna Moshi,Shija Mkina na Ulimboka Mwakinge wamepooza sana kule mbele,ni wazembe,hawawezi kumalizia...Simba wangekuwa na safu nzuri ya ushambuliaji wangeweza hata kufunga magoli matatu half hii ya kwanza.......Kwa upande wa Yanga nao licha ya kuwa na safu nzuri ya ushambuliaji ya Mwape,Hamis Kiiza,Taita na Tegete nao wameshindwa kufunga,hawajaleta kashikashi langoni mwa Simba....

Ngoja tuangalie kipindi cha pili ambacho kinaanza sasa...
 
Wew sio shabiki wa yanga usingesema hayoo,tutashinda tu
leo yanga akishinda ntashangaa, kwa kweli simba leo wameupiga mno, yanga wangu sijui wamechoka? Wako wazito na hawafiki mbele kabisa! Kazi tunayo wana kandambili!
 
Leo Yanga akishinda ntashangaa, kwa kweli Simba leo wameupiga mno, Yanga wangu sijui wamechoka? Wako wazito na hawafiki mbele kabisa! Kazi tunayo wana kandambili!

Simba wamecheza dakika 25 za mwanzo.....Baada ya hapo walionesha kupooza hasa katikam safu ya kiungo baada ya kuumia kwa Mwinyi Kazimoto....Ngoja tuone kipindi hiki cha pili
 
Mbona wote wanapiga piga tu hapa, waweke mpira chini na waanze kucheza mpira
 
Sina wasiwasi na vijana wa dar yng african.huko msimbazi waanda jeneza
 
Mpira bado ni butua butua tu.......

Hakuna ile ladha ya mpira kabisa
 
Back
Top Bottom