CGTN documentary ni channel bora kabisa kwa nchi za kiafrika na kwa waafrika

CGTN documentary ni channel bora kabisa kwa nchi za kiafrika na kwa waafrika

Naipenda sana sana halafu hata kama hujalipia kingamuzi cha DStv wanaonyesha Bure kabisa
Kama sijakosea ni channel 348
 
Naipenda sana sana halafu hata kama hujalipia kingamuzi cha DStv wanaonyesha Bure kabisa
Kama sijakosea ni channel 348
Bora huko DSTV bure startimes usipo lipia haupati kitu.

Ni hiyo channel inayo lazimisha king'amuzi kilipiwe na National Geography na International news channels bila hivyo hata king'amuzi sifikiri kama kitatumika.

Ila ni Channel bora napenda kuitizama mara kwa mara
 
Mimi siagalia ule upuu wa Domo anasema , anachukua anaweka waa , nyoka anateleza anaingia shimoni
 
CGTN ni bonge la channel. Nilianza na CCTV sasa nimeongeza CGTN
Kumbe wadau mpo wengi.

Kuna hizi programmes:-
  • China Mega Projects
  • Travelogue
  • China's war on poverty
  • Remarkable construction
  • Kuna nyengine inahusu harakati zao za uhuru, mahangaiko na mateso waliyopitia mpaka kupata uhuru na mpaka sasa walipo jina limenitoka kidogo

Jamaa wapo vizuri sana
 
Mimi siagalia ule upuu wa Domo anasema , anachukua anaweka waa , nyoka anateleza anaingia shimoni
😀 Wasanii wa bongo wanachangamoto kweli ngoma zao sio za kusikiliza mbele ya kadamnasi.
 
Usipozibwa ukweli na propaganda za vyombo vya Magharibi hizi programmes zitakusaidia kujua kwa nini China imeibuka kuwa taifa lenye uchumi mkubwa

Wengi wamedangwanywa kuwa China isingekuwa hapo bila uwekezaji wa West. Ila zile documentaries zinaonyesha wazi jamaa walikuwa na long plan kufikia walipo sasa
Nakubaliana na wewe.

Namna wanavyo set mipango yao unaona kabisa wanaplan wawe wapi na kwa muda gani mfano kupambana na umasikini waliset kabisa goals kwa mwaka gani wanatakiwa wawe wameishinda poverty line na kweli wakaingia mzigoni serious mpaka wakafanikisha.

Sasa hivi wame set mipango kwenye clean energy na wanapambana kweli watimize malengo yao nafuatilia mara kwa mara programme hii.

Ila wanakutana na challenges nyingi kwenye construction za madaraja maana China milima mingi balaa ila haiwazuii kufanya maajabu.
 
Na hapa kwa sasa Mchina hana mpinzani mfano kwenye photovoltaic technology na EV kwa ajili ya clean energy
Ni kweli kwenye solar ana kimbiza na huko kwenye EV napo ana kimbiza hawa jamaa kile chama chao ni kama kipo mbele ya muda hata kuhusu chips ni kama walishtukia mipango ya U.S mapema wakaanza kujiwekeza ndani na sasa wana ongeza uwekezaji na R&D sio muda mrefu napo wataanza kukimbiza huko.

Hawa jamaa na kile chama chao na serikali yao wapo mbele ya muda
 
Hii mashine imevumbuliwa China inaitwa iron monster imefanya waweze kujenga madaraja kwa haraka na kutandaza reli
View attachment 2773909

Na hii ni kwa ajili ya kuchimba mahandaki inaitwa shield tunneling machine
View attachment 2773915

Hizi mashine zimesaidia kwenye ujenzi haraka wa reli na madarajalicha ya kuwa China baadhi ya maeneo ina milima mingi

Hawa jamaa ni wachapa kazi sana
Daah! Hizi mashine nimeziona sana kwenye programmes zao kwenye construction katika kuchimba tunnels.

Hiyo kitu ya kuchimba mahandaki sio poa inapiga kazi mpaka miamba inanyooka.

Hilo goma la kutandaza reli hatari linavyo tembea toka sehemu moja mpaka nyingi mpaka HSR ina kamilika inastahajabishana sana.

Kuna ujenzi pia wa hydroelectric power kule napo wanafanya maajabu huwa natazama nabaki kushangaa tu hawa jamaa walipo
 
project ya umeme solar

Only in China

20231006_214639.jpg


20231006_214653.jpg


20231006_214718.jpg
 
Mtoa mada alivoweka bandiko mchana ikabidi niwashe tv kuzama kwenye channel nimeona wapo katika project ya umeme solar, uwanja wa kuenea viwanja vya soka 8000 wamezaja masolar pannels za kutosha, hapo kwenye EV ana magari makali ya umeme

ndo maana kwenye mambo ya rushwa hawana utani wanakufyeka kwelikweli
Kitu pekee nilicho gundua kuhusu hawa jamaa ile ishi ya ukoloni na kutawaliwa ndani ya nchi yao inawauma sana hawataki kabisa kurudia makosa.

Serikali na wananchi wote kwa pamoja historia ya humiliation ni kama inawakumbusha kujenga China bora ndio maana mpaka leo chuki waliyo nayo wachina wengi dhidi ya Japan ni kubwa balaa.

Sisi huku ni kama historia ya ukoloni na utumwa haituumizi ili tusirudie makosa ya kuwa dhaifu na kuweza kufanyiwa humiliation.

Historia ya dunia na viumbe hai inasema ukiwa dhaifu ni lazima ugandamizwe na wenye nguvu hii kitu kwetu haija kaa vizuri katika vichwa vya watu ndio maana possibility kubwa kuwekwa utumwani tena sisi tunayo kwa sababu ni dhaifu mpaka sasa
 
Back
Top Bottom