Chacha Maboto, Mbunge wa Bunda (CCM): Lugha ya kwenye Mkataba wa DP World sikuielewa, mnisamehe

Unaweza kuwa hujui,KATIBA MBOVU ndio kiini cha yote haya yanayotendeka leo
Katiba wanabadilisha tu hawa mbwa hata iwe nzuri kiasi gani, mbona sasa wanataka kubadilisha sheria za umiliki wa ardhi watashindwa kubadilisha wanachokitaka?
 
"kushindwa kuwawakilisha vyema kwa kutokujua kilichoandikwa"
Yaani anawawakilisha wana kanisa? Ndio anawaomba radhi? Kwani ndio waliomchagua? Hii mpya
 
"kushindwa kuwawakilisha vyema kwa kutokujua kilichoandikwa"
Yaani anawawakilisha wana kanisa? Ndio anawaomba radhi? Kwani ndio waliomchagua? Hii mpya
Muhishimiwa Gama kwani ukishakuwa Mwana kanisa unapoteza sifa ya kuwa Raia wa Tanzania? kwa kuweza kupiga kura maana Raia wakiompigia kura miomgoni mwao wapo kanisani au na hilo nahitaji kuanza kutoa notes uelewe?
 
Ndiyo maana mambo kama haya wabunge wanatakiwa wapewe siku nyingi kabla waende wakasome vizuri, wakaombe ushauri na ufafanuzi kwa watu wenye ujuzi wa mambo husika.
Kama jambo la kisheria wakaombe kwa wanasheria, kitabibu waende kwa daktari, kiuchumi waende kwa wachumi, n.k.
Wakishapata kuelewa vizuri ndipo wakapigie kura bungeni.
 
Doh hii ngoma imebuma *****

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa samahani yake itabadirisha nini🤔🤔 si unafki huo 😡😡 kama hakuelewa kwa nini aliupigia kura ya ndio au ndicho kilichompeleka pale🤔🤔 huyo ni mnafki tuu
 
Nilisikia mwanamama mmoja mbunge alipoongea muda ukaisha akaambiwa "...unga mkono hoja..." Akaunga akibabaika.

Kwahiyo, ukiacha kutopewa muda bado wanashinikizwa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Arejeshe na posho aliyochukua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…