Chacha Maboto, Mbunge wa Bunda (CCM): Lugha ya kwenye Mkataba wa DP World sikuielewa, mnisamehe

Mbunge wa Bunda Mh.Robert Mabotto akiri mbele ya kanisa leo Mbele ya Padri baada ya padri kumaliza kusoma Waraka wa TEC kuwa hakuelewa chochote kuhusu mkataba huo kwani lugha iliyotumika ilikuwa Ni ngumu kwake kuielewa hivyo alipiga tu kura kutimiza wajibu wake...
Mbali na hilo amechukua nafasi hiyo kuomba radhi kwa Padri na waumini wote kanisani kwa kushindwa kuwawakilisha vyema kwa kutokujua kilichoandikwa

Kipande cha Video hapa chini angalia....
View attachment 2723007
Kwamba hata pesa aliyopewa Kwa bahasha hakujua ni ya nini!!
 
Ndo maana mimi naona kuna haja ya kuangalia vipengele vya namna jinsi gani wabunge wanapatikana. Maana elimu ni muhimu na maarifa ni muhimu zaidi
Tatizo sio usomi tatizo kukosekana kwa uzalendo;
 
Lakini amekiri kutokujua kilichoandikwa na kama yeye kakiri bhasi huenda wapo wengi ambao hawakuelewa pia WASAMEHEWE
Tusisahau, sifa ya kuwa mbunge hapa Tanzania ni kujua kusoma na kuandika na usiwe chini ya la saba..!!! Sasa la saba wetu wa shule ya msingi Nanguruwe unategemea ajuwe kiingereza kilichoandikwa kwenye mkataba wa DPW na Tanzania?
 
Mbunge wa Bunda Mh.Robert Mabotto akiri mbele ya kanisa leo Mbele ya Padri baada ya padri kumaliza kusoma Waraka wa TEC kuwa hakuelewa chochote kuhusu mkataba huo kwani lugha iliyotumika ilikuwa Ni ngumu kwake kuielewa hivyo alipiga tu kura kutimiza wajibu wake...
Mbali na hilo amechukua nafasi hiyo kuomba radhi kwa Padri na waumini wote kanisani kwa kushindwa kuwawakilisha vyema kwa kutokujua kilichoandikwa

Kipande cha Video hapa chini angalia....
View attachment 2723007
Asante Mungu, Maneno ya Mwabukusi yametimia, wamekiri kwamba hawakujua walicho pitisha.
 
Huyo maboto ndio mmilikiwa Ile taasisi ya mikopo umiza inayoitwa maboto finance? Au ni majina tu
 
Mbunge wa Bunda Mh.Robert Mabotto akiri mbele ya kanisa leo Mbele ya Padri baada ya padri kumaliza kusoma Waraka wa TEC kuwa hakuelewa chochote kuhusu mkataba huo kwani lugha iliyotumika ilikuwa Ni ngumu kwake kuielewa hivyo alipiga tu kura kutimiza wajibu wake...
Mbali na hilo amechukua nafasi hiyo kuomba radhi kwa Padri na waumini wote kanisani kwa kushindwa kuwawakilisha vyema kwa kutokujua kilichoandikwa

Kipande cha Video hapa chini angalia....
View attachment 2723007
Huyu atatimuliwa kesho asubuhi
 
Ubunge imekuwa ni biashara badala ya uwakilishi wa kweli wa wananchi.
Rushwa na gharama kubwa kwenye uchaguzi inathibitisha hilo.
Ili kupata uwakilishi wa kweli wa wananchi, wabunge wawe watu wa kujitolea kwa gharama sawa na watumishi waandamizi wa serikali.
Pili, sifa iwe uwezo wa kujenga hoja, ushirikiano, uelewa wa jamii na eneo analowakilisha.
 
Back
Top Bottom