Chacha Maboto, Mbunge wa Bunda (CCM): Lugha ya kwenye Mkataba wa DP World sikuielewa, mnisamehe

Chacha Maboto, Mbunge wa Bunda (CCM): Lugha ya kwenye Mkataba wa DP World sikuielewa, mnisamehe

Tusisahau, sifa ya kuwa mbunge hapa Tanzania ni kujua kusoma na kuandika na usiwe chini ya la saba..!!! Sasa la saba wetu wa shule ya msingi Nanguruwe unategemea ajuwe kiingereza kilichoandikwa kwenye mkataba wa DPW na Tanzania?
Kumbuka maneno ya mbunge aliyekuwa wa ccm ndugu Ole Medei kuwa wabunge wote wa ccm huwa wanaandikiwa nini cha kuongea
 
Ubunge imekuwa ni biashara badala ya uwakilishi wa kweli wa wananchi.
Rushwa na gharama kubwa kwenye uchaguzi inathibitisha hilo.
Ili kupata uwakilishi wa kweli wa wananchi, wabunge wawe watu wa kujitolea kwa gharama sawa na watumishi waandamizi wa serikali.
Pili, sifa iwe uwezo wa kujenga hoja, ushirikiano, uelewa wa jamii na eneo analowakilisha.
Mishahara na posho zishuke kwa 70%
 
Mbunge wa Bunda Mh.Robert Mabotto akiri mbele ya kanisa leo Mbele ya Padri baada ya padri kumaliza kusoma Waraka wa TEC kuwa hakuelewa chochote kuhusu mkataba huo kwani lugha iliyotumika ilikuwa Ni ngumu kwake kuielewa hivyo alipiga tu kura kutimiza wajibu wake...
Mbali na hilo amechukua nafasi hiyo kuomba radhi kwa Padri na waumini wote kanisani kwa kushindwa kuwawakilisha vyema kwa kutokujua kilichoandikwa

Kipande cha Video hapa chini angalia....
View attachment 2723007
Aahaaaaa
 
Wangekuwa wanaelewa tusingekuwa na mikataba ya hovyo kama iliyopo.
Wataelewaje wakati Spika aliwapitishia vimemo toka kwa M/K Taifa wa chama chao kabla ya mkataba wenyewe?.

Suala la mkataba wa Bandari wakulaumiwa ni watu watu:
1. Mwenyekiti wa CCM Taifa
1. Mwanasheria Mkuu wa Serikali
3. Spika wa Bunge la JM wa Tanzania.
 
Bora kukaa kimya, anajiabisha zaidi, unagombeaje ubunge kama lugha rasmi hujui?
Kwani kujua Kiingereza ni kigezo cha kugombea ubunge?!
Ninachojua ili uwe mbunge sharti ujue kusoma na kuandika. Na bahati nzuri au mbaya haijainishwa ujue kusoma na kuandika lugha ipi!
 
Katiba wanabadilisha tu hawa mbwa hata iwe nzuri kiasi gani, mbona sasa wanataka kubadilisha sheria za umiliki wa ardhi watashindwa kubadilisha wanachokitaka?
Katiba itatupa fursa ya kuwang'oa CCM madarakani
 
Kwani kujua Kiingereza ni kigezo cha kugombea ubunge?!
Ninachojua ili uwe mbunge sharti ujue kusoma na kuandika. Na bahati nzuri au mbaya haijainishwa ujue kusoma na kuandika lugha ipi!
Wabunge wa ccm n majanga
 
Mswaada na mkataba ulikuwa kwa Kingereza??
 
Kuna watu humu hamna hekima. Mnamshambulia wa nini wakati yeye kaelezea ukweli ulivyo??? Wanasheria wa bunge wapo na wao walielimishwa mkataba hauna shida. Na tunasema haina gogoro kabisa.
Mbunge anatakiwa awe na staffs wake na wanasheria wake mwenyewe binafsi.
 
Back
Top Bottom