Chacha: Nani asiyejua kuwa Viongozi wote na Dola ni Mali ya CCM?

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Idara ya Oganaizesheni, Paul Chacha, ametangaza hadharani kuwa vyombo vyote vya dola na viongozi wa serikali ni mali halali ya CCM kwa kuwa chama hicho ndicho kilichowaweka madarakani.

Akizungumza leo, Jumamosi, Septemba 26, 2026, katika mkutano maalumu wa CCM Mkoa wa Iringa uliojadili maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa chama hicho mwaka 2027 na maadhimisho ya miaka 50 ya CCM, Chacha amewajibu kwa ukali wakosoaji na vyama vya upinzani vinavyohoji umiliki wa dola na utaratibu wa CCM kuwasomba wananchi kwenye mikutano yao.

Chacha amesisitiza kuwa CCM haitaacha utaratibu wake wa kukodi mabasi, kuwasomba wanachama na kuwapatia posho pindi wanapohudhuria mikutano ya chama hicho kote nchini. "Nani hajui kuwa dola ni mali ya CCM!?

Vyombo vya dola na viongozi wa serikali ni mali ya CCM kwa sababu ni chama hiki ndicho kilichowaweka katika nafasi hizo. Kuhusu madai ya upinzani kwamba tunasomba watu, tutaendelea kuwasomba kwa mabasi na kuwapa posho," amesema Paul Chacha.

Kauli hiyo imezua gumzo kubwa katika uwanja wa siasa nchini, huku wachambuzi wa masuala ya kisheria na kikatiba wakitafsiri kauli hiyo kama msimamo unaoonyesha wazi mtazamo wa chama tawala kuelekea uchaguzi wa ndani na maandalizi ya uchaguzi mkuu.

Ndio maana tunasema katiba mpya ni ya lazima.

Chini ya katiba mpya vilaza kama hawa hawatakua na uwezo wa kuropoka ujinga na kuvunja sheria hovyo.

Nchi itaendeshwa kwa sheria mama ambayo ni katiba na mtu akivunja sheria atachukuliwa hatua bila kujali ana cheo gani.
 
Chacha yuko sahihi 100%
ni CCM pekee ndio chama pekee cha siasa chenye malengo ya kukamata dola, kuunda serikali, kuongoza nchi, kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo waTanzania.

Vyama vingine vya siasa nchini Tanzania, malengo yao ni kuchochea chuki, kuleta fujo, uharibifu, ghasia na maafa pekee 🐒
 
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Idara ya Oganaizesheni, Paul Chacha, ametangaza hadharani kuwa vyombo vyote vya dola na viongozi wa serikali ni mali halali ya CCM kwa kuwa chama hicho ndicho kilichowaweka madarakani.

Akizungumza leo, Jumamosi, Septemba 26, 2026, katika mkutano maalumu wa CCM Mkoa wa Iringa uliojadili maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa chama hicho mwaka 2027 na maadhimisho ya miaka 50 ya CCM, Chacha amewajibu kwa ukali wakosoaji na vyama vya upinzani vinavyohoji umiliki wa dola na utaratibu wa CCM kuwasomba wananchi kwenye mikutano yao.

Chacha amesisitiza kuwa CCM haitaacha utaratibu wake wa kukodi mabasi, kuwasomba wanachama na kuwapatia posho pindi wanapohudhuria mikutano ya chama hicho kote nchini. "Nani hajui kuwa dola ni mali ya CCM!?

Vyombo vya dola na viongozi wa serikali ni mali ya CCM kwa sababu ni chama hiki ndicho kilichowaweka katika nafasi hizo. Kuhusu madai ya upinzani kwamba tunasomba watu, tutaendelea kuwasomba kwa mabasi na kuwapa posho," amesema Paul Chacha.

Kauli hiyo imezua gumzo kubwa katika uwanja wa siasa nchini, huku wachambuzi wa masuala ya kisheria na kikatiba wakitafsiri kauli hiyo kama msimamo unaoonyesha wazi mtazamo wa chama tawala kuelekea uchaguzi wa ndani na maandalizi ya uchaguzi mkuu.

View attachment 3678443
 
Attachments

  • 6405188-8fd715c9093808790118fec3dd5983a7.mp4
    15.6 MB
  • 6403529-6f253ec74c59a615dfdc6041e21e7142.mp4
    11.6 MB
Back
Top Bottom