Chacha: Nani asiyejua kuwa Viongozi wote na Dola ni Mali ya CCM?

Chacha: Nani asiyejua kuwa Viongozi wote na Dola ni Mali ya CCM?

Chacha yuko sahihi 100%
ni CCM pekee ndio chama pekee cha siasa chenye malengo ya kukamata dola, kuunda serikali, kuongoza nchi, kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo waTanzania.

Vyama vingine vya siasa nchini Tanzania, malengo yao ni kuchochea chuki, kuleta fujo, uharibifu, ghasia na maarifa pekee 🐒
Sawa
 
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Idara ya Oganaizesheni, Paul Chacha, ametangaza hadharani kuwa vyombo vyote vya dola na viongozi wa serikali ni mali halali ya CCM kwa kuwa chama hicho ndicho kilichowaweka madarakani.

Akizungumza leo, Jumamosi, Septemba 26, 2026, katika mkutano maalumu wa CCM Mkoa wa Iringa uliojadili maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa chama hicho mwaka 2027 na maadhimisho ya miaka 50 ya CCM, Chacha amewajibu kwa ukali wakosoaji na vyama vya upinzani vinavyohoji umiliki wa dola na utaratibu wa CCM kuwasomba wananchi kwenye mikutano yao.

Chacha amesisitiza kuwa CCM haitaacha utaratibu wake wa kukodi mabasi, kuwasomba wanachama na kuwapatia posho pindi wanapohudhuria mikutano ya chama hicho kote nchini. "Nani hajui kuwa dola ni mali ya CCM!?

Vyombo vya dola na viongozi wa serikali ni mali ya CCM kwa sababu ni chama hiki ndicho kilichowaweka katika nafasi hizo. Kuhusu madai ya upinzani kwamba tunasomba watu, tutaendelea kuwasomba kwa mabasi na kuwapa posho," amesema Paul Chacha.

Kauli hiyo imezua gumzo kubwa katika uwanja wa siasa nchini, huku wachambuzi wa masuala ya kisheria na kikatiba wakitafsiri kauli hiyo kama msimamo unaoonyesha wazi mtazamo wa chama tawala kuelekea uchaguzi wa ndani na maandalizi ya uchaguzi mkuu.

View attachment 3678443
 
Attachments

  • 6405188-8fd715c9093808790118fec3dd5983a7.mp4
    15.6 MB
Kwa hiyo, si sahihi kimfumo kusema kwamba kila mwananchi ni CCM. Uanachama wa chama ni jambo tofauti na uraia. Katiba pia inalinda uhuru wa mtu kujiunga na chama au jumuiya, na hairuhusu mtu kulazimishwa kujiunga na chama.
 
Si kila mwananchi ni mwanachama wa CCM. Tanzania ina mfumo wa vyama vingi vya siasa, hivyo uraia wa Mtanzania hauhitaji kuwa mwanachama wa CCM.
 
Majaji, mahakimu, Mwanasheria mkuu wa Serikali, Waziri mkuu, wakuu wa mikoa,wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa Halmashauri ,usalama wa Taifa, mapolisi, magereza, Rais ni mali ya CCM sio mali ya Watanzania! Je ni kila mwananchi ni CCM?
 
Duh kumbe vyama vya siasa vinaweza kumiliki vyombo vya ulinzi...kwa hiyo ccm inaweza kuchukua bunduki za wanajeshi na polisi na kuzitumia, kwa sababu ni mali za chama ?
 
Duh kumbe vyama vya siasa vinaweza kumiliki vyombo vya ulinzi...kwa hiyo ccm inaweza kuchukua bunduki za wanajeshi na polisi na kuzitumia, kwa sababu ni mali za chama ?
Ndio! Tatizo ni muundo wa CCM ,aliouweka Nyerere kuwa Rais awe Mwenyekiti wa Chama.
 
Chacha yuko sahihi 100%
ni CCM pekee ndio chama pekee cha siasa chenye malengo ya kukamata dola, kuunda serikali, kuongoza nchi, kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo waTanzania.

Vyama vingine vya siasa nchini Tanzania, malengo yao ni kuchochea chuki, kuleta fujo, uharibifu, ghasia na maarifa pekee 🐒
Vyama vingine vya siasa nchini Tanzania, malengo yao ni kuchochea chuki, kuleta fujo, uharibifu, ghasia na maarifa pekee 🐒
(haujakosea kuandika hapo).
 
Vyama vingine vya siasa nchini Tanzania, malengo yao ni kuchochea chuki, kuleta fujo, uharibifu, ghasia na maarifa pekee 🐒
(haujakosea kuandika hapo).
kama chama chako cha siasa hakina malengo, ya kushiriki wala kushinda uchaguzi, kukamata dola au kuunda serikali, kuongoza nchi na kuwatumikia wananchi,

hiyo chama ni useless kabisa gentleman,
waambie na wenzako kuhusu hili na itapendeza zaidi 🐒
 
Angalia maneno yaliyokolezwa, umeyaandika mwenyewe acha kurukaruka.
 
Back
Top Bottom