Chacha: Nani asiyejua kuwa Viongozi wote na Dola ni Mali ya CCM?

Chacha: Nani asiyejua kuwa Viongozi wote na Dola ni Mali ya CCM?

Vyama vingine vya siasa nchini Tanzania, malengo yao ni kuchochea chuki, kuleta fujo, uharibifu, ghasia na maarifa pekee šŸ’
(haujakosea kuandika hapo).

kama chama chako cha siasa hakina malengo, ya kushiriki wala kushinda uchaguzi, kukamata dola au kuunda serikali, kuongoza nchi na kuwatumikia wananchi,

hiyo chama ni useless kabisa gentleman,
waambie na wenzako kuhusu hili na itapendeza zaidi šŸ’
Unarukaruka nini angalia ulichoandika mwenyewe kwanza.
 
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Idara ya Oganaizesheni, Paul Chacha, ametangaza hadharani kuwa vyombo vyote vya dola na viongozi wa serikali ni mali halali ya CCM kwa kuwa chama hicho ndicho kilichowaweka madarakani.

Akizungumza leo, Jumamosi, Septemba 26, 2026, katika mkutano maalumu wa CCM Mkoa wa Iringa uliojadili maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa chama hicho mwaka 2027 na maadhimisho ya miaka 50 ya CCM, Chacha amewajibu kwa ukali wakosoaji na vyama vya upinzani vinavyohoji umiliki wa dola na utaratibu wa CCM kuwasomba wananchi kwenye mikutano yao.

Chacha amesisitiza kuwa CCM haitaacha utaratibu wake wa kukodi mabasi, kuwasomba wanachama na kuwapatia posho pindi wanapohudhuria mikutano ya chama hicho kote nchini. "Nani hajui kuwa dola ni mali ya CCM!?

Vyombo vya dola na viongozi wa serikali ni mali ya CCM kwa sababu ni chama hiki ndicho kilichowaweka katika nafasi hizo. Kuhusu madai ya upinzani kwamba tunasomba watu, tutaendelea kuwasomba kwa mabasi na kuwapa posho," amesema Paul Chacha.

Kauli hiyo imezua gumzo kubwa katika uwanja wa siasa nchini, huku wachambuzi wa masuala ya kisheria na kikatiba wakitafsiri kauli hiyo kama msimamo unaoonyesha wazi mtazamo wa chama tawala kuelekea uchaguzi wa ndani na maandalizi ya uchaguzi mkuu.

View attachment 3678443
Mbona wanaogopa michakato huru ya kiuchaguzi? Yaani mbona wanawaogopa wananchi? Cha atazidi kukigharimu Chama, kauli za aina hiyo ndiyo hupelekea wansnchi kufanya uasi.
Kujisifu kwamba Jeshi, Polisi , Usalama wa taifa ni mali ya Chama (kwanza si kweli) hiyo ni matusi kwa Wananchi, huko ni kuwa mddle finger wananchi. Price kauli za hivi ni kubwa sana kuzilipa.
 
kuleta fujo
SASA MBONA MKIAMBIWA MAJAJI NA VYOMBO VYA DORA NI MACCM MNAKASIRIKA IKIWA MNAJUA SETIKALI YOTE NI MALI YA CHAMA CHA MAPINDUZI?? JE MKIITWA MADIKTETA NAPI MTAKASILIKA?? MAANA SERIKALI NI MALI YENU NA SINA UHAKIKA KAMA WATU WOTE WAPO KWENYE CHAMA CHA CCM SO HUON KAMA HUO NI UDIKTETA KUTAKA KUAMINISHA DUNIA KUWASERIKALI YOTE NI MALI YA CHA CHENU WAKAT KUNA MFUMO WA VYAMA VINGI?? BINAFSI SIDHAN KAMA NI SAHIHI MAANA KUNA WANACHAMA WA CHADEMA, ACT, CUF YAN WOTE AUTOMATICALLY MMEWAFANYA KUWA CCM?? BAS LISSU AKUKOSEA ALIVYOSEMA MAJAJI NA VYOMBO VYA DORA NI MACCM
 
acha porojo na upotoshaji gentleman,
mwenye mihemko na makasiriko ni wewe na wafuata mkumbo wenzako na si vinginevyo.

nadhani hili liko wazi kwa wadau wote wa JF šŸ’
 
Chama kinachoshabikia uvunjaji wa sheria na katiba, hapo amalizie na mahakama.
Ipo siku watatoka na kukiri mauaji ya mwaka jana...taratibu tu.
Sema CCM
 
Lilivyo halina akili sidhani kama linajua kailo kama hizi zinakoleza moto wananchi wazidi kudai katiba mpya.
 
Na mahakama ni zao pia.
Ikiwa Jaji/Majaji, Mwanasheria Mkuu pamoja na Msajili wa Mahakama wameteuliwa na M/Kiti wao nao ni mali ya CCM na nilazima watekeleze matakwa yao kwa kufuata ilani ya CCM na siyo Katiba ya Nchi. Wamekiri hadharani leo wenyewe.

Tukisema Mahakama zetu haziko huru tunatekwa na kupotezwa na hao hao wateule wa mwenyekiti wao.
 
Chacha yuko sahihi 100%
ni CCM pekee ndio chama pekee cha siasa chenye malengo ya kukamata dola, kuunda serikali, kuongoza nchi, kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo waTanzania.

Vyama vingine vya siasa nchini Tanzania, malengo yao ni kuchochea chuki, kuleta fujo, uharibifu, ghasia na maarifa pekee šŸ’
šŸ–
 
Huyu baba mnamkumbuka?
 
Attachments

  • 1788870522926.png
    1788870522926.png
    657.8 KB · Views: 9
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Idara ya Oganaizesheni, Paul Chacha,
Utamlaumu mtu kama huyu kwa jambo gani wakati anayosema ndiyo wanayoyaamini viongozi wote ndani ya hicho chama.

Umuhimu wa taarifa kama hizi ni kujuwa hali halisi ilivyo, na kusoma kwa usahihi mtazamo na mori unaojitokeza kwa watu waliomo ndani ya chumba hicho.
Hawa wote wamepewa hamasa ya kuendeleza utaratibu huo huo anaouzungumzia mwenza ili waendelee kunufaika wao.

Soma vizuri hiyo video jinsi wahusika wanavyoitikia taarifa hiyo.

Napendekeza video hii iwekwe mahali salama kama kumbukumbu za huko baadae.
CHADEMA wasikose kuiweka kwenye 'archive' yao, ni video muhimu sana hii.
 
..kwa hiyo mauaji ya OCT 29 yalifanywa na Ccm?

..Mwenyekiti wa Ccm anaepuka vipi lawama ktk mazingira kama haya?
Swali linabaki kuwa lilelile, ila sasa kuna 'urgency' ya kipekee kabisa:
Tutatokaje hapa!
 
Baada ya kukanusha muda mrefu kuhusu kusomba na ushahidi kuweka hadharani, hatimaye wameona bora wakiri tu hadharani kwani walikuwa wanaona aibu kuonekana ni hadi wasombe na kulipa watu.
Chacha yupo sahihi 100%
- Amethibitisha, wanasomba watu kwa magari. Jambo lililokanushwa miaka mingi
-Kwamba wanalipa posho (rushwa) wanaohudhuria mikutano. Sasa hakuna ubishi tena!
-Amekiri, vyombo vya dola ; JWTZ, Police, Usalama n.k. ni mali ya CCM. Ilifahamika, Chacha kathibitisha
-Kwamba, Watumishi wa Serikali wakiwemo Mawakili wa Serikali na Majaji ni mali ya dola. Lilijulikana muda tu

Chacha ni kiongozi amenyooka kwa maelezo !

Ahsante Chacha!

JokaKuu
 
..kwa hiyo mauaji ya OCT 29 yalifanywa na Ccm?

..Mwenyekiti wa Ccm anaepuka vipi lawama ktk mazingira kama haya?
Sasa mkuu si Chacha keshasema wanamiliki vyombo vya dola na serikali!
Mwenyekiti ni sehemu ya chama na Serikali, Chacha keshasema ndio wenye shughuli
 
Chacha yupo sahihi 100%
- Amethibitisha, wanasomba watu kwa magari. Jambo lililokanushwa miaka mingi
-Kwamba wanalipa posho (rushwa) wanaohudhuria mikutano. Sasa hakuna ubishi tena!
-Amekiri, vyombo vya dola ; JWTZ, Police, Usalama n.k. ni mali ya CCM. Ilifahamika, Chacha kathibitisha
-Kwamba, Watumishi wa Serikali wakiwemo Mawakili wa Serikali na Majaji ni mali ya dola. Lilijulikana muda tu

Chacha ni kiongozi amenyooka kwa maelezo !

Ahsante Chacha!

JokaKuu
Kasema ukweli
 
Back
Top Bottom