Uchaguzi 2020 CHADEMA, ACT Wazalendo vyapigwa marufuku kunadi wagombea wasio wa vyama vyao. Waambiwa kufanya hivyo ni kuwachanganya Wananchi

Siasa haitaki hasira.
Ni kama Mchezo wa riadha,wote mnakimbia mbio zilezile,lakini waweza kumkabidhi mwenzio kijiti amalize mbio!hauwezi kuuliza kwa nini,hakumaliza mbio wewe mwenyewe!
Hapa naona ni timu mbili zipo katika kinyang'anyiro,mwingine anaushawishi na Taasisi za Serikali na vyombo vya dola na mwingine hana fursa ya kushawishi wala kuvisimamia vyombo vya dola na taasisi za Serikali.!!
Hizi ni mbio aidha ukimbie mwenyewe hadi mwisho wa kamba au umpe kijiti mwingine mwenye pumzi ili afike mwisho(finishing line).
 
Watanzania hatuna misimamo katika maisha yetu. Yaani kazi za serikali pia zimekuwa za kujikomba kwa Jiwe. Siyo kwa merit tena. Yaani kila mtu yuko busy ili aonekane anamzidi mwezie kujikomba. Kwa kweli tunahitaji katiba mpya kuondokana na hali hii.
 
Mrema na Cheyo hawajasimamisha mgombea URAIS hivyo watampigia moja kwa moja MAGUFULI kwa sababu hawatamkuta mgombea URAIS wa TLP au wa UDP.
 
CHADEMA si walisema imefutika kwahiyo sasa wanasumbuka na mzimu tu
 
walikuwa wanaruhusiwa kukutana na wanachi? tuwe na kumbukumbu
 
Mbona jana yule kiongozi wa Tume alikua anamnadi mgombea fulani je sio kutuchanganya huko?
 
Sasa si asubiri aone kama wananchi aka wapiga kura watachaganya madesa.
Labda itawachanganya wale watoto wa shule wanaofika kwenye kampeni za CCM badala ya kukaa darasani na kusoma.
 
Naomba kuuliza Swali: kwa hivyo tumewaafikiana kwamba miaka 5 ya kwanza ya bwana magufuki , maisha ya wananchi hayajaboreshwa? Kwani alivyoomba Kura 2015, si alisema maisha ya wananchi yataboreshwa na tutakuwa Ulaya? Kama kashindwa awamu ya kwanza, kwanini apewe awamu ya pili?
 
Mrema hawajasimamisha mgombea wa URAIS kwa hiyo hategemei kuunda serikali.
Kwahio wakati wa Kampeni mgombea hawezi kuona kwamba hii kazi siiwezi/siitaki au fulani anaweza kuifanya vema kuliko mimi kwahio tumpe yeye...., kipi bora niendelee kuwaambia wananchi wanichague mimi wakati sitaki au niwaambie nani anafaa kuliko mimi?
 
Vyama vyote vyenye wagombea uraisi vinavyoacha kunadi wagombea wao na kunadi mgombea wa nyumba ya jirani

Mmebaki kuscreen shot post za watu na kuwawekea watu ambacho hawajaongea. Hiki ulichokiedit na kuniquote mimi, ni mimi ndio niliyesema? Mods huu mchezo wa kuedit post za watu na kuelekeza kwa watu wengine, unazidi kushika kasi hapa jukwaani, chukueni hatua.
 
Waliokuchagua ugombee kuanzia kamati kuu,halmashauri kuu na mkutano mkuu ina maana wote walikuwa akili hawana walipokuteua? Wewe uliyeteuliwa ndio una akili kubwa!??
 
Hata akinadiwa Nani Bora kuliko kumnadi mtu wa nje. Sheria za kipuuzi kweli
 
Uchaguzi uliopita TLP ilikuwa na mgombea wa Urais wa Tanzania lakini Mwenyekiti wao Mrema alitangaza kumuunga mkono Magufuli na alifanya hivyo.
NEC His Master's Voice.
 
Waliokuchagua ugombee kuanzia kamati kuu,halmashauri kuu na mkutano mkuu ina maana wote walikuwa akili hawana walipokuteua? Wewe uliyeteuliwa ndio una akili kubwa!??
Kwani wananchi wana akili ndogo ?, si wataamua wanachokiona siku ya siku...., yeye mgombea na Chama kinaona fulani anafaa iweje NEC ndio ilazimishe mtu apigiwe kura wakati yeye mwenyewe anaona vinginevyo?
 
Mrema alishafuata sheria ipi?
Mimi si mwana siasa
Tafadhali nijibu kutaalamu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…