Wakuu mkistaajabu ya tume ya uchaguzi basi jiandae kuona ya msajili.
Jana kumbe Sisty kuwahi kote huko na boda boda pale makao makuu ya Chadema ni kupeleka barua ya katazo kuwa kuwanadi wagombea wa nje ya vyama vyao ni kukiuka maadili ya uchaguzi hivyo wamepigwa marufuku.
Yani hii ofisi ya msajili imekuja na kituko cha aina yake!
===
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Sisty Nyahoza ahudhuria kipindi cha Clouds360 kinachoendeshwa na Clouds Media na kuongea masuala mbalimbali wakati huu nchi ikiwa inaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu.
Aidha, katika mahojiano hayo, Sisty aliulizwa kuhusu masuala mbalimbali ikiwamo suala zima la Vyama vya Siasa kuungana na kushirikiana katika uchaguzi.
Akitoa ufafanuzi wa kina kuhusu suala hili Mh. Sisty Nyahoza alisema “Vyama pekee vimewahi kuungana ni ASP na TANU viliungana ikawa CCM. Kilichofanyika 2015 kwa jina la UKAWA ule ni ushirikiano kwamba wote mnabakia mna status ya kisheria kama chama cha siasa halafu mnashirikiana kwenye shughuli za kisiasa”
Ameongeza kuwa "Kisiasa kuna ushirikiano wa aina mbili, wa kwanza ni Coalition mnashirikiana kwa malengo ya kushinda uchaguzi. Halafu kuna Alliance mnashirikiana katika mambo yanayojitokeza tu katika siasa halafu kila mmoja anaendelea na shughuli zake, Coalition imewekewa masharti”
“Ni vyema haya mambo ya ushirikiano vile vyama vinataka kushirikiana viingie mkataba wakubaliane sera zetu zitakuwa zipi, tutawekaje wagombea, tutaundaje Serikali, tutagawanaje vipi ruzuku. Baada ya hayo makubaliano wayalete kwa msajili wa vyama vya siasa”
“Waliokuwa wameshasema wanaunga mkono wa chama kingine wanachopaswa wanatakiwa wabakie kama walivyobakia baada ya uteuzi wa Wagombea, baada ya uteuzi wa wagombea Urais Agosti 25 hawawezi kuteua tena mgombea Urais”
Aidha akiweka bayana kuhusu ushirikiano unaofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo na ACT Wazalendo Sisty Nyahoza amesema “Wao (CHADEMA, ACT) hawapaswi kwenda hadharani na kumsapoti mgombea yule kwa sababu ukiwa unamnadi mgombea wa chama kingine na wewe una chama na sera zako, wananchi hawajui baada ya uchaguzi mtaunda Serikali moja au utatekeleza ya kwako. Mnawachanganya wananchi”-