PreGE2025 CHADEMA; baada ya tamko la kutoshiriki Uchaguzi Mkuu, fanyeni haya

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Kwa sababu wanaweza kujenga ma-mall halafu wasiwe wameisaidia jamii, kwani wafanyabiashara wa jamii za hali ya chini hawataweza kupanga.

Hapa kikubwa wazingatie ni mradi gani binafsi uwe mkubwa, wa kati au mdogo; unakwenda ku-suit eneo gani.
 
Nyie mmefeli..wapewe wengine wakifeli watapewa wengine pia...Hiyo ndo demokrasia..mkuu.
 
Nyie mmefeli..wapewe wengine wakifeli watapewa wengine pia...Hiyo ndo demokrasia..mkuu.
Zipo tuhuma nyingi sana zilizo za kweli na zisizo za kweli zinazowakabili CCM, lakini tuhuma hizi zimechangiwa ni vitu vingi;
  1. Ukubwa wa chama chenyewe
  2. Watu wengi zaidi maarufu, wenye hamasa au ushawishi kwa jamii kuwa upande wa CCM, mfano wasanii.
  3. Kujulikana kwa chama chenyewe mpaka kwenye maeneo ambayo yako interior sana hapa Tanzania; hivyo kwa vyama vyenye ushawishi mkubwa kwenye maeneo ya mijini tu wakishafanya uchunguzi wa hapa na pale wakagundua kuna baadhi ya maeneo wameongoza wanadhani basi ushindi ni wa kwao, hata matokeo yakitangazwa wanashtuka imekuwaje! Wameiba kura hawa! Haiwezekani! Wanasahau kuna maeneo huko hata Kiswahili wanakiongea kwa lafudhi zao, hawana internet, chama pekee wanachokijua na kukishabikia ni CCM na kura ni lazima wawapigie CCM. Ikumbukwe pia kuwa maeneo ya aina hii Tanzania ni makubwa zaidi pia.
Mimi ningependekeza uchaguzi huu wa mwaka 2025, kama huwa kuna watafiti kutoka Tanzania na mataifa mbalimbali, kama huwa kuna watu wanaofanya tathmini ya uchaguzi seriously kabisa basi waende maeneo ya vijijiniiiiii, vijiji vya kati na nje ya miji; waachane na kutafiti mijini ambako kumejaa watu wa Mitandao ya Kijamii.
 
Weken Tume Huru ya Uchaguzi...mbona waoga sana.
 
Wewe ni kichwa maji.
 
A reason to why nimependekeza vyama pinzani vya siasa navyo vijitengenezee relationship (guanxi) imara na watanzania mpaka wa maeneo ya vijijini sana; na hii ni kupitia kuanzisha miradi inayogusa mioyo ya jamii hizo; kwani jamii kama hizi huwezi ukatumia mitandao ya kijamii kuzifikia.
 
Weken Tume Huru ya Uchaguzi...mbona waoga sana.
Siku ya uchaguzi kafanyeni utafiti vijijini kwanza acheni maneno mengi; ili mje na utafiti ulio kamili, kwani hizi tafiti za viraka viraka ndizo zinawafanya mnadhani CCM ni wachawi kumbe ni woga wenu tu na hofu na mashaka.
 
Hapana mimi si kichwa maji, mimi ni Mtanzania mzalendo niliyeamua kusema ukweli kwa vyama vyetu vya siasa. Kwa atakayeukubali sawa na kwa atakayeukataa pia sawa.
Wewe kweli unaona tatizo ni vyama vya siasa au mfumo CCM, katiba mbovu na watawala wabovu? Afadhali ungesema tatizo ni wananchi wapole.
 
Wewe kweli unaona tatizo ni vyama vya siasa au mfumo CCM, katiba mbovu na watawala wabovu? Afadhali ungesema tatizo ni wananchi wapole.
Tatizo ni vyama vya siasa vimewekeza kwenye maneno makali, lugha zisizofaa, kuhamasisha vitendo hasi, n.k. wakidhani kuwa ndiyo njia ya kuchukua madaraka kutoka kwa CCM au wakidhani kuwa ndiyo njia ya kuwabadilisha CCM, katiba na mifumo ya utawala jambo ambalo ni BIG NO!

Siasa za vitendo chanya, tulivu, za hekima, kukubali maridhiano na za kuenenda kwa utaratibu ikiwemo kutogomea uchaguzi ili kupata nafasi za kugombea Ubunge na Udiwani hata chama kwa mfano CHADEMA wakipata nafasi kadhaa za ubunge; kule ndiko mahali sahihi pa kama kuna 'NO REFORM NO ELECTION' (kwa ajili ya chaguzi zijazo), kama kuna mifumo haiko sawa, kama kuna katiba, n.k. Bungeni ndiko jikoni.

Sasa wao wanakataa kugombea means hawautaki Ubunge wala Udiwani, halafu huku mitandaoni na huko mitaani wanachapisha 'NO REFORMS NO ELECTION' 'TUNATAKA KATIBA MPYA' 'CCM INA UTAWALA MBOVU' 'CCM INA MIFUMO MIBOVU' sasa unadhani wananchi wa kawaida wanaowaambia huku watawasidia nini? Sana sana watashabikia eee ndiyo! Tukinukishe! Ndiyoo! Halafu hatimaye ziiiiiiiiiiii kimya kimetawala, hakuna suluhu wala chochote kilichopatikana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…