Hawa CHADEMA naona hapo walipofika wamejisahau kabisa na anguko lao linakuja muda si mrefu na wakija wakishtuka itakuwa too late. Hakuna cha mwenye afadhali hapo Halima Mdee aliifanya nini CHADEMA mahakamni eti alikaa kimya kwa nini hakuutema ubunge feki. Je leo CHADEMA ikichukuwa nchi halafu apewe uwaziri si atauza nchi huyo. Huyo Msigwa naye mpaka akabebeshwa picha eti leo watu wanamtetea hapa. Yule Selasini ndio mafia kabisa alichomfanyia Mbatia kule NCCR leo hii kuna wapuuzi eti wamesahau. Huyo akipata cheo hapo CHADEMA mna uhakika gani kama hataofanya aliyoyafanya kule NCCR? Kwa kweli intelijinsia ya CHADEMA imekwisha na nina wasiwasi kuna mapandikizi yalibakizwa hapo wakati wenzao wanaenda CHAUMA. Haiwezekani CHADEMA ilivyokuwa "serious" kikamanda leo eti inawapokea wasiliti kimdebwedo kiasi hicho
Kwa upuuzi huu wa kukumbatia hao wasaliti ni bora tu CCM waendelee kutawala kwani afadhali ya zimwi likujualo. Kama wanashindwa kuvaa uso wa mbuzi wanaoneana aibu sasa hivi wakishika nchi si itakuwa balaa wataweza kweli kukemea mafisadi hawa. Hebu fikiria mpaka sasa hivi hakuna kiongozi wajuu aliyejitokeza kutoa taarifa kuhusu hawa viongozi wa zamani waliorudi na adhabu au utaratibu watakaopewa. Kumbuka hao waliorudi sio wanachama wa kawaida ni viongozi wa zamani waliokuwa ngazi ya juu. Maana yake kesho ukisikia Selasini au Msigwa kateuliwa/kachaguliwa kamati kuu usishtuke. Vipi wale makamanda wengine waliokuwa wanapambania nembo ya chama kwenye nyakati ngumu watajiskiaje? Kwa hili waliopo karibu na Heche na Mnyika wawakumbushe kuwa ule umati wanauona kwenye mikutano sio wajinga kama wao wanavyosemega kwenye mikutano kwa hiyo wasiruhusu upuuzi wowote ule. Hakuna mtu mwenye akili zake timamu atakubali kuona mtu aliyewaita wanachadema "wajinga" miezi michahce tu nyuma au ailyepelekeshana na chama mahakamani kwa ubunge feki au yule aliyeifanyia umafia NCCR na kuididimiza kwenye shimo halafu anakuja kupewa madaraka hapo CHADEMA halafu yeye aendelee kuwa mwanachama au shabiki mtiifu. Inatakiwa msaliti akirudi awe mwanachama wa kawaida kwa miaka mitatu au zaidi asiruhusiwe hata kuongoza msingI wa CHADEMA.
Pamoja nakuwa CCM ina madhaifu kwenye baadhi ya maeneo lakini nyie CHADEMA hebu nendeni mkajifunze namna gani CCM inadili na wasaliiti. Na kwa hili msione aibu nendeni pale Lumumba mkajifunze maana inaonekana kila siku mnarudia makosa yale yale wala hamtaki kujifunza kwa Lowasa, Sumaye na wengineo.
Ni mtizamo tu.