#COVID19 CHADEMA: Chanjo ya COVID-19 iwe ya lazima

#COVID19 CHADEMA: Chanjo ya COVID-19 iwe ya lazima

Kamanda Asiyechoka

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2020
Posts
3,315
Reaction score
5,058
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeomba huduma ya utoaji chanjo ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu, inayosababishwa na Virusi vya Corona (COVID-19), iwe ya lazima badala ya hiari kama ilivyotangazwa na Serikali.

Mbowe.jpeg

Wito huo umetolewa leo Jumatatu, tarehe 19 Julai 2021 na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, akizungumza na wanahabari jijini Mwanza.

“Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, iweke utaratibu mzuri wa chanjo kuwa ya lazima kwa Watanzania,” amesema Mbowe.

Aidha, Mbowe ameitaka Serikali iongeze juhudi katika kutoa elimu kwa wananchi juu ya kujikinga na maambukizi ya COVID-19, kwa kuwa wengi hawachukui tahadhari dhidi ya janga hilo.

“Lakini public awareness (uelewa kwa umma) haiko, wala usifikiri Watanzania hawana akili, wamedanganywa hawajui washike la rais au la nani,” amesema Mbowe.

Mbowe ameongeza “ wameweka usugu hawaogopi Corona, wanafikiri ugonjwa huu wanaambukiza wachache.”

Wakati huo huo, Mbowe ameiomba Serikali iweke mkakati wa kutoa matibabu ya COVID-19 bure kwa wananchi, kwa kuwa wengi hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu.

“Kitu kikubwa hatujakijua ni gharama za matibabu, kimsingi gharama za COVID-19 ilipaswa kusimamiwa na Serikali kwa asilimia 100,” amesema Mbowe na kuongeza:

“Sababu janga limetengazwa la kidunia na Shirika la Afya Duniani (WHO). Serikali na nchi zake zinawajibika kuwatibu na kuwakinga wananchi.”

Serikali ya Tanzania, imesema imekamilisha muongozo wa kuingiza na kutoa chanjo ya COVID-19, na kwamba zitaingizwa nchini hivi karibuni.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi, alisema chanjo hiyo itatolewa bure kwa Wananchi watakaohitaji.

Mwanahalisi
 
Bora Mafisi. Kuliko kulazimisha watu wapewe Sumu.

Ameona ajenda ya chanjo imekubalika. Ameanza stori za alinacha eti iwe lazima. Kama kapokea pesa mission failed
Ngoja nikuulize,hata ile ya polio ni hiari sio,achilia mbali pepopunda,kifaduro,kutajakwa uchache.
 
Huyu naanza kuamini kuwa anatumiwa na mabeberu. Kweli
Nchi hii kuna ufala mwingi sana, ukichunguza vizuri wanaopinga chanjo chanzo ni Gwajima alipoanza kuipinga mwaka jana, mbona chanjo zote tulizochanjwa ni za wazungu?

Kwanini tusiachane nazo?

Hebu pingeni chanjo kwa hoja za kisayansi ili tuwaunge mkono basi?
Kwani hata zile chanjo za kitoto huwa ni hiari eeeh?
 
Nchi hii kuna ufala mwingi sana, ukichunguza vizuri wanaopinga chanjo chanzo ni Gwajima alipoanza kuipinga mwaka jana, mbona chanjo zote tulizochanjwa ni za wazungu?
Kwanini tusiachane nazo?
Hebu pingeni chanjo kwa hoja za kisayansi ili tuwaunge mkono basi?
Kutengeneza baiskeli zakwetu wenyewe kunatushinda,tunakuja na porojo humu.
 
Nchi hii kuna ufala mwingi sana, ukichunguza vizuri wanaopinga chanjo chanzo ni Gwajima alipoanza kuipinga mwaka jana, mbona chanjo zote tulizochanjwa ni za wazungu?
Kwanini tusiachane nazo?
Hebu pingeni chanjo kwa hoja za kisayansi ili tuwaunge mkono basi?
Hii haijafikia viwango vya chanjo.
Chanjo gani ukichanjwa eti ndio unaugua baada ya kupokea kinga.
 
Back
Top Bottom